Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

itasaidia kwenye kujua kama kazi zitaendelea siku ya ijumaa au la kama wote wataenda kusali msikitini

Pia kuna packages za mikopo ya iddi na Christmass kwa watumishi wa umma, itasaidia taasisi za serikali kujipanga na kuzuia upigaji

Pia kuna masuala ya kijamii kama vile vifo, ndoa, haki za urithi za warithi wa marehemu katika mafao yaliyoko huko kazini

Lakini pia ili serikali iweze kuondoa udini, maana kama watu wa dini moja ndo wanaonekana wanapata hizi ajira, au wamejazana kwenye taasisi moja lazima serikali iweze kukusanya data na kujua kwa nini, hii inaweza kuifanya serikali ichukue hatua za kuaddress hilo tatizo ili harmony ipatikane katika nchi la sivyo grievances zinaweza kupelekea katika chuki na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe, naamini hutaki hilo litokee.
Moja,
Kazi hazijawahi kusimama Kwa sababu ya watu kwenda kuabudu.

Pili,
Hakuna packages za kidini, ktk utumishi wa Umma, Hapa mnataka kujenga kaburi ambalo hata urefu wake hamlijui.

Tatu,
Serikali haihusiki na mirathi na mambo ya maziko ya watumishi, haihusiki kabisa na hizo taratibu. Nakupa elimu kwa sababu inaonekana huna ufahamu na ofisi za umma.

Nne,
Hilo la malalamiko mbalimbali, aangalie ni wapi wanalalamika na aende huko kuhoji. Sio utumishi nchi nzima kujazishwa hivi. Na haielezi lengo ni nini
 
Mambo haya ni kinyume na misingi iliyoasisi taifa hili hayaruhusiwi popote pale hata kufanywa na mjumbe wa nyumba kumi;
  • Kuruudisha uchifu ambao waasisi walithibisha kwa vitendo haufai kwa mustakabali wa taifa.
  • Kurudisha utegemezi kwa mabepari ambao ni kinyume na misingi ya kujitegemea, hata kama hilo la kujitegemea ni la propaganda zaidi kuliko utekelezaji wake, sio vema kulikana hadharani mchana kwwupe.
  • Kurudisha huo ukabila na udini na uzanzibari, hata kama hausemwi lakini tunaona.
Mwalimu na Karume na wazee wenzao hawakuwa wajinga hata kama wakati wao wengi hawakuwa na elimu, wewe huwezi kuwazidi wazee wale, na akili yao ilikuwa haijachafuliwa na pollution yoyote iwe ya kimaadili ama ya vyakula, leo hii kwa sababu hatunauangalizi mkali wa misingi yetu kanaweza kuibuka kajinga fulani katika mfumo wa utawala kuanzia ngazi ya chini hata ya taifa , kalikofanya ufuska wakutosha kwa pollution za western cultures, akili yenyewe mbovu, kakaja kupinga mambo mazito kama hayo, yaani kamtu kama hako kanataka kaumbe taifa lake kenyewe na ss ndio katufanye watoto wake, kutoka kwa baba wa taifa ambae ss ni watoto wake tangu mwanzo,
Mfumo jike ni hatari sana,USA waliliona hili wakati wa ushindani wa H.Clinton na Trump.

Wanaume na wanawake ni tofauti sana ktk mental ability,tumeumbwa tofauti sana
 
Itumike huko inakotumika, mtumishi akienda kuupgrade ataelewa akiombwa hizo details, sio kuomba details kiholelaholela,
Point kubwa sana.
Na hawasemi wanaenda kuboresha nini.
Mtu yupo , umeshamuajiri, hujawahi kumtuhumu, hata sijui Dini itakusaidia kumpa nini ..
Kabila la kazi gani?
 
Itumike huko inakotumika, mtumishi akienda kuupgrade ataelewa akiombwa hizo details, sio kuomba details kiholelaholela,
Ina tegeme una fanya study kwa mtindo gani kama ni una angalia ma file ya watumishi tu?
 
Boss sio kweli mm wakati naanza ajira kuna kipengele kwenye mkataba wangu ajira za serikali kinauliza dini.Hili jambo sio jipya nashangaa kuona mleta mada analikuza kana kwamba limekuja leo.Au kwakuwa kwenye ajira za serikali ni mgeni.
Kwenda zako huko. Kuna sehemu walikuuliza kabila?
Usituletee ukabila hapa.
 
Waziri gani anahusika na huu upumbav?
Mtajeni tupeleke jina lake mbele
Taarifa za watumishi wote zitapelekwa Kwa Msajili wa Hazina.
Nafikiri ipo chini ya Wizara ya Fedha.
Hawa ndio wasimamizi wa Taasisi na mashirika ya Umma.
 
