Watumishi wa TISS huwa si maarufu, Ilikuwaje Marehemu Membe awe maarufu kwa utumishi wa TISS?

Watumishi wa TISS huwa si maarufu, Ilikuwaje Marehemu Membe awe maarufu kwa utumishi wa TISS?

Hakuna Jasusi kil.aza vile.... Yaani uwe Jasusi afu uropoke kuhusu informants waliopandikizwa Acacia? Hapo hapo akajisifia anavyodukua mawasiliano ya wakurugenzi na DC??

Ni hivi kazi kubwa kwa Jasusi ni kumaliza threats kwa usiri.... Yaani mfano Lissu wangemuua hata kwa kupandikizwa saratani n.k sio ku order SMG zitumike!! Huwezi ukawa Jasusi alafu ukafanya blunders kama hizo.

So nakataa JPM hakuwahi kuwa TISS na Hana sifa za kuwa TISS.
Hakuwahi kuwa..
 
Naomba nikujibu hivi; maafisa usalama wa kawaida ni hawa ma rso na dso na wa chini kabisa ni wale wanaosimamia mitihani ya la nne la sana form two form four na wale walioko nectar wanaotisha walimu wa Mpwayungu Village kila siku bernard camilius membe alishapita level hizo toka mwaka 1980 na kimsingi hakuwahi kuwa huko chini kwa taarifa yako wakati waziri mkuu mizengo kayanza peter pinda akiwa mkuu wa usalama wa ikulu wakati wa nyerere membe tayari alishakuwa ndani ya ofisi ya rais mchambuzi wa mifumo ya ulinzi na usalama wa nchi set up unayoiona leo nje ya nchi na ndani pokea hiyo. Itoshe kusema mizengo pinda alilinda ikulu na familia ya nyerere na membe alilinda taifa nchi !
Noted with full naked truth
 
Sio kweli wengine ni informants tu maana TISS haiwezi kuwa na mtumishi Kila eneo so inatumia wale ambao wapo huko tayari kupata taarifa. Mfano jela mnapochunguza mtuhumiwa wa kifo inaweza ikawa ngumu kumpelekea Jasusi ila ikawa rahisi kumtrain mfungwa au nyapara mbinu za kijasusi Ili apate taarifa zake kiurahisi.
Sahihi...
Tatizo ni hao informer wakijisahau huropoka mtaani. Watu hujifanya wamewajua ..
 
Jibu swali kama hao TISS ni professionals kiasi hawawezi mkosa Lissu kwa risasi niambie ilikuaje wakashindwa mlinda Ibilisi wenu Hadi akafa kizembe zembe vile?

Kituko zaidi taarifa za kifo chake zilivuja Dunia nzima huku nyie makondoo mkibisha humu Mitandaoni. Sasa hao TISS kama ni imara how did they let the information leak?

Mnachekesha sana
Ibilisi mama mkwe wako mama zitto kabwe nenda kamfukue mama mkwe wako
 
naskia marehemu Augustino Mahiga nae alikuwa TISS
Dr. Mahiga alikaimu Ukurugenzi wa Idara ya Usalama (enzi hizo kitengo cha Ikulu, kabla TISS haijaanzishwa rasmi kisheria).

Na alikuwa ni sehemu ya timu iliyopangua jaribio la kumpindua Nyerere miaka ya mwanzo ya 1980s.

Ukisoma kesi ya uhaini iliyotokana na jaribio hilo la Mapinduzi, Dr. Mahiga alikuwa shahidi aliyepewa jina la "Mr. X".

Baada ya hapo alipelekwa nje sana, Canada, Uswizi, Liberia, India, Italy, akifanyia kazi mashirika ya UN kama UNHCR na serikali ya Tanzania, kabla ya kupewa ubalozi kamili na rais Mkapa na kutumikia kama Muwakilishi wa Tanzania katika UBalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York City, kuanzia mwaka 2003, kisha akarudi kufanya kazi Umoja wa Mataifa kama Muwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa Somalia, kisha akaja kugombea urais Tanzania, na baadaye akateuliwa na Magufuli kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, kisha Waziri wa Sheria, mpaka mauti yalipomkuta.

