Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Huku kwenye taaluma yetu hiyo ni criteria ingawa it is qualified not absolute. Na imeisaidia sana Mahakama kufikia maamuzi ya haki mara kadhaa.

Nikuongezee mfano mwingine wa kwenye kesi za udhalilishaji (defamation). Kuna kabila mtu akikutamkia neno flani linakuwa ni udhalilishaji kwa kabila hilo, lakini kwa kabila lingine ni utani. Kwahiyo wafanya maamuzi wa Mahakama wanapaswa kulizingatia hili kabla ya kufanya maamuzi, vinginevyo watu watawajibishwa/kutowajibishwa kimakosa halafu mrudi humu kulalamika.

Hivyo ni lazima uelewe kwamba kwenye baadhi ya maeneo ni lazima ubainishe kabila lako kwa dhumuni jema kabisa ambalo huenda likakusaidia wewe mwenyewe.
Unachanganya baina ya matumizi ya maeneo na kabila. Hoja yako naona ina msingi kwa kuegemea kwenye eneo lakini sio kabila; kwasababu kinacholeta tofauti baina ya makundi ya watu ni mazingira sio kabila lake. Anyway, tusonge mbele.
 
Kichuguu,
Hizo takwimu hapo chini zinatoka katika Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania.
Uliwekwa kwa madhumuni ya kuwazindua Watanzania hali iliyoko nchini:

''Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mwaka (2015), Rais alifanya uteuzi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi mbalimbali. Uteuzi wake ulikuwa kama ifuatavyo:

Mawaziri na Manaibu: 30.

Waislamu 10, sawa na asilimia 33%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 67%.

Makatibu Wakuu na Manaibu: 50.

Waislamu 10, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 40, sawa na asilimia 80%.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya: 166.

Waislamu 41, sawa na asilimia 25%.

Wakristo 125, sawa na asilimia 75%.

Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya: 163.

Waislamu 24, sawa na asilimia 15%.

Wakristo 139, sawa na asilimia 85%.

Wakurugenzi mbalimbali: 249.

Waislamu 45, sawa na asilimia 18%.

Wakristo 204, sawa na asilimia 82%.

Manaibu Kamishna wa Polisi: 25.

Waislamu 5, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 80%.

Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi: 33

Waislamu 7, sawa na asilimia 21%.

Wakristo 26, sawa na asilimia 79%.

Jumla Kuu ya Uteuzi:

Waislamu asilimia 20%.

Wakristo asilimia 80%.

Uteuzi huo umekuwa kama Sera kwa teuzi zinazoendelea ndani ya miaka yote mitano. Vilevile kama Mwongozo kwa wateule wenye mamlaka ya kuteuwa. Mwelekeo huo unakinzana na Katiba ya nchi ibara ya 13(4)(5), inayokataza ubaguzi wa aina zote. Kwa hakika Taifa halihitaji kiongozi wa nchi akiwa Muislamu basi ateuwe idadi kubwa ya Waislamu wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi au akiwa Mkristo atumie uongozi wake kuteua idadi kubwa ya Wakristo wenzake katika uongozi nchini. Au akiwa Mzanaki ateuwe idadi kubwa ya Wazanaki wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi na mfano wa hayo.''
@Mohamed Said wewe ni mdini sana, uteuzi hauangalii huyu katokea dini fulani, zaidi ni weledi na utendaji wa mtu. Halafu tambua uwiano wa waislamu kwa wakristo huku bara siyo 50/50 kwahiyo usitegemee hiyo ratio kuwa sawa hata kwenye ajira na teuzi.

Hiyo ni sawa na wakristo kudai kwamba wanabaguliwa Zanzibar eti kwa sababu zaidi ya 95% ya nafasi za SMZ ni waislamu na wao (wakristo) kudai 50/50 bila kujali population yao ndani ya Zanzibar.

Ukiishi mikoa ya pwani tu unaweza kudhani na pengine kuamini nchi hii uwiano wa wakristo kwa waislamu ni 50/50, pengine kudhani waislamu ni 60% huku wakristo ukidhani ni 40%, kitu ambacho si sahihi unapotembelea upande mwingine wa nchi.

