Shige2,
Nilikutana na takwimu hizo za CIA katika mhadhara niliofanya University of Iowa, Marekani.
Nilielezwa kuwa magawanyo wa nafasi Tanzania ni lazima Waislam wawe wachache kwa kuwa wao ni wachache.
Mimi nilikuwa na takwimu zangu za ''religious didtribution,'' lakini Wamarekani wanaziamini takwimu zao za CIA.
Nikawaomba Wamarekani wanipe mfano wa nchi moja duniani ambayo imevamiwa na wakoloni kutoka nje na waliosimama kunyanyua silaha na kupigana na wavamizi wakawa ni wale wachache.
Hapa nikatoa mfano wa Vita Vya Maji Maji na jinsi Waislam walivyosimama kupambana na ukoloni wa Wajerumani 1905 - 1907.
Kwa bahati katika hadhira ile alikuwapo Prof. James Giblin ambae ni Prof. wa History na ameandika kitabu kuhusu Vita Vya Maji Maji.
Niliieleza hadhira ile kuwa Vita Vya Maji vina historia kubwa na Waislam na kumbukumbu yao ipo Kilwa na Mahenge Songea.
Huko ndiko yalipo makaburi ya Abdulrauf Songea Mbano na Khadija Mkomanile majemadari walionyongwa na Wajerumani juma yao 67 na wote Waislam.
(Wanahistoria wetu haya majina ya Kiislam hawayataji utasoma Songea Mbano na Mkomanile.
Majina ya Kiislam wanayakwepa).
Nikauliza tena hadhira yangu yangu kuwa hao wengi walikuwa wapi wasitoke na jeshi kupambana na wavamizi wa nchi yao?
Nikaingia katika ''nationalist politics,'' somo ambalo Wamarekani ni bingwa.
Nikauliza hadhira yangu historia yote ya kupigania uhuru wa Tanganyika nani waliokuwa mstari wa mbele?
Jibu liko wazi na kitabu changu, The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' wanakitumia kama kitabu cha rejea.
Hao wanaoelezwa na CIA Fact Book kuwa ndiyo wengi walikuwa wapi wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika?
Mbona wingi wao haukuonekana?
Nikawaomba watoe mfano wa nchi moja tu duniani ambako wachache walisimama kuikomboa nchi yao.
Ukumbi ulikuwa kimya.
Hapakuwa na jibu.
Takwimu za CIA hazikuweza kujibu haya maswali yangu.
Wamarekani wanajidai sana kuwa wao wanajua kila kitu.
Si kweli.
Ukikaanao utawajua vyema kuwa yapo mengi hawajui.
Majibu yangu haya nilikuja kuelezwa baadae kuwa yalipitishwa kwingi kutaka kujua kama kuna nchi ambayo ''minority,'' ndiyo walioongoza harakati za kupigania uhuru.
Haikupatikana hata nchi moja.
Ukweli ni kuwa siku zote wale wengi ndiyo wanaokuwa na nguvu ya kupambana na adui na wengine huwa nyuma kuongeza nguvu.
View attachment 2098840
Prof. James Giblin na kitabu cha Abdul Sykes
Ukitaka kujifunza zaidi kuhusu somo hili ingia hapo chini:
mubindi said: ↑ Kwani sida ni nini hapo. Mahali fulani imeandikwa waungwana huchunguza. Naona watu wanabisha halafu hawana hizo t...
mohamedsaidsalum.blogspot.com