Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Habari wana JF ..

Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata
Waasisi wa "Génocidaires" huko Rwanda, Burundi, Yugoslavia, Myanimar, Germany na kwingineko walianza mdogo mdogo kwa kuweka vigezo vyenye viashiria vya kibaguzi kwenye taasisi wanazozimudu, kisha kufanya "Lobbing" kwenye taasisi nyingine nyeti ngumu kwa kuwalainisha viongozi wa juu ili azma Yao itimie..

Ngondo itakuja pale wale wanaohujumiwa watakapoanza kujipanga kujibu mapigo.....

Kama kuna harakati hizo za hovyo zinaendelea, zikomeshwe mara moja kabla ya mambo kuharibika.
 
Mambo mengine ni ya kipumbavu kwa wajinga
Mimi ni mimi niulize mimi na kosa nikifanya ni mimi
Hiyo sheria ya kuuliza majina matatu ya mzazi ipo wapi duniani kama sio kwetu tu

Hawajui kuwa wengine hawawajui wazazi wao?
Wengine hata kabila hawajui unataka adanganye?
Acheni kabisa ujinga huu
Kuna watu wanatetea wanasema ni kawaida.
Mimi najiuliza Dini, Kabila vinasaidia nini ktk utendaji wa mtumishi.?!
Tunataka kujua Kabila lake, leo, na yupo kazini miaka, tulishamuajiri kwa vigezo vya elimu, uzoefu, ujuzi,n.k.
Kabila la nini leo? Tumpandishe Cheo kwa kabila, au tupime utendaji wake kwa Dini?
 
Nahisi utakuwa unahusika na zile meseji za "ndagu" na "tuma kwa namba hii" kwenye hiki kiswaswadu changu.
 
Waasisi wa "Génocidaires" huko Rwanda, Burundi, Yugoslavia, Myanimar, Germany na kwingineko walianza mdogo mdogo kwa kuweka vigezo vyenye viashiria vya kibaguzi kwenye taasisi wanazozimudu, kisha kufanya "Lobbing" kwenye taasisi nyingine nyeti ngumu kwa kuwalainisha viongozi wa juu ili azma Yao itimie..

Ngondo itakuja pale wale wanaohujumiwa watakapoanza kujipanga kujibu mapigo.....

Kama kuna harakati hizo za hovyo zinaendelea, zikomeshwe mara moja kabla ya mambo kuharibika.
Kuna watu wanatetea hili.
Nashangaa sana.

Nimewaambia jambo moja. TAIFA halijengwi kwa matofali, zege, na nondo.

Mnapalilia msioyajua.
 
Kuna watu wanatetea wanasema ni kawaida.
Mimi najiuliza Dini, Kabila vinasaidia nini ktk utendaji wa mtumishi.?!
Tunataka kujua Kabila lake, leo, na yupo kazini miaka, tulishamuajiri kwa vigezo vya elimu, uzoefu, ujuzi,n.k.
Kabila la nini leo? Tumpandishe Cheo kwa kabila, au tupime utendaji wake kwa Dini?

Labda hawataki tena kuwapa kazi wenye asili za nchi jirani
Ila sijui nimewaza tu
 
Mbona mahakamani police unaulizwa dini yako kabla ya kutoa ushahidi au maelezo uhoji inasadia ata wkt wa teuzi kubwa kujua ili wakt wa kiapo usimpe shida k/kiongozi akupe kitabu gani msaafu au biblia wkt wa kuapa au ata utakapokufawajue uzikwe kwa dini gani au uandaliwe kwa dini gani
 
Hahahaha lkn Samia yeye ni Mzanzibari hana Kabila, ila ninyi backward, uncivilized tribes mnapangwa kwa Makabila mkapige ramli na kuzindika.
 
Mbona hii Document nilijaza mwaka ambao nilihamia Taasisi/Shirika la Umma ila sikumbuki kama nilijaza wakati naajiriwa ajira ya kwanza Halmashauri.
 
Ukishamjua Dini yake, ndio utendaji wake na ujuzi kazini unaongezeka?
itasaidia kwenye kujua kama kazi zitaendelea siku ya ijumaa au la kama wote wataenda kusali msikitini

Pia kuna packages za mikopo ya iddi na Christmass kwa watumishi wa umma, itasaidia taasisi za serikali kujipanga na kuzuia upigaji

Pia kuna masuala ya kijamii kama vile vifo, ndoa, haki za urithi za warithi wa marehemu katika mafao yaliyoko huko kazini

Lakini pia ili serikali iweze kuondoa udini, maana kama watu wa dini moja ndo wanaonekana wanapata hizi ajira, au wamejazana kwenye taasisi moja lazima serikali iweze kukusanya data na kujua kwa nini, hii inaweza kuifanya serikali ichukue hatua za kuaddress hilo tatizo ili harmony ipatikane katika nchi la sivyo grievances zinaweza kupelekea katika chuki na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe, naamini hutaki hilo litokee.
 
