Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Moja,
Kazi hazijawahi kusimama Kwa sababu ya watu kwenda kuabudu.

Pili,
Hakuna packages za kidini, ktk utumishi wa Umma, Hapa mnataka kujenga kaburi ambalo hata urefu wake hamlijui.

Tatu,
Serikali haihusiki na mirathi na mambo ya maziko ya watumishi, haihusiki kabisa na hizo taratibu. Nakupa elimu kwa sababu inaonekana huna ufahamu na ofisi za umma.

Nne,
Hilo la malalamiko mbalimbali, aangalie ni wapi wanalalamika na aende huko kuhoji. Sio utumishi nchi nzima kujazishwa hivi. Na haielezi lengo ni nini
 
Mfumo jike ni hatari sana,USA waliliona hili wakati wa ushindani wa H.Clinton na Trump.

Wanaume na wanawake ni tofauti sana ktk mental ability,tumeumbwa tofauti sana
 
Itumike huko inakotumika, mtumishi akienda kuupgrade ataelewa akiombwa hizo details, sio kuomba details kiholelaholela,
Point kubwa sana.
Na hawasemi wanaenda kuboresha nini.
Mtu yupo , umeshamuajiri, hujawahi kumtuhumu, hata sijui Dini itakusaidia kumpa nini ..
Kabila la kazi gani?
 
Itumike huko inakotumika, mtumishi akienda kuupgrade ataelewa akiombwa hizo details, sio kuomba details kiholelaholela,
Ina tegeme una fanya study kwa mtindo gani kama ni una angalia ma file ya watumishi tu?
 
Boss sio kweli mm wakati naanza ajira kuna kipengele kwenye mkataba wangu ajira za serikali kinauliza dini.Hili jambo sio jipya nashangaa kuona mleta mada analikuza kana kwamba limekuja leo.Au kwakuwa kwenye ajira za serikali ni mgeni.
Kwenda zako huko. Kuna sehemu walikuuliza kabila?
Usituletee ukabila hapa.
 
Waziri gani anahusika na huu upumbav?
Mtajeni tupeleke jina lake mbele
Taarifa za watumishi wote zitapelekwa Kwa Msajili wa Hazina.
Nafikiri ipo chini ya Wizara ya Fedha.
Hawa ndio wasimamizi wa Taasisi na mashirika ya Umma.
 
Mimi Ni mtani na mnyamwezi. Kawaambieni hao watu wa serikali tuone Kama itawasaidia kuboresha utawala huu.
Hata Magufuli pamoja na kukataa kuwapa fidia waliovunjiwa nyumba na serikali, hajawahi kuchukua kabila/dini la mtu Kama kigezo Cha kumpandisha cheo wazi wazi.
 
Ina tegeme una fanya study kwa mtindo gani kama ni una angalia ma file ya watumishi tu?
Mkuu weighing out the balance shows kuna faida kubwa kuyaacha hayo kuliko kudeal nayo, tunaweza kurudishwa mbali tulikotoka kwa njia ya shortcut, hao watu ni hatari sana kwa mistakabali wa taifa letu, can you imagine tunavyoinjoi the diversity nchi hii, tunachanganyikana makanisani, misikitini, makazini, masokoni, mashuleni mitaani , michezoni n.k jambo kubwa ambalo ss kwa kulizoea tunalichukulia poa , angalia walikolikosa kwa wenzetu limewagharimu maisha yote : uhai, uchumi , maendeleo , amani n.k
Shetani ni shetani tu hawezi kosa reason fulani ya kudanganyia ili apenyeze upuuzi wake, lazima atunge ushawishi ili akubalike,
 
Mwingira aliwahi kusema kuwa ikulu kuna shetani,I second him
Labda Kuna "invincible hand", inalipeleka Taifa letu somewhere ambako hata wao hawajui.

Ni hatari hii. Na wao wanaona kawaida.

Ujuzi, Elimu, Maarifa, Uzoefu ndio msingi wa Utendaji ktk utumishi wa Umma,

Dini na Kabila vya nini.
Tutavitumia kupandisha mshahara, au vyeo, au madaraja?

Tunalenga nini
Kusali maofisini, au kuongea kikabila!!
 
Wakristo Wana chuki Sana na Waislamu,Cha ajabu Waislamu Wala hawawachukii wakristo!

Magufuli kweli alikuwa mdini na mkabila wakutisha,lakini Hawa kenge hatukusikia wakiliongelea humu mitandaoni,

Cha ajabu hizo chuki zao kwa viongozi wenye utu wa kiislamu,inawaongezea umri mrefu na afya tele
 
Kabila na dini havina maana zaidi ya uchawi/tambiko tu na ubaguzi
 
Taarifa za dini ya mtu ni muhimu. Labda hatujakaa tufikiri vizuri tu.Mfano, watumishi wanakufa kila leo na wanahitaji huduma kwa mujibu wa dini zao. Kama serikali haina taarifa sahihi itawahudumiaje hawa watu?
Taarifa za dini sio muhimu, badala ya kulazmisha dini kwa kigezo cha kifo ni vyema hao watumishi wafundishwe kuandika wosia au wawe wanajaza fomu fupi za wakifa wanataka wazikweje.
 
Umeongea fact mkuu!
 
Point kubwa:

Kuna faida kubwa sana kuacha kuulizana Dini na Kabila, kuliko kuyadadisi.

Unataka upate tija gani ktk utendaji wa mtumishi?

Au tusalishane maofisini, au tuongee kikabila.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…