Kwahiyo Mohamed Said 'et al' hoja za udini, mfumo Kristo, mfumo Islam na upuuzi mwingine hazijengi Taifa bali zinatugawa sana. Stop that nonsense
 
Yaani nyinyi waislam hata ukienda chuoni tu unaiona hali halisi kuwa wanafunzi wa kikristo ni wengi hata nusu yao waislam hamfikii leo hii mnataka kubalance! Ndio maana anatoa mawaziri wakristo kwa kisingizio wakajiandae na 2025?
Utajisikiaje siku linaundwa baraza la mawaziri kisha 80% wawe waislamu?, Si utapiga yowe wewe!
Lakini hapa nchini haya tumeyashuhudia katika nyakati mbalimbali za utawala wa maraisi wakiristo, sometimes baraza la mawaziri zaidi ya 80% ni wakiristo tupu
Magufuli ndo alikuwa komesha, teuzi zake nyibgo sana zilinuka udini
 
@Mohamed Said wewe ni mdini sana, uteuzi hauangalii huyu katokea dini fulani, zaidi ni weledi na utendaji wa mtu. Halafu tambua uwiano wa waislamu kwa wakristo huku bara siyo 50/50 kwahiyo usitegemee hiyo ratio kuwa sawa hata kwenye ajira na teuzi.

Hiyo ni sawa na wakristo kudai kwamba wanabaguliwa Zanzibar eti kwa sababu zaidi ya 95% ya nafasi za SMZ ni waislamu na wao (wakristo) kudai 50/50 bila kujali population yao ndani ya Zanzibar.

Ukiishi mikoa ya pwani tu unaweza kudhani na pengine kuamini nchi hii uwiano wa wakristo kwa waislamu ni 50/50, pengine kudhani waislamu ni 60% huku wakristo ukidhani ni 40%, kitu ambacho si sahihi unapotembelea upande mwingine wa nchi.

Kwahiyo Mohamed Said 'et al' hoja za udini, mfumo Kristo, mfumo Islam na upuuzi mwingine hazijengi Taifa bali zinatugawa sana. Stop that nonsense
Bara Waislamu ni wengi kuliko wakiristo.

Sehemu nyingi huku bara unazodhani ni wakiristo ni wafuasi wa dini za jadi
 
Unachanganya baina ya matumizi ya maeneo na kabila. Hoja yako naona ina msingi kwa kuegemea kwenye eneo lakini sio kabila; kwasababu kinacholeta tofauti baina ya makundi ya watu ni mazingira sio kabila lake. Anyway, tusonge mbele.
Una hoja. Lakini mimi nimetazama maudhui ya andiko la mtoa mada kwa mapana zaidi kwasababu katika kila eneo husika asilimia kubwa ya wakazi wa eneo hilo kikabila ni kubwa kuliko wakazi wageni katika muktadha uleule wa kikabila.

Dsm wazaramo ni wengi kuliko makabila mengine...

Mwanza wasukumu ni wengi kuliko makabila mengine.. n.k, n.k...

Naomba kubakia.
 
CIA factbook.
Shige2,
Nilikutana na takwimu hizo za CIA katika mhadhara niliofanya University of Iowa, Marekani.

Nilielezwa kuwa magawanyo wa nafasi Tanzania ni lazima Waislam wawe wachache kwa kuwa wao ni wachache.

Mimi nilikuwa na takwimu zangu za ''religious didtribution,'' lakini Wamarekani wanaziamini takwimu zao za CIA.

Nikawaomba Wamarekani wanipe mfano wa nchi moja duniani ambayo imevamiwa na wakoloni kutoka nje na waliosimama kunyanyua silaha na kupigana na wavamizi wakawa ni wale wachache.

Hapa nikatoa mfano wa Vita Vya Maji Maji na jinsi Waislam walivyosimama kupambana na ukoloni wa Wajerumani 1905 - 1907.

