Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Mama anataka kufanya usawa wa kidini kwenye uteuzi.

Huoni leo akiteua mkirito lazima ateue na musilamu, akiondoa mkiristo anaweka muislamu.

Angalia baraza la mawaziri toka ameingia, ameondoa wakristo 7 akateua waislamu 7 ila akawawekea wasaidizi wakristo.

Yeye mama akiteua boss muislamu basi msaidizi wake ni mkiristo.

Kwa sasa anataka dini zenu ili anapofanya uteuzi ajue wewe ni dini gani akupe ama ampe mwingine.

Wanasema wanataka kuvunja mfumo kristo.

Na sisi tusio na dini wapagani atheists na wale wabudha tunasimama wapi
 
Mungu aliipenda Sana Tz kwa kutupa Nyerere kua baba wa Taifa maana bila hivyo nchi hii ingekua imegawanyika kikabila/kidini mbaya kabisa.

Asante Sana Mungu.

Halafu Nyerere bwana, nimegundua hata zile picha zake zote wanazoweka ukutani na marais wengine zao zimeandikwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr/Blah blah blah wakati zake ni simpy Mwalimu JKN Baba wa Taifa
 
Tulizeni mishono dawa iwaangie, tuhuma za udini na ukabila kwenye taasisi za sirikali zimekithirini sana, sasa mama anachunguza je ni kweli ama laa? Hakuna ubaya kuchunguza tuhuma nzito kama hizo ,

Kama mbwai mbwai tu , lakini lazma tuchunguze na kuleta uwiano sawa kwenye sirikali, sio dini fulani au kabila moja mkurugenz hadi mfagiaji.

Keki ya taifa lazma watu wote wapate . Haki na usawa

Mbona sensa kipengele cha dini mlikifuta?
 
Habari wana JF ..

Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata kufikiri yanaweza kufanyika kwa karne hii.

Mimi niwaombe Serikali, niwaombe CCM, niwaombe washauri wa Rais, kama mmechoka, mtuachie hili Taifa.
Wengine bado tunataka kuliona Taifa letu likiwa moja.

Vyombo vya usalama, basi mshaurini mheshimiwa Rais vizuri, msijisahau sana mkaiacha nchi kwenye auto-pilot.
Niwakumbusheni Taifa hili halikujengwa kwa matofali, la hasha!

Mpitisheni Mh. Rais katika historia ndogo ndogo zile njema, zilizotufanya Watanzania japo tukawa wamoja, potelea pote na umaskini wetu.

Sasa hamuwezi amini, leo hii Hazina inaomba taarifa za watumishi (CV), na miongoni mwa taarifa wanazotakiwa kujaza hao watumishi ni:-
1. Kabila lako .....
2. Dini yako .......

Zipo taarifa zingine, za kipuuzi zinazoombwa, ila haina haja sana kuzitaja, kwani hazina athari sana kama hizi mbili.

Hivi kweli, leo mnataka DINI ya mtumishi, iwasaidie nini?
Hii taarifa mnaitumia kuboresha nini?
Udini wa nini katika Tz ya leo.
Tuna ajenda gani na Dini za watu, (watumishi). DINI, DINI.....DINI...!!!!?....,leo tunauliza DINI yako ni ipi? Kweli mh. Rais Samia.

Halafu mnataka na KABILA, kabila la mtumishi litumike kuboresha nini?
Mna ajenda gani huko?

KABILA, leo mnamuuliza mtu KABILA. Kweli mh Rais Samia , ulisema wewe huna kabila, sijui ni Mzanzibar, sasa hawa watumishi, karne ya 21, mwaka 2022, wawajazie makabila yao, muyajue, myafanyie nini?!

Mh Rais Samia, hebu kataa mambo mengine.

Siku Taifa hili likiparaganyika mikononi mwako, hao unaowaona, watakukataa.

