Watumishi wa Umma wakimaliza utumishi wa kisiasa warudi kwenye ajira zao mpaka watakapostaafu

Hakuna kitu kama hicho. sema waliogopa kumwaga mamilioni yao ya kila mwezi ndani ya hicho chama kwa kazi ya miaka mitano tena yenye kupelekeshwa na wakuu wa mikoa.
 
NAUNGA MKONO HOJA. NDIYOOOO. TUMEPANDIKIZWA IMANI POTOFU JUU YA SIASA KAMA SIASA NI KITU MBAYA HATARI KINACHOAMBATANA NA MANENO MABAYA KAMA UONGO, UCHAWI, USHIRIKINA, UUAJI, N.K. LKN SASA MBONA WENGI WANAKIMBILIA HUKO! AU WALIOHUKO WANAJILINDI WASIINGILIWE HUKO KUZURI! NCHI ZILIZOENDELEA KAMA USA WATU WOTE WANAJUA SIASA NI MAISHA NA WOTE WANAHUSIKA KIKAMILIFU. NAONA HII KUTORUHUSU NA KUWEKEANA VIGINGI KWA MTUMISHI KUINGIA KWENYE SIASA SI HAKI NA NI HADAA. KILA MTU YEYOTE HATA MCHUNGAJI KAMA ANAUWEZO NA WANANCHI WANAMTAKA INATAIWA KUSHIRIKI SIASA. KINYUME NA HAPO NDO MATATIZO HAYA SASA. KUKAMATANA, KUSHITAKIANA, UADUI BADALA YA USHINDANI, UFICHO/ USIRI BADALA YA UWAZI, CHUKI BADALA YA UPENDO, NK
 
Kuna sheria ya utumishi wa Umma endapo mtumishi akitoka kwenye ajira yake na kuteuliwa kwenye nafasi kisiasa hata kama bado haja staafu hawezi kurudia ajira yake.

Miezi kadhaa kuna mabosi wa Chama cha Walimu walikataa katakata kutoka kwenye ajira zao na kwenda kwenye teuzi.

Mimi binafsi niliwaelewa sana, maana wangetoka kwenye ajira baadae wakafanya kosa na kutenguliwa basi hawawezi kurudi kwenye ajira zao na kuwalazimisha kuwa machawa mpaka watakapopata teuzi zingine.

Hatua hii imefanya wanasiasa wengine kujishushia heshima na utu ili tu wapate teuzi. Mfano kuna Professor alimuita Rais Mungu.

Hii mada nawaelekezea watumishi mbalimbali ambao wapo katika ajira za kisiasa hasa Wabunge na Mawaziri na Marais mfanyie marekebisho sheria hii.

Hii sheria ni ya kikoloni na kibaguzi. Unakuta Daktari mzuri kabisa au Professor mzuri lakini akiteuliwa basi ameaga R.I.P na Madini ya kichwani.

Tunaomba Wabunge na Mawaziri wenye madini lukuki kichwani badilsheni hii sheria. Kuna siku nchi itatawaliwa na vijana ambao hawajaiva kitaaluma kama akina Mkumbo, watabakia machawa kusaka teuzi.

Nawasilisha.

Inaruhusiwa kurudi mkuu, Yule aliyeteuliwa kule kazini kwake anahesabika kama mtumishi aliyeazimwa kwenda kutumika mahali pengine.
 
Gladius Byakanwa alikuwa rc Lindi akaliwa kichwa.

Ameibukia kwenye ubalozi akitokea kwenye ubalozi Fulani huko Asia
 
Kuna sheria ya utumishi wa Umma endapo mtumishi akitoka kwenye ajira yake na kuteuliwa kwenye nafasi kisiasa hata kama bado haja staafu hawezi kurudia ajira yake.

Miezi kadhaa kuna mabosi wa Chama cha Walimu walikataa katakata kutoka kwenye ajira zao na kwenda kwenye teuzi.

Mimi binafsi niliwaelewa sana, maana wangetoka kwenye ajira baadae wakafanya kosa na kutenguliwa basi hawawezi kurudi kwenye ajira zao na kuwalazimisha kuwa machawa mpaka watakapopata teuzi zingine.

Hatua hii imefanya wanasiasa wengine kujishushia heshima na utu ili tu wapate teuzi. Mfano kuna Professor alimuita Rais Mungu.

Hii mada nawaelekezea watumishi mbalimbali ambao wapo katika ajira za kisiasa hasa Wabunge na Mawaziri na Marais mfanyie marekebisho sheria hii.

Hii sheria ni ya kikoloni na kibaguzi. Unakuta Daktari mzuri kabisa au Professor mzuri lakini akiteuliwa basi ameaga R.I.P na Madini ya kichwani.

Tunaomba Wabunge na Mawaziri wenye madini lukuki kichwani badilsheni hii sheria. Kuna siku nchi itatawaliwa na vijana ambao hawajaiva kitaaluma kama akina Mkumbo, watabakia machawa kusaka teuzi.

Nawasilisha.
Brigedia generali Marco Gaguti alikuwa mkuu wa Mkoa Kigoma then Kagera baadae nafikiri Lindi au Mtwara ametumbuliwa sasa hivi karudi jeshin
 
Back
Top Bottom