Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Huna hoja za msingi sasa CV ni taarifa za mtu binafsi kwanini ufiche taarifa zako kama dini na kabila jambo ambalo ni muhimu sana., acheni ujinga nyi majinga mafomu mangapi tunajaza Online nchi kibao duniani zinataka kujua dini yako? mbona hukuhoji kuhusu Umri na tarehe za kuzaliwa? maana nao kwa mujibu hoja zako pia unaweza kuleta ubaguzi wa Kiumri.

Polisi wakitukamata mabarabarani zile bondi zao zinakuuliza dini yako na kabila pia kwanini humuulizi kamanda Siro kwanini bondi zenu zina masuala ya makabila?

Nadhani ni hoja dhaifu sana tupa kule kwa dustbin., Kengee

Mbona hoja hii waislamu huwa hawaileti siku zote zinaletwa na wakiristo tu? hofu yenu ni nini hasa nyie wakiristo na dini yenu?

Mimi naiomba Serikali pia kwenye sensa inayokuja pia kuwe na hili suali kuhusu dini ili Nchi ijuwe waislamu wangapi na wakiristo wangapi lakini kama kuna ambao hawana dini pia ni wangapi

Si lazima kila wakati uje hapa na kuandika tu chochote.,
 
Acha ujinga wako! Wakristo ulishawahi kuwakuta wanahangaika na kujadili waislam? Nyingi ndo kila siku mnafundishwa chuki juu ya wakristo!
 
Kwani wewe unapata shida gani hizo taarifa zikichukuliwa? - Kwa nini huoni ajabu taarifa za jinsia kuchukuliwa, wewe unadhani jinsia yako inaisadia nini serikali?

Lengo la Taarifa hizi ni ili serikali iweze kuondoa ubaguzi katika utumishi wa umma, au hujui kuwa rais ameapa kutimiza majukumu yake bila upendeleo wa dini, kabila au jinsia? —Hizi data zinasaidia serikali kusolve ishu ya inequalities katika utumishi wa umma, ili keki ya Taifa isiliwe na watu wa mrengo mmoja, ni hatarisana kama inaonekana watu wa dini moja ndo wana fursa halafu wengine hola
 
Ndugu yangu, jamaa anasema tuache kazi apate kazi, sijui anamaanisha nini .

Leo Kila sehemu tukianza kuulizana Dini na Kabila, tutakuwa na Taifa kweli.!
Kuna wengine wanasema et, unaweza ukaweka Dash, kwa maana ukaacha wazi sehmu ya kabila na dini. Hawajui kwamba huyu mtu anayetaka kuwatambua waatu kwa makabila na dini zao, hiyo dash au usipojaza uakuwa unaongezea ama kupunguza nini upande upi. Na hujui hiyo dash ina maanisha nini katika kutimiza agenda zake za kidini na kikabila anazotaka kuzisimika.
 
Dini au kabila ni maumbile kwamba mtu hawezi kujibadilisha na hvyo anahitaji kuzingatiwa kwa jinsi alivyo? Huo ndio upumbavu tunaousema wa kuwa na watu wasio na eliimu sahihi wala exposure. Magari ya ukabila na udini yalishaondolewa barabarani. Tuko kwenye globalization error halafu ninyi maaanza kutafuta ujinga wa kuturudisha kule dunia ilishaatoka. Pumbavu sana.
 
Hakuna kitu kinachoitwa 'mfumo kristu' kwenye hili taifa........hizo ni kampeni za kueneza chuki, fitina na hila ovu dhidi ya kundi fulani la ki-imani.
Tena
Huyu 2025 inabidi aende likizo. Atatuharibia undugu wetu tuliojiwekea kwa ujinga wa siasa za kishamba.
 
Data na information yoyote ya mambo ya kijamii ni muhimu kwa serikali. Inasaidia serikali kwenye mambo mengi ikiwemo affirmative action ikibidi au kwenye kuzuia udini na ukabila kwenye ajira.
 
Du hata kwenye sensa kipengele cha dini na kabila halipo,kwa kuamini Tanzania haina udini na ukabila, hata ukitaka kufanya tafiti mojawapo ya masharti ya kupitishwa kwa dodoso la utafiti ni kutokuweka kipengele cha dini na kabila.
 