Mimi Ni mtani na mnyamwezi. Kawaambieni hao watu wa serikali tuone Kama itawasaidia kuboresha utawala huu.
Hata Magufuli pamoja na kukataa kuwapa fidia waliovunjiwa nyumba na serikali, hajawahi kuchukua kabila/dini la mtu Kama kigezo Cha kumpandisha cheo wazi wazi.
 
Ina tegeme una fanya study kwa mtindo gani kama ni una angalia ma file ya watumishi tu?
Mkuu weighing out the balance shows kuna faida kubwa kuyaacha hayo kuliko kudeal nayo, tunaweza kurudishwa mbali tulikotoka kwa njia ya shortcut, hao watu ni hatari sana kwa mistakabali wa taifa letu, can you imagine tunavyoinjoi the diversity nchi hii, tunachanganyikana makanisani, misikitini, makazini, masokoni, mashuleni mitaani , michezoni n.k jambo kubwa ambalo ss kwa kulizoea tunalichukulia poa , angalia walikolikosa kwa wenzetu limewagharimu maisha yote : uhai, uchumi , maendeleo , amani n.k
Shetani ni shetani tu hawezi kosa reason fulani ya kudanganyia ili apenyeze upuuzi wake, lazima atunge ushawishi ili akubalike,
 
Mwingira aliwahi kusema kuwa ikulu kuna shetani,I second him
Labda Kuna "invincible hand", inalipeleka Taifa letu somewhere ambako hata wao hawajui.

Ni hatari hii. Na wao wanaona kawaida.

Ujuzi, Elimu, Maarifa, Uzoefu ndio msingi wa Utendaji ktk utumishi wa Umma,

Dini na Kabila vya nini.
Tutavitumia kupandisha mshahara, au vyeo, au madaraja?

Tunalenga nini
Kusali maofisini, au kuongea kikabila!!
 
Niliajiriwa mwaka 2009, nilikutana na fomu yenye vipengele vyote hivyo. Mwaka 2019 tulitakiwa ku-update taarifa zetu kwa kutakiwa kujaza cv iliyoandaliwa serikalini na ilikuwa na vipengele vyote ninavyoviona hapo; hakukuwa na kelele wala miguno ya kidini kwa kiongozi aliyekuwepo. Kwa sasa tangu achukue nchi mama samia nimejifunza yafuatayo;

1. Samia anachukiwa sababu ya dini yake tu basi. Kila anachofanya lazima KILAZIMISHWE kuhusishwa na dini yake na kikihusishwa na dini yake basi lazima ILAZIMISHWE kuwa kapendelea dini yake. Hali haikuwa hivyo kwa mtangulizi wake aliyeleta upendeleo sio wa udini tu bali hadi ukabila.....alisifiwa na kutukuzwa huku habari ya udini wake wa wazi na ukabila hata haukusemwa! Mapungufu meeengi tunayoambiwa ya samia, ukweli uliofichika ni chuki dhidi ya dini yake tu asingekuwa dini hiyo ninaamini hata tusingesikia. Hata huyu Kikwete asiyekoma kutukanwa na kuhusishwa na utawala wa mama samia, sababu kuu ni dini yake tu. Mkapa angelikuwa hai hata usingesikia mashambulizi yoyote dhidi yake.

2. Chuki na hila za maadui kumbe huleta baraka sana; tutulie na kuwapenda tu maadui Mungu yupo na anaangalia na analipa. Nimejifunza hili kutoka kwa mwinyi, kikwete na sasa huyu mama samia. Hawa watu hukuti jema linasemwa kuhusu wao humu mitandaoni. Ni taarifa hasi tu dhidi yao kuwa hawajui kuongoza, wana udini, hawajaleta maendeleo yoyote n.k Yanasemwa hayo huku waliokuwa wadini haswa wakiachwa, wenye roho mbaya wakiachwa, wenye upendeleo wa wazi wa kikanda wakiachwa. Uungwana wao wa kuwapenda watu na kuwapa furaha kwa kuwamwagia ajira na fursa zingine unafichwa ndani huko. Lakini mwisho wa yote Mungu anawafariji kwa kuwapa umri mrefu wenye furaha na vizazi vyema vinavyochipua (sote ni mashahidi hapa).
Wakristo Wana chuki Sana na Waislamu,Cha ajabu Waislamu Wala hawawachukii wakristo!