Alivyokuwa Usalama, tukiwa wadogo, tulikuwa tunajua Mzee Mahiga anafanya kazi muhimu Ikulu, lakini hatukuwahi kujua kama alikuwa bosi wa Usalama wa Taifa.

Alijiweka kuwa kama mtu wa kawaida sana.

Mpaka alivyokuja kuw balozi alikuwa anajichanganya sana na Watanzania kwa unyenyekevu mzuri tu kama mtumishi wa serikali.
 
Membe kabla ya serikali ya awamu ya tano kumnyanyua kisiasa alikuwa afisa wa usalama wa kawaida tu hakuna cha maana sana alichokuwa amefanya zaidi ya wengine.

Unless kama umemfahamu juzi, kwa taarifa yako tu ni kuwa huyu ni koja ya seniour officers idaran toka kitambo, na kufika nafasi ya kuwa seniour officer is no joke, si kikombe cha kila mtu
 
Wako tunalewa wote viti virefu na wanaringia UTIS. Hapa kijitonyama wengine wanakuja pub na bastola zinaninginia matakoni kishamba tu! Wengi ni Maafisa Ulevi wa Taifa! Acha jasusi mbobezi ajitofautishe na hao wapuuzi!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Unless kama umemfahamu juzi, kwa taarifa yako tu ni kuwa huyu ni koja ya seniour officers idaran toka kitambo, na kufika nafasi ya kuwa seniour officer is no joke, si kikombe cha kila mtu
Hayo ni maneno tu sisi tunayemjua alikuwa junior matupu. Ndio maana hata wewe unakuja hapa na maneno tu. Niambie alikuwa Mkurugenzi wa Kurugenzi ipi hapo Idarani? Angekuwa mbobezi kama Balozi Mahiga naona mngesema sana! Balozi Mahiga pamoja na ubobezi wake lakini alikuwa very humble!!
 
Sikumbuki vizuri kama wasifu wa Mahiga walisema alikuwa TISS anaekumbuka atujuze

Balozi Agustine Mahiga na safari ya utumishi wa miaka 45 kwa Tanzania na UN
1 Mei 2020
Balozi Mahiga
CHANZO CHA PICHA, TANZANIA FA MINISTRY
Augustine Philip Mahiga, ambaye amefariki hii leo jijini Dodoma ni moja ya wanadiplomasia mahiri kuwahi kutokea nchini Tanzania.
Pia ni moja kati ya watu wachache amabao wamefanya kazi katika ngazi za juu na awamu zote tano za serikali ya Tanzania kutoka kwa rais wa kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpaka awamu hii ya rais John Pombe Magufuli.
Licha ya utajiri wake wa maarifa na uzoefu mkubwa ndani na nje ya Tanzania, Balozi Mahiga alikuwa mtu ambaye hakujikwaza kwa mamlaka yake. Na hiyo ni moja ya sifa ambayo watu wanaomuomboleza hii leo wanampamba nayo.
"Pamoja na umri wake mkubwa na uzoefu wa kushika madaraka katika nyadhifa mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa, marehemu Balozi Mahiga alikuwa mnyenyekevu na mtiifu kwa kila jukumu nilomtuma," ameeleza Rais Magufuli katika salamu zake rasmi za rambirambi.
MATANGAZO

