Pascal Ndege
JF-Expert Member
- Nov 24, 2012
- 2,977
- 1,897
Kuna sheria ya utumishi wa Umma endapo mtumishi akitoka kwenye ajira yake na kuteuliwa kwenye nafasi kisiasa hata kama bado haja staafu hawezi kurudia ajira yake.
Miezi kadhaa kuna mabosi wa Chama cha Walimu walikataa katakata kutoka kwenye ajira zao na kwenda kwenye teuzi.
Mimi binafsi niliwaelewa sana, maana wangetoka kwenye ajira baadae wakafanya kosa na kutenguliwa basi hawawezi kurudi kwenye ajira zao na kuwalazimisha kuwa machawa mpaka watakapopata teuzi zingine.
Hatua hii imefanya wanasiasa wengine kujishushia heshima na utu ili tu wapate teuzi. Mfano kuna Professor alimuita Rais Mungu.
Hii mada nawaelekezea watumishi mbalimbali ambao wapo katika ajira za kisiasa hasa Wabunge na Mawaziri na Marais mfanyie marekebisho sheria hii.
Hii sheria ni ya kikoloni na kibaguzi. Unakuta Daktari mzuri kabisa au Professor mzuri lakini akiteuliwa basi ameaga R.I.P na Madini ya kichwani.
Tunaomba Wabunge na Mawaziri wenye madini lukuki kichwani badilsheni hii sheria. Kuna siku nchi itatawaliwa na vijana ambao hawajaiva kitaaluma kama akina Mkumbo, watabakia machawa kusaka teuzi.
Nawasilisha.