Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Kwahiyo ukibadili dini unaenda kubadili tena taarifa zako? Na sie wengine hatujui ni kabila gani ukiniuliza kabila nakutajia lolote tu nitakalojisikia.
 
Kama vile wako immigration office wanajaza fomu za kuomba passport
 
Hamna mtu amewahi kufanya kwenye Serikali yetu asitoe hizo taarifa. Acha kazi tu kujiepusha na hilo kama hupendi. Kumbuka hata Polisi ukienda wakaandika taarifa zako zozote, za kushtaki au kushtakiwa, na hilo wataandika. Tena wale wanaandika kwenye counter book kwa herufi kubwa tupu 😀
 
Msiwe mnaongea vitu bila kujua maana yake. Polisi wanauliza kabila au dini maana makosa ya jinai yanaweza kufanyika kutokana na mila za watu au dini ya mtu. Mfano Mjahidina wanaona ni fahari kujitoa mhanga. Hospitali wanauliza kabila kwa vile magonjwa mengine ni ya kurithi au yanasababishwa na imani. Mfano ulaji wa vyakula fulani. Je, umuhimu wa kabila na Dini kiserikali ni upi, kama si kwa ajili ya kubaguana?
 
Kweli kabisa hii ni mbaya. Mie kwenye Dini na Kabila nimeacha blank!
 

Haya anayofanya Samia yanaweza Kuleta matataizo ya ukabila ambao umeishaanza kuota mizizi na ndio maana unasikia makundi kama SUKUMA GANG , CHAGAs etc. na hii sio ishara nzuri!! Huu ni Mwanzo ambao mwisho wake unaweza kuleta vita ya wenyewe kwa wenyewe kitu ambacho nchi imeweza kukiepuka kwasababu ya misingi iliyowekwa ya umoja!!!
Wazee wa ccm acheni njaa yenu na kuwa wanafiki kwa kukaa kimya na kumuacha Samia anafanya mambo ya kuigawa nchi kwa misingi ya ukabila ambao unaweza kulisambaratisha Taifa!! Mlikaa kimya wakati Magufuli anainajisi katiba kwa vitendo vyake viovu na baadae kuja kumlaumu baada ya kifo chake, na inaelekea mnamuonea aibu Samia wakati anafanya mambo ya hatari kwa Taifa. Huo sio uzalendo hata siku moja ni uhaini!!
 
Kama huo mfumo upo,hawawezi kuuvunja,japo sina hakika kama huo mfumo upo.
 
Baba wa Taifa ktk moja ya hotuba zake zenye upeo wa juu sana, alisema suala la kujua Dini za Watanzania, waachiwe Maaskofu na Mashehe huko Makanisani na Misikitini. Na pia alisisitiza kuhsu Ukabila, na kusema ktk mipango ya Serikali au Utumishi wake, masula ya DINI na UKABILA hayana mashiko kuyajua. Alisisitiza, wanao-angaliwa ni WATANZANIA.

Sasa hao wanaotaka kujaribu kumwaga kimiminika cha Petrol kwenye moto...acha waendelee...
 
Sasa mbona serikali yake ilikuwa inataka kujua jinsia ya mtu ilitaka kuchumbia?
 
Kwenye rekodi za ajira wanaweka mpaka kabila la mtu, dini, kijiji anachotokea, mtu maarufu kijijini kwao n.k

Walioajiriwa wanajua hili. Hiyo ni mwanzoni kabisa wakati faili linafunguliwa.

Acheni kupotosha watu
Unadhani jambo hili lina tija ?
 
HAKUNA Mfumo Kristo Tanzania ni nadharia ya kipumbavu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…