Waandishi wa habari nchi hii hopeless kabisa zingekuwa nchi zingine zilizoendelea wangekuwa wangemshukia kama mwewe kuhoji waziri wa fedha au Raisi

Naomba BBC wamhoji raisi ukabila na udini wa mini na motive ya hii kitu ni nini?

BBC hojini Rais hilo
 
Labda wanahisi wengine wamebadiri DINI
 
Nahisi kama kuna kundi linatakiwa kuwa eliminated kabisa ndani ya nchi. Kwa kuwa nia ya kukusanya tawkimu kwa majina binafsi haijawekwa wazi, ninahisi kama sasa wasiotakiwa wataanza kuwa replaced, frustrated ama sidelined na kuawa kabisa ili agenda inayofukuziwa ifikiwe.

Huu ni wasiwasi mkubwa unaosababishwa na haya mambo ya ajabu yanayotokea katika kipindi cha uharifu ufiohojiwa wala kutolewa maelezo.
Ninapata wasiwasi na usalama wa hao kundi lililo kwenye black list.
 
Huku kwenye taaluma yetu hiyo ni criteria ingawa it is qualified not absolute. Na imeisaidia sana Mahakama kufikia maamuzi ya haki mara kadhaa.

Nikuongezee mfano mwingine wa kwenye kesi za udhalilishaji (defamation). Kuna kabila mtu akikutamkia neno flani linakuwa ni udhalilishaji kwa kabila hilo, lakini kwa kabila lingine ni utani. Kwahiyo wafanya maamuzi wa Mahakama wanapaswa kulizingatia hili kabla ya kufanya maamuzi, vinginevyo watu watawajibishwa/kutowajibishwa kimakosa halafu mrudi humu kulalamika.

Hivyo ni lazima uelewe kwamba kwenye baadhi ya maeneo ni lazima ubainishe kabila lako kwa dhumuni jema kabisa ambalo huenda likakusaidia wewe mwenyewe.
 
kuna kale ka msemo ukielimisha mwanamke, umeelimisha jamii...nadhani kwa tz inatakiwa kafutwe
 
Kama tuvoyapinga huko serikali tuyapinge vile vile kwenye sekta binafsi...
Taarifa nyeti kama umri, jinsia, dini, kabila, makazi, pakuzaliwa, hali ya ndoa, taarifa za wazazi, mtu wa karibu... zote hizo zinatakiwa kuwa hiyari na siri.
Na ukizitoa ni vizuri kujiridhisha zitatumikaje...
 
Angalia baraza la mawaziri juzi, waliopigwa chini wote ni wakristu na replacement yake utapata jibu
 
Kwa uzoefu wangu hizi taarifa sio mpya kwenye utumishi wa umma, unapoajiriwa kwa mara ya kwanza taarifa hizo huwa zinachukuliwa kupitia fomu flani ambayo mtumishi huwa anajaza. Pia, kama upo Wizarani na umefanyiwa vetting, taarifa za ajabu ajabu kama hizo huhitajika ikiwemo hadi details za wakwe zako na dada na kaka wa mkeo. Mimi kwangu cha kushangaza, kwanini wanazitaka hivi sasa wakati tayari taarifa hizo zote wanazo? Ni uvivu wa kupekua nyaraka au?
 
Wakristo mbona mna hofu Sana,au kwakuwa mmejazana kwenye maofisi mnajishtukia, muacheni Rais apige kazi,hizi kelele mngezipiga kipindi kile Cha dikteta
Waislamu akishika uraisi muislamu mwenzao wanamsumbua sana Raisi kwa hoja za kuokoteza

Mfano angalia Mwinyi alipokuwa Raisi akamuweka Kighoma Malima mwislamu mwenzie kuwa waziri wa Elimu Malima akasema ohhh waislamu shule zao zinafeli sana sababu wasahihishaji mfumo kristu wakiona mtoto jina LA kiislamu wanamfelisha kwa makusudi zitumike namba tu za mitihani sio majina .Wakristo wakakubali Leo hii shule za kiislamu bado zinashika mkia wanafeli hasa Likiwemo somo lao LA Islam Knowledge linalofundishwa na ma ustaadhi na kusahihishwa na maustaadhi wenyewe

Leo wanataka Dini na kabila viwekwe wazi isiwe siri !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…