Kwa bahati katika hadhira ile alikuwapo Prof. James Giblin ambae ni Prof. wa History na ameandika kitabu kuhusu Vita Vya Maji Maji.

Niliieleza hadhira ile kuwa Vita Vya Maji vina historia kubwa na Waislam na kumbukumbu yao ipo Kilwa na Mahenge Songea.

Huko ndiko yalipo makaburi ya Abdulrauf Songea Mbano na Khadija Mkomanile majemadari walionyongwa na Wajerumani juma yao 67 na wote Waislam.

(Wanahistoria wetu haya majina ya Kiislam hawayataji utasoma Songea Mbano na Mkomanile.

Majina ya Kiislam wanayakwepa).

Nikauliza tena hadhira yangu yangu kuwa hao wengi walikuwa wapi wasitoke na jeshi kupambana na wavamizi wa nchi yao?

Nikaingia katika ''nationalist politics,'' somo ambalo Wamarekani ni bingwa.

Nikauliza hadhira yangu historia yote ya kupigania uhuru wa Tanganyika nani waliokuwa mstari wa mbele?

Jibu liko wazi na kitabu changu, The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' wanakitumia kama kitabu cha rejea.

Hao wanaoelezwa na CIA Fact Book kuwa ndiyo wengi walikuwa wapi wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika?

Mbona wingi wao haukuonekana?

Nikawaomba watoe mfano wa nchi moja tu duniani ambako wachache walisimama kuikomboa nchi yao.

Ukumbi ulikuwa kimya.
Hapakuwa na jibu.

Takwimu za CIA hazikuweza kujibu haya maswali yangu.
Wamarekani wanajidai sana kuwa wao wanajua kila kitu.

Si kweli.
Ukikaanao utawajua vyema kuwa yapo mengi hawajui.

Majibu yangu haya nilikuja kuelezwa baadae kuwa yalipitishwa kwingi kutaka kujua kama kuna nchi ambayo ''minority,'' ndiyo walioongoza harakati za kupigania uhuru.

Haikupatikana hata nchi moja.

Ukweli ni kuwa siku zote wale wengi ndiyo wanaokuwa na nguvu ya kupambana na adui na wengine huwa nyuma kuongeza nguvu.

1643396385078.png

Prof. James Giblin na kitabu cha Abdul Sykes

Ukitaka kujifunza zaidi kuhusu somo hili ingia hapo chini:

Hiki kinachojengwa sasa hivi ni cha hatari sana kwa usalama wa nchi. Rwanda, Burundi, Kenya, South Sudan, Sudan, Ethiopia, Zimbabwe n.k. wanapambana na changamoto za ama ukabila au udini baada ya madhara makubwa kutokea, sisi tunashabikia na kutaka kwenda huko kwa nguvu. Hili linavunja taifa ....na kuzika kazi kubwa aliyoifanya baba wa taifa (Nyerere). Nasikitika kusema usalama wa taifa hili uko mashakani sana........!
 
Mama Samoa Luna watu wanamwangusha technically

Hizo fomu hicho kipengele cha dini na kabila kiondolewe

In hatari sababu kitawapa watu mianya ya kuoendeleana mfano bosi was Shirika au wizara akijua huyu dini yangu au kabila langu ataibua upendeleo hata kwenye ajira MTU anayeajiri aweza kitumia kuonea wengine kuwa ah huyu anayeomba kazi in kabila language akampendelea

Hayo yalikuwa yameondolewa naona yanarudishwa lengo nini?