"Upumzike kwa Amani Balozi Mahiga. Ulikuwa mtu mwema sana," ameomboleza mbunge wa upinzani nchini humo Halima Mdee kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Salamu za rambirambi pia zimetumwa kwa kutumia ukurasa wa Twitter kutoka balozi za Uingereza, Canada, Ufaransa, Sweden na Uchina nchini Tanzania zimemwagia sifa ya kuwa mwanadiplomasia mbobezi aliyewaikilisha vyema nchi yake.
Safari ya utumishi wa Mahiga inatoka mwaka 1975 mpaka umauti wake 2020
Maelezo ya picha,
Balozi Mahiga, mwanadiplomasia nguli aliyehudumu kwa miongo mitano
Je, amefanya kazi gani ndani ya Tanzania?
Mpaka umauti unamfika alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria nafasi ambayo alikuwa akihudumu toka mwezi Machi 2019.
Kabla ya hapo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje nafasi ambayo alihudumu kutoka mwaka 2016.
Mahiga pia alikuwa mbunge wa kuteuliwa na rais mpaka umauti unamkuta.
Mwaka 2015 Mahiga alikuwa ni moja ya wananchama wa CCM ambao waligombea tiketi ya kuwania urais katika kinyang'anyiro ambacho Magufuli aliibuka na ushindi.
Mahiga pia alifundisha kama Mhadhiri Mwandamizi wa Mahusiano ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baina ya mwaka 1975 mpaka 1977.
Baada ya hapo alihamia katika ofisi ya rais Ikulu akiwa kama Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo.
Kutoka mwaka 1980 mpaka 1983 akapandishwa kazi katika ofisi hiyo ya rais na kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Pia kwa vipindi tofauti katika utumishi wake amekuwa mhadhiri mtembezi katika Chuo cha Diplomasia jijini Dar es Salaam.
Mwanadiplomasia nguli
Kwa kipindi cha miaka 30 kutoka mwaka 1983 mpaka 2013 Balozi Mahiga alifanya kazi ya diplomasia akiiwakilisha nchi yake kama balozi na pia kuwakilisha Umoja wa Mataifa (UN) katika nchi mbalimbali.
Kwa miaka sita kutoka 1983 mpaka 1989 alikuwa balozi wa Tanzania nchini Canada na kutoka 1989 mpaka 1992 akahudumu katika ubalozi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi za UN jijini Geneva, Uswizi.
Kutoka mwaka 1992 mpaka mwaka 1994 alihudumu kama mwakilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi UNHCR nchini Liberia.
Kutoka 1994 mpaka 1998 alirudi Geneva na kuwa mratibu na mkurugenzi msaidizi wa Operesheni za Dharura za Wakimbizi katika eneo la Maziwa Makuu barani Afrika. Katika kipindi hicho kulikuwa na vita zilizoangamiza maisha ya makumi kwa maelfu ya watu na kuzalisha mamia ya wakimbizi kutoka nchi za Rwanda, Burundi na DRC.
Kutoka 1998 mpaka 2002 alikuwa mwakilishi mkaazi wa UNHCR India, na kutoka 2002 mpaka 2003 akawa mwakilishi wa Shirika hilo katika nchi za Italia, Malta na San Marino.
Mwaka 2003 akateuliwa na Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania Benjamin Mkapa kuwa Balozi wa Tanzania katika Ofisi za Kudumu za Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York na kusalia katika nafasi hiyo katika muhula wa kwanza wa rais wa nne wa Tanzania Jakaya Kikwete mpaka 2010.
Mwaka 2010 akateuliwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa UN kipindi hicho Ban Ki-moon kuwa mwakilishi wake maalum kwa Somalia nafasi ambayo alihudumu mpaka Juni 2013.
Mahiga amefariki akiwa na miaka 74 (amezaliwa Agosti 28 1945) na kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu kifo chake kimetokana na kuugua ghafla alfajiri ya Ijumaa Mei Mosi.
Alipata shahada yake ya kwanza ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1970, mwaka 1971 alipata shahada ya Uzamili katika Mahusiano ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Toronto na mwaka 1975 akahitimu shahada ya Uzamivu (PhD) ya Mahusiano ya Kimataifa katika Chuo hicho pia.
Waziri wa Katiba wa Tanzania Augustine Mahiga amefariki dunia alfajiri ya leo mjini Dodoma.
Taarifa iliyotiwa saini na Rais John Magufuli ilisema kuwa Mahiga aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma alfajiri ya Ijumaa, Mei mosi na alifikishwa hospitali akiwa ameshafariki.
 
Back
Top Bottom