Mfumo wa CV (format) na taarifa zinazotakiwa nimeambatanisha hapa.
denooJ , MTAZAMO , barafu , Tindo , Chige , shige2 , Malcolm X5 , MALCOM LUMUMBA ,

Huenda wengine wakalikuchua jambo hili kama si serious vile. Ila ukiangalia between the lines utaona kuna nia na kusudi baya ambalo SSH angependa alitimize kabla ya 2025. Ila ni lazima tumkumbushe kuwa Tanzania Bara si Zanzibari ambapo kuanzia mwenyekiti wa mtaa hadi Mawaziri ni DINI moja. Hivo basi Tanzania Bara ni tofauti sana na Zanzibari Akiendelea hivi naona anatupeleka pabaya.
 
Mama anataka kufanya usawa wa kidini kwenye uteuzi.

Huoni leo akiteua mkirito lazima ateue na musilamu, akiondoa mkiristo anaweka muislamu.

Angalia baraza la mawaziri toka ameingia, ameondoa wakristo 7 akateua waislamu 7 ila akawawekea wasaidizi wakristo.

Yeye mama akiteua boss muislamu basi msaidizi wake ni mkiristo.

Kwa sasa anataka dini zenu ili anapofanya uteuzi ajue wewe ni dini gani akupe ama ampe mwingine.

Wanasema wanataka kuvunja mfumo kristo.
Ni vizuri tumkumbushe kuwa Tanzania Wakristo ni 64.1% vs Waislamu 34:1% tofauti na Zanzibar ambapo zaidi ya ya 90+%ni Waislamu. Kubadilisha hili itamuia vigumu sana. Ni vizuri SSH aende polepole asijikwae bure!!
.
 
Habari wana JF ..

Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata kufikiri yanaweza kufanyika kwa karne hii.

Mimi niwaombe Serikali, niwaombe CCM, niwaombe washauri wa Rais, kama mmechoka, mtuachie hili Taifa.
Wengine bado tunataka kuliona Taifa letu likiwa moja.

Vyombo vya usalama, basi mshaurini mheshimiwa Rais vizuri, msijisahau sana mkaiacha nchi kwenye auto-pilot.
Niwakumbusheni Taifa hili halikujengwa kwa matofali, la hasha!

Mpitisheni Mh. Rais katika historia ndogo ndogo zile njema, zilizotufanya Watanzania japo tukawa wamoja, potelea pote na umaskini wetu.

Sasa hamuwezi amini, leo hii Hazina inaomba taarifa za watumishi (CV), na miongoni mwa taarifa wanazotakiwa kujaza hao watumishi ni:-
1. Kabila lako .....
2. Dini yako .......

Zipo taarifa zingine, za kipuuzi zinazoombwa, ila haina haja sana kuzitaja, kwani hazina athari sana kama hizi mbili.

Hivi kweli, leo mnataka DINI ya mtumishi, iwasaidie nini?
Hii taarifa mnaitumia kuboresha nini?
Udini wa nini katika Tz ya leo.
Tuna ajenda gani na Dini za watu, (watumishi). DINI, DINI.....DINI...!!!!?....,leo tunauliza DINI yako ni ipi? Kweli mh. Rais Samia.

Halafu mnataka na KABILA, kabila la mtumishi litumike kuboresha nini?
Mna ajenda gani huko?

KABILA, leo mnamuuliza mtu KABILA. Kweli mh Rais Samia , ulisema wewe huna kabila, sijui ni Mzanzibar, sasa hawa watumishi, karne ya 21, mwaka 2022, wawajazie makabila yao, muyajue, myafanyie nini?!

Mh Rais Samia, hebu kataa mambo mengine.

Siku Taifa hili likiparaganyika mikononi mwako, hao unaowaona, watakukataa.

Mfumo wa CV (format) na taarifa zinazotakiwa nimeambatanisha hapa.
denooJ , MTAZAMO , barafu , Tindo , Chige , shige2 , Malcolm X5 , MALCOM LUMUMBA ,

Naambiwa fomu za kwanza zilijazwa na kupelekwa Ikulu!!!
 
Ni vizuri tumkumbushe kuwa Tanzania Wakristo ni 64.1% vs Waislamu 34:1% tofauti na Zanzibar ambapo zaidi ya ya 90+%ni Waislamu. Kubadilisha hili itamuia vigumu sana. Ni vizuri SSH aende polepole asijikwae bure!!
.
Source ya Takwimu hizi ni sensa au?
 
