Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Unakataa kupeleka pesa kwenu wakati huo huo ukweni kwako wanapelekewa pesa yako kupitia mkeo!
 
Pole sana ndugu yangu. Pengine labda sehemu ulipokuwa ulikuwa unapata hela nyingi zaidi ya hizo, ila kama hukuwa na kazi inashangaza kidogo.
Ukiwa hujapata kazi unadhani ukipata ukawa na mshahara basi mambo yataenda murua, ila baada ya kuipata ndipo unagundua mshahara hautoshi.
Na huku hospitali extra duty zinaweza zisilipwe au wakalipa tatu kwa mwezi.
Ushauri wangu ni huu.
1. Acha kutuma hela nyumbani kama hamna sababu. Kabla hujapata kazi walikuwa wanaishi na hata ukifa wataishi tu. Tuma endapo kuna serious issue. Naamini wazee tayari umewakatia bima ya afya.
2. Hujasema wife yeye anaweka sh ngapi mezani. Haya maisha ni kusaidiana. Lazima wife nae achangie kwenye kuhudumia familia. Leo upo, kesho unaweza usiwepo, atatunza vipi familia? Kama hana kazi mfungulie biashara ndogo ndogo, hiyo itasaidia kucover mahitaji madogo madogo hapo nyumbani.
3. Hiyo amount itakaa bila kuongezeka kwa muda mrefu, unless mwanasiasa aingiwe huruma. Jaribu kufikiria namna nyingine ya kuingiza pesa kwenye muda ambao unakuwa hauko kwa mwajiri.
4. Mwisho lakini si kwa umuhimu, usimpeleke huyo mtoto shule ya English medium kwa hicho kipato.
 
Kama wewe unabaki na laki moja na inaisha hujui imeishaje mimi nafikri na wife usimlaumu! Shida ni moja kwako tu hutoi zaka!!
 
Hii njia na mimi nimeitumia hela inakaa aise! Sio wanawake wote wanajua kutumia hela wengi wapo rough sana! Mimi nampa kila siku
 
Kwanini ukae nyumba ya ovyo? Pesa haitoshi na haijawahi kutosha.....waza kuongeza kipato...... Kama mke hana kazi mtafutie kishughuli cha kufanya upunguze mzigo kwa kiasi

Mwambie Afanye Vyote lakini akae sehemu Safi, Inayo eleweka.

Your Environment Influence Your thoughts and Work Efficiency
 
Mshahara serikali inakulipa kwa ajili ya wewe na mkeo na watoto wako, hayo mengine tunajiwekea tu! Usije ukafanya kosa familia kutokula vizuri kisa una matumizi nyumbani!! Ushauri wangu wewe ndio unaofanya kazi unapaswa uishe vizuri na mke na watoto wafurahie kazi yako! Fanya hivyi hakikisha unga haukosi ndani alafu kila siku mwachie wife wako 10k yeye atajua mtakula nini kwa siku hiyo! Usijibine kula wali maharage na ugali, wakati kuna ndizi, viazi, tambi, chips, viazi vitamu, nk ! Fanya hivyo uone utaishi maisha murua! Mimi mshahara wangu hatutofautiani na wewe na mimi nakaa dodoma huku chumba sebule ni 130k nimeajiriwa nina miezi tano! Nina vyitu vyote ndani, friji, tv, kitanda, vyombo vya ndan, kochi nk! Natuma hela nyumbani kila mwezi zaidi ya 80k, kwa ajili matumizi mbalimbali na nina mke na watoto wawili, lakini pia nasaidia watu wengine, plus na sadaka kanisani lakini maisha yangu ni mazuri tu na naufurahia mshahara wangu!! Kikubwa ni kutumia akili kama mwanaume maisha ni the way umeyatune kama mtu analipwa 300k na anaishi vizuri kwanini wewe 600k ushindwe???
 
Umejitahidi kukumbuka njugu mawe ila wapi dengu ..watu mnadharau dengu sana
 
H
Afya ni kada ya afya na Niko hospitali ya mkoa kabisa...
1. Hongera kwa kupata ajira, hiyo ni ngazi ya kwanza.
2. Hongera kwa kubaini mahitaji makubwa ya pesa, itakurahisishia kujipanga mapema..
3. Wengi wamekushauri kupunguza matumizi kwa kukata misaada nyumbani. Kama hakuna mgonjwa, kata nusu
4. Hapo unapofanya kazi naamini kuna wateja (wahitaji huduma) wanataka huduma za express, hawahitaji kukaa kwenye line. Watafute (kwa umakini sana usije Kuhatarisha kibarua chako), hawa watakuachia 20, 30, 50 za Asante. Jenga mazoea na returning clients.....unapaswa kuwajua kwani upo kwenye kisima cha taarifa. Hawa ukiwa na ukaribu nao watakupigia simu kabla hawajaja ili wakifika uwapokee na kuwapatia huduma bila kuwasubirisha. Hawa watakuachia 30-50k. Kiufupi, namna unavyowahudumia na kuwapenda wagonjwa ndivyo utakavyoondokana na utegenezi wa mishahara.
Deal na wote, zingatia sana Wanawake (mpaka uitwe "Doctor wangu, Daktari wa family).
 
Mimi kazini natembea nafanya afya so sifanyi shift za jumatatu ijumaa Bali kuna siku nakuwa mchana kuna siku naingia asubuhi na night pia k
Kazini kwangu ni makao ni mjini ya mkoa hivyo hata Kodi zimechangamka japo ninaweza kutafuta chini ya hapo
Okay fanya kutafuta , so far mkuu wadau wameweka mawazo mengi sana --- imebakibutekelezaji tu sasa
 


Tulia hapo kwanza, ushauri wa Bure, ukikurupuka tu kwa sasa itaharibu!
 
Aiseee ....kumbe wee mke kweli.
Mammy...ndoa ipo wee andaa vilago vyako uhamie kwangu baada ya shamra shamra za harusi. Huyu sasa ndio wife material
 
Wako mjini sema watoto tulkubaliana tuwe tunatumia laki Moja kila mwezi japo Mimi nilioona Bora nifanye ushauri kama wako wa biashara na hapo yenyewe natumaga 50K Tena wanalalamika haiwatoshi
Kuna muda wazazi ndio wanaowafelisha watoto wao, sasa angalia kama wewe umeanza kazi tu hata hujajijenga mzazi anataka kukutegemea wewe kila kitu, kusaidia wazazi ni muhimu lakini sio kwa style iyo yako yaani kila mwezi na ndo umeanza kazi hapo hutoboi mkuu labda uibe kazini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…