Unaweza kukuta ata hakuna cha maana wanachoenda kufanya na hizo taarifa.wanaacha kuboresha maslahi ya watumishi wao kazi kujaza madocument yasiyo na msingi.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hizo ni nadharia tu za ndoa za boma lakini sababu ya uwepo wa ndoa za serikali ni kwa sababu tu wazazi wa Amina wamekataa kufungisha ndoa ya binti yao kwa Peter na hivyo amina peter kuhalalisha ufuska na ukaidi wao kwa wazazi wameamua kwenda kwa baraza la wilaya ili kuruhusiwa waishi kama mama na baba kwa wanao.
Hizi dini na makabila yapo kikanda na wilaya. Mfano Ruvuma Mbinga wakristo na wamatengo, Songea wakristo na wangoni, Namtumbo waisilamu na wandendeule, Tunduru Waisilamu na wayao. Umkute mmatengo muisilamu lazima akupe sababu kwa nn yeye muisilamu hivyo hivyo ukikutana na Myao mkristo lazima akupe sababu ya yy kuwa mkristo. Leo hii ukienda Mbeya wanyakyusa waisilamu wapo ila wachache sana na wanasababu za kuwa huko ila 98% wakristo.
Sababu hizo zinazotolewa kwa sababu tu sio athiri yao kuwa dini hizo. Tanzania dini zipo na makabila yapo na ukitaka idadi nitakupa
Umeandika ujinga mtupu
 
Habari wana JF ..

Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata kufikiri yanaweza kufanyika kwa karne hii.

Mimi niwaombe Serikali, niwaombe CCM, niwaombe washauri wa Rais, kama mmechoka, mtuachie hili Taifa.
Wengine bado tunataka kuliona Taifa letu likiwa moja.

Vyombo vya usalama, basi mshaurini mheshimiwa Rais vizuri, msijisahau sana mkaiacha nchi kwenye auto-pilot.
Niwakumbusheni Taifa hili halikujengwa kwa matofali, la hasha!

Mpitisheni Mh. Rais katika historia ndogo ndogo zile njema, zilizotufanya Watanzania japo tukawa wamoja, potelea pote na umaskini wetu.

Sasa hamuwezi amini, leo hii Hazina inaomba taarifa za watumishi (CV), na miongoni mwa taarifa wanazotakiwa kujaza hao watumishi ni:-
1. Kabila lako .....
2. Dini yako .......

Zipo taarifa zingine, za kipuuzi zinazoombwa, ila haina haja sana kuzitaja, kwani hazina athari sana kama hizi mbili.

Hivi kweli, leo mnataka DINI ya mtumishi, iwasaidie nini?
Hii taarifa mnaitumia kuboresha nini?
Udini wa nini katika Tz ya leo.
Tuna ajenda gani na Dini za watu, (watumishi). DINI, DINI.....DINI...!!!!?....,leo tunauliza DINI yako ni ipi? Kweli mh. Rais Samia.

Halafu mnataka na KABILA, kabila la mtumishi litumike kuboresha nini?
Mna ajenda gani huko?

KABILA, leo mnamuuliza mtu KABILA. Kweli mh Rais Samia , ulisema wewe huna kabila, sijui ni Mzanzibar, sasa hawa watumishi, karne ya 21, mwaka 2022, wawajazie makabila yao, muyajue, myafanyie nini?!

Mh Rais Samia, hebu kataa mambo mengine.

Siku Taifa hili likiparaganyika mikononi mwako, hao unaowaona, watakukataa.

Mfumo wa CV (format) na taarifa zinazotakiwa nimeambatanisha hapa.
denooJ , MTAZAMO , barafu , Tindo , Chige , shige2 , Malcolm X5 , MALCOM LUMUMBA ,

View attachment 2095758
Hatari hii🙄
 
Labda wanataka kutambika. Mimi nasubiria mei mosi mama aseme kitu kuhusu ongezeko la mtonyo.....
 
Back
Top Bottom