Nadhani hili sio jipya na ni usumbufu tu kwani mtu anapoajiriwa, taarifa hizo karibu zote hutakiwa kuzijaza sasa sijui kwanini wanaziomba upya.

Hata Polisi wanapochukua taarifa za wahalifu, huchukua taarifa zikiwemo za kabila la mtu na sijui ni kwanini.
Inasaidia upelelezi
 
.

Hivi kweli, leo mnataka DINI ya mtumishi, iwasaidie nini?
Hii taarifa mnaitumia kuboresha nini?
Udini wa nini katika Tz ya leo.
Tuna ajenda gani na Dini za watu, (watumishi). DINI, DINI.....DINI...!!!!?....,leo tunauliza DINI yako ni ipi? Kweli mh. Rais Samia.

Halafu mnataka na KABILA, kabila la mtumishi litumike kuboresha nini?
Mna ajenda gani huko?

KABILA, leo mnamuuliza mtu KABILA. Kweli mh Rais Samia , ulisema wewe huna kabila, sijui ni Mzanzibar, sasa hawa watumishi, karne ya 21, mwaka 2022, wawajazie ] ,

Bwashee umepatwa weye. Ukitajiwa neno dini au kabila wewe waona ni dhambi. Lkn maneno hayo mawili yapo ndani ya katiba.

Kwa ufupi ni hivi siasa za SSH anautashi wa kupenda siasa jumuishi. Kwa maana dini, ranging, kabila, ambayo ndio makundi makubwa yenye maono tofauti yanatambuliwa na kujumuishwa.

Kwa tz kumjua Hutu ni dini gn anatoka wapi utambuzi huo ni rahisi kwa 80%. Sasa hakuna tatizo badala ya kubahatisha serikali ije na mfumo ulio wazi.

Dini, kabila, mtaa unakoishi ni mambo ya kawaida kuulizwa ktk baadhi ya ofs za serikali. Mwenye damu iliyopatwa na ubaguzi tu ndio itakayoona kuombwa taarifa za dini yako ni udini.

Plz relux
 
Hakuna kitu kinachoitwa 'mfumo kristu' kwenye hili taifa........hizo ni kampeni za kueneza chuki, fitina na hila ovu dhidi ya kundi fulani la ki-imani.
Mfumo huo upo sana. Kwa kuwa wewe ni mkristu huwezi kuona athari yake.
 
Hicho kipengele cha dini kwenye hiyo fomu sijakiona!!
 
Mfumo huo upo sana. Kwa kuwa wewe ni mkristu huwezi kuona athari yake.
Yaani nyinyi waislam hata ukienda chuoni tu unaiona hali halisi kuwa wanafunzi wa kikristo ni wengi hata nusu yao waislam hamfikii leo hii mnataka kubalance! Ndio maana anatoa mawaziri wakristo kwa kisingizio wakajiandae na 2025?
 
Kila anapo ongoza muislam wakiristo huleta mada hizi na kuwaingizia watu wapumbavu kuwa rais muislam au kiongozi Mkuu huyo ameleta taratibu mpya za dodoso wakati tukazamani zipo tu hii nchi mtambue sioyakwenu pekeyenu haya yote nikumtisha rais awapuuze waislam tujiulize rais afanye hayo wakati vyombo vikubwa vimeshikwa nawakina nani mfano
Mkuu majeshi
Mkuu Wa mapolisi
Uhamiaji
Magereza
Jkt
Wote hao ni wadini gani na watuondolee uongo yaani ukimteuwa muislam unaleta udini ukimteuwa mkiristo ndio unajenga umoja toka wameteuliwa hao wakiristo wewe mkiristo umepata nini? Toka wameteuwa waislam Mimi muislamu nimepata nini ?
Rais anateuwa MTU kwa uwezo wake na apendavyo wengene tuendelee nashughuli zetu
 
Kwani kulikuwa kuna haja ya kumtukana huyo mtu? Nani punguani sasa, kati yake na yako?
Ni vema tuijue lugha yetu ya kiswahili vizuri. Sikumwambia yoyote kuwa punguani au mpumbavu, nimetumia maneno "upunguani" na "upumbavu".
 
Back
Top Bottom