Magufuli kweli alikuwa mdini na mkabila wakutisha,lakini Hawa kenge hatukusikia wakiliongelea humu mitandaoni,

Cha ajabu hizo chuki zao kwa viongozi wenye utu wa kiislamu,inawaongezea umri mrefu na afya tele
 
Kuna watu wanatetea wanasema ni kawaida.
Mimi najiuliza Dini, Kabila vinasaidia nini ktk utendaji wa mtumishi.?!
Tunataka kujua Kabila lake, leo, na yupo kazini miaka, tulishamuajiri kwa vigezo vya elimu, uzoefu, ujuzi,n.k.
Kabila la nini leo? Tumpandishe Cheo kwa kabila, au tupime utendaji wake kwa Dini?
Kabila na dini havina maana zaidi ya uchawi/tambiko tu na ubaguzi
 
Taarifa za dini ya mtu ni muhimu. Labda hatujakaa tufikiri vizuri tu.Mfano, watumishi wanakufa kila leo na wanahitaji huduma kwa mujibu wa dini zao. Kama serikali haina taarifa sahihi itawahudumiaje hawa watu?
Taarifa za dini sio muhimu, badala ya kulazmisha dini kwa kigezo cha kifo ni vyema hao watumishi wafundishwe kuandika wosia au wawe wanajaza fomu fupi za wakifa wanataka wazikweje.
 
Niliajiriwa mwaka 2009, nilikutana na fomu yenye vipengele vyote hivyo. Mwaka 2019 tulitakiwa ku-update taarifa zetu kwa kutakiwa kujaza cv iliyoandaliwa serikalini na ilikuwa na vipengele vyote ninavyoviona hapo; hakukuwa na kelele wala miguno ya kidini kwa kiongozi aliyekuwepo. Kwa sasa tangu achukue nchi mama samia nimejifunza yafuatayo;

1. Samia anachukiwa sababu ya dini yake tu basi. Kila anachofanya lazima KILAZIMISHWE kuhusishwa na dini yake na kikihusishwa na dini yake basi lazima ILAZIMISHWE kuwa kapendelea dini yake. Hali haikuwa hivyo kwa mtangulizi wake aliyeleta upendeleo sio wa udini tu bali hadi ukabila.....alisifiwa na kutukuzwa huku habari ya udini wake wa wazi na ukabila hata haukusemwa! Mapungufu meeengi tunayoambiwa ya samia, ukweli uliofichika ni chuki dhidi ya dini yake tu asingekuwa dini hiyo ninaamini hata tusingesikia. Hata huyu Kikwete asiyekoma kutukanwa na kuhusishwa na utawala wa mama samia, sababu kuu ni dini yake tu. Mkapa angelikuwa hai hata usingesikia mashambulizi yoyote dhidi yake.

2. Chuki na hila za maadui kumbe huleta baraka sana; tutulie na kuwapenda tu maadui Mungu yupo na anaangalia na analipa. Nimejifunza hili kutoka kwa mwinyi, kikwete na sasa huyu mama samia. Hawa watu hukuti jema linasemwa kuhusu wao humu mitandaoni. Ni taarifa hasi tu dhidi yao kuwa hawajui kuongoza, wana udini, hawajaleta maendeleo yoyote n.k Yanasemwa hayo huku waliokuwa wadini haswa wakiachwa, wenye roho mbaya wakiachwa, wenye upendeleo wa wazi wa kikanda wakiachwa. Uungwana wao wa kuwapenda watu na kuwapa furaha kwa kuwamwagia ajira na fursa zingine unafichwa ndani huko. Lakini mwisho wa yote Mungu anawafariji kwa kuwapa umri mrefu wenye furaha na vizazi vyema vinavyochipua (sote ni mashahidi hapa).
Umeongea fact mkuu!
 
Mkuu weighing out the balance shows kuna faida kubwa kuyaacha hayo kuliko kudeal nayo, tunaweza kurudishwa mbali tulikotoka kwa njia ya shortcut, hao watu ni hatari sana kwa mistakabali wa taifa letu, can you imagine tunavyoinjoi the diversity nchi hii, tunachanganyikana makanisani, misikitini, makazini, masokoni, mashuleni mitaani , michezoni n.k jambo kubwa ambalo ss kwa kulizoea tunalichukulia poa , angalia walikolikosa kwa wenzetu limewagharimu maisha yote : uhai, uchumi , maendeleo , amani n.k
Shetani ni shetani tu hawezi kosa reason fulani ya kudanganyia ili apenyeze upuuzi wake, lazima atunge ushawishi ili akubalike,
Point kubwa:

Kuna faida kubwa sana kuacha kuulizana Dini na Kabila, kuliko kuyadadisi.

Unataka upate tija gani ktk utendaji wa mtumishi?

Au tusalishane maofisini, au tuongee kikabila.
 
Back
Top Bottom