Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Niliogopa ulipoanza kusema ila baada ya kuona hiyo CV nikaona ni kitu cha kawaida sana braza. Wewe kama mtumishi, ni muhimu sana mwajiri wako akajua hizo taarifa ikiwemo dini yako, kabila lako, wazazi wako, kwenu ni wapi na taarifa nyingine. Hizo ulizoziainisha ni sawa na zile ulizoandika wakati unajaza kwenye NIDA. Kwa sasa wana establish mifumo ambayo inakuwa na taarifa zako sahihi kote za kikazi na kiraia.

Kwa wewe kama mtumishi, unaweza ukafa kazini, je wakuhudumie kwa imani gani ya dini? Je wakupeleke wapi? Je taratibu za kabila lako zikoje? Haya ni mambo ambayo hayahitaji kubahatisha. Kwa sababu kuna watu walishawahi zikwa kwa imani tofauti maiti ikaja fukuliwa kuzikwa upya. Hapa nimetolea mfano tu braza lakini kunaweza kuwa na sababu zingine muhimu tu zaidi. Kwa hiyo hupaswi kuwa na hofu ya namna hiyo. By the way, wewe kutakiwa kujaza dini haitakuwa mara yako ya kwanza, naamini kuna sehemu nyingi tu wewe na mimi tumeandika ikiwemo kwenye kupata kitamburisho cha Nida, Lesseni za udereva n.k. Relax
 
Asante. Nime jifunza
 
Mkuu ninakupata. Ila usisahau kuwa ktk swala la elimu uliloligusia, ukiangalia kwa makini na kufanya utafiti hata LEO ni kuwa Wakristo na Taasisi zao za Dini walipoingia Tanganyika walijikita zaidi ktk kujenga Taasisi za Elimu, Hospitali nk. Wakati huo huo Taasisi za Kiislamu zilijikita sana ktk kiwafundisha WATOTO wao elimu ya Madrassa wakisema Elimu dunia ni upuuzi. Hata hivyo baadhi ya Wazazi waliojaliwa uelewa hawakukubaliana na hilo. Baada ya Madrassa waliwaingiza watoto wao katika shule za MISHENI/KIKRISTO ili wasome. Miongoni mwao ni kina Jakaya Kikwete na wengine wengi. Sasa ukiangalia hiyo ratio inajieleza yenyewe. Wakristo wakasoma hasa. Waislamu wengi wakakataa hata kuwaingiza watoto wao ktk shule za Kikristo ndo kushuka kwa idadi ya WASOMI miongoni mwa Waislamu. Jaribu kuchukua Data za IDADI ya Taasisi za ELIMU, Hospitali, Nyumba za Wazee nk utakuta ni NYINGI sana sana. Ukilinganisha za Kiislamu utakuta zile KIDOGO zilizopo zimeanzishwa miaka ya hivi karibuni kama vile chuo cha UMMA huko Morogoro. Kwa hiyo basi