Hata kwenye sensa yaliondolewa kuwa MTU asihojiwe kabila au dini yake .Waislamu siasa Kali walitaka kiwemo ili serikali iwasaidie kujua wako wangapi .Wakajibiwa nendeni mkajihesabu huko misikitini
Sasa naona serikali imeanza sensa ya kuhesabu waislamu wako wangapi

Hiyo mifomu yenye dini na kabila ilishaondolewa hiyo sehemu za ajira huyu mama anataka kuturudisha nyuma

Wakristo mnateseka sana katika hili,naona mnavojaribu kupindisha pindisha sentence
 
Hiki kinachojengwa sasa hivi ni cha hatari sana kwa usalama wa nchi. Rwanda, Burundi, Kenya, South Sudan, Sudan, Ethiopia, Zimbabwe n.k. wanapambana na changamoto za ama ukabila au udini baada ya madhara makubwa kutokea, sisi tunashabikia na kutaka kwenda huko kwa nguvu. Hili linavunja taifa ....na kuzika kazi kubwa aliyoifanya baba wa taifa (Nyerere). Nasikitika kusema usalama wa taifa hili uko mashakani sana........!
Msijifiche kwa Nyerere,nyie si ndio mnaosema waislamu hawakusoma ndio maana fursa nyingi zinawapita mbali
 
Shige2,
Nilikutana na takwimu hizo za CIA katika mhadhara niliofanya University of Iowa, Marekani.

Nilielezwa kuwa magawanyo wa nafasi Tanzania ni lazima Waislam wawe wachache kwa kuwa wao ni wachache.

Mimi nilikuwa na takwimu zangu za ''religious didtribution,'' lakini Wamarekani wanaziamini takwimu zao za CIA.

Nikawaomba Wamarekani wanipe mfano wa nchi moja duniani ambayo imevamiwa na wakoloni kutoka nje na waliosimama kunyanyua silaha na kupigana na wavamizi wakawa ni wale wachache.

Hapa nikatoa mfano wa Vita Vya Maji Maji na jinsi Waislam walivyosimama kupambana na ukoloni wa Wajerumani 1905 - 1907.

Kwa bahati katika hadhira ile alikuwapo Prof. James Giblin ambae ni Prof. wa History na ameandika kitabu kuhusu Vita Vya Maji Maji.

Niliieleza hadhira ile kuwa Vita Vya Maji vina historia kubwa na Waislam na kumbukumbu yao ipo Kilwa na Mahenge Songea.

Huko ndiko yalipo makaburi ya Abdulrauf Songea Mbano na Khadija Mkomanile majemadari walionyongwa na Wajerumani juma yao 67 na wote Waislam.

(Wanahistoria wetu haya majina ya Kiislam hawayataji utasoma Songea Mbano na Mkomanile.

Majina ya Kiislam wanayakwepa).

Nikauliza tena hadhira yangu yangu kuwa hao wengi walikuwa wapi wasitoke na jeshi kupambana na wavamizi wa nchi yao?

Nikaingia katika ''nationalist politics,'' somo ambalo Wamarekani ni bingwa.

Nikauliza hadhira yangu historia yote ya kupigania uhuru wa Tanganyika nani waliokuwa mstari wa mbele?

Jibu liko wazi na kitabu changu, The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' wanakitumia kama kitabu cha rejea.

Hao wanaoelezwa na CIA Fact Book kuwa ndiyo wengi walikuwa wapi wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika?

Mbona wingi wao haukuonekana?

Nikawaomba watoe mfano wa nchi moja tu duniani ambako wachache walisimama kuikomboa nchi yao.

Ukumbi ulikuwa kimya.
Hapakuwa na jibu.

Takwimu za CIA hazikuweza kujibu haya maswali yangu.
Wamarekani wanajidai sana kuwa wao wanajua kila kitu.

Si kweli.
Ukikaanao utawajua vyema kuwa yapo mengi hawajui.

Majibu yangu haya nilikuja kuelezwa baadae kuwa yalipitishwa kwingi kutaka kujua kama kuna nchi ambayo ''minority,'' ndiyo walioongoza harakati za kupigania uhuru.

Haikupatikana hata nchi moja.

Ukweli ni kuwa siku zote wale wengi ndiyo wanaokuwa na nguvu ya kupambana na adui na wengine huwa nyuma kuongeza nguvu.

View attachment 2098840
Prof. James Giblin na kitabu cha Abdul Sykes

Ukitaka kujifunza zaidi kuhusu somo hili ingia hapo chini:

Nashukuru sana kwa kueleza kwa kirefu kuhusu uhalali wa CIA Factbook ya idadi ya hizi dini mbili kubwa. Ni kweli kule Kusini wakati wa vita vya Majimaji wengi walikuwa ni Waislam. Lakini unajua ni kwa nini?
Sehemu ya ukanda wa PWANI yote ambako Waarabu walianzia kufanya biashara zao na wenyeji, hilo liliwafanya wengi kuikumbatia dini hii mpya kwao. Ndo hapo mpaka leo wengi ni Waislamu.Hivyo basi Wakristo hawakuwa wengi vile. U kristo uliongezeka baada ya Wamissionary wa CMS na Katoliki kuingia na kuanza kazi yao. Ndo hapo hapo tunakuta Peramiho nk.
Kama nilivyosema Waislamu wengi walikuwa na wako mwambao wa Pwani. Ila Bara Wakristo ni wengi sana. Na hivyo no kusema kuwa CIA Factbook wanatumia data zilizo Factual kulingana na utafiti wao. Hili halina mjadala. Ratio ni 64.1 % Wakristo vs 34.1% Waislam. Kando ya hizo data za Wa Marekani, bado kuna data zingine zinazokubaliana na hizo za Wa Marekani. Maana dunia ni kijiji kwa Karne hii. Nashukuru mkuu.
 
Msijifiche kwa Nyerere,nyie si ndio mnaosema waislamu hawakusoma ndio maana fursa nyingi zinawapita mbali

Kwani uongo?

Hata kwa kuzingatia historia iko hivyo.

Elimu ililetwa na wamisionari (Wakristo), Muslims wachache sana walioamua kwenda kusoma Shule za makafiri ndio wakaanza kuwa wasomi nao wakati huo gap Yani pengo kubwa lilishajiweka baina ya wakristo wasomi na Muslims wasomi mpaka leo.

Muslims wengi wako mwambao wa Pwani ya bahari ya Hindi.

Je huko mwamko na mwitikio wa elimu ukoje?

Jamii zinahamasa ya kupenda kusoma kwa kiasi gani ukilinganisha na kwingine?

Angalia kuanzia Tanga, Morogoro, Pwani , Mtwara, Lindi kuna mwamko kiasi gani ukilinganisha na mikoa ya bara? Hususa kanda ya ziwa? Na magharibi achilia mbali kaskazini ukitoa Tanga ?

Dar es salaam ni ya pekee sababu ya mchanganyiko maalum.
 
Mpaka miaka baada ya Uhuru wasomi waislam walikuwa wanahesabika, halafu leo Eti mnataka pasu tu pasu ?![emoji848]

Halafu Kwani si kuna utaratibu wa usaili?

Kwani vigezo na Sifa Mbona zipo ?

Yani mnataka mtu aajiriwe kwa kigezo cha dini hata kama kwenye mchujo wa ushindani ameshindwa?

Tutajenga Taifa la namna gani?

Aibu.
 
Waislam walichelewa kuitikia kwenda Shule kusoma kwa kuzingatia kuwa elimu ililetwa na wamisionari wakristo.

Kule walikuwa wanafuga na kuchinja nguruwe kwa sana.

Kwa hiyo Kwa kweli sincerely hata ningekuwa mimi I could react the same probably.

Ilichukua muda mrefu baada ya kuhamasika kuona faida ya kusoma , waislam wachache walopiga moyo konde kwa kusema mtumikie kafiri upate mradi wako ndio wakaamua kwenda kusoma Shule za missionary za kikristo.

Sasa wakati ule wanajiuliza waende kusoma misheni au wasiende wenzao wakristo walikuwa wanasonga mbele kielimu na hakuna namna ya kuliondoa hilo pengo naturally.
 
Nashukuru sana kwa kueleza kwa kirefu kuhusu uhalali wa CIA Factbook ya idadi ya hizi dini mbili kubwa. Ni kweli kule Kusini wakati wa vita vya Majimaji wengi walikuwa ni Waislam. Lakini unajua ni kwa nini?
Sehemu ya ukanda wa PWANI yote ambako Waarabu walianzia kufanya biashara zao na wenyeji, hilo liliwafanya wengi kuikumbatia dini hii mpya kwao. Ndo hapo mpaka leo wengi ni Waislamu.Hivyo basi Wakristo hawakuwa wengi vile. U kristo uliongezeka baada ya Wamissionary wa CMS na Katoliki kuingia na kuanza kazi yao. Ndo hapo hapo tunakuta Peramiho nk.
Kama nilivyosema Waislamu wengi walikuwa na wako mwambao wa Pwani. Ila Bara Wakristo ni wengi sana. Na hivyo no kusema kuwa CIA Factbook wanatumia data zilizo Factual kulingana na utafiti wao. Hili halina mjadala. Ratio ni 64.1 % Wakristo vs 34.1% Waislam. Kando ya hizo data za Wa Marekani, bado kuna data zingine zinazokubaliana na hizo za Wa Marekani. Maana dunia ni kijiji kwa Karne hii. Nashukuru mkuu.
Shinge2,
Zipo na data zinazopingana na data za CIA na kama ninavyokueleza nimezijibu takwimu za CIA kwa jicho lililoshuhudia harakati za uhuru 1950s.

Pia kuna mjadala wa sensa ya 1967 na yaliyojiri na nimeandika niliyokutananayo katika kitabu cha Abdul Sykes.

Siku zote mimi nimekuwa nikikwepa kuzungumza suala hili kwa kutambua linavyogonga nyoyo za watu.

Ninazo taarifa nyingi tu ambazo zinaonyesha tatizo katika utoaji wa nafasi za elimu.

Kuna utafiti wa Warsha (1981), Barua ya Prof. Kighoma Malima kwa Rais Ali Hassan Mwinyi kuhusu aliyogundua Wizara ya Elimu (1987) na Hotuba ya Kitwana Kondo Bungeni 1999.

Utafiti wa Warsha ulighabisha sana serikali na wako waliofukuzwa nchini na wengine kuigwa marufuku kutokuwa viongozi katika taasisi yeyote ya Kiislam, Prof. Malima akatolewa Wizara ya Elimu na Kitwana Kondo hakuweza tena kutetea kiti chake.

Nadhani unaweza kukisia kwa nini ilikuwa hivi.

Ukisoma taarifa hizi utaogopa na utajiuliza kweli haya wanafanyiwa Waislam nchi hii?
Je, serikali inayajua haya?

Hapa sina haja ya kueleza tuhuma za Waislam dhidi ya NECTA zilizopelekea Waislam kufanya maandamano mwaka wa 2012.

Ndugu yangu nina mengi niyajuayo katika miaka yangu ya utafiti wa historia ya Waislam wa Tanganyika.
 
Akili...
Si kweli kuwa shule zimekuja na ukoloni.
Bahati mbaya unaandika kitu usichokuwa na ujuzi nacho.

Watu wa mwanzo kujua kile kinachoitwa 3Rs na wataalamu wa elimu ni Waislam, yaani Reading, Writing and Arithmetic.

Elimu yote hii ikisomeshwa katika madrasa na irabu zilizotumika zilikuwa za Kiarabu.
Wakoloni kwa hasad wakapiga marufuku matumizi ya irabu za Kiarabu na kuingiza za Kirumi.

Shule za wamishionari zilikuja baadae sana baada ya Berlin Conference 1884.

Kuna paper ya Ishumi unaweza kuipata Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kaeleza haya kwa kirefu.

Bahati mbaya jina na mwaka nimesahau.
Mimi nina p:aper mbili kuhusu Elimu na Waislam:

The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).

Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).

Nimekuwekea hizo paper hapo juu kukuzindua kuwa unazungumza na mtu aliyetafiti.
Nimeona jinsi unavyoandika unahitaji kusoma zaidi ili ulijue somo unalochangia.
 
Back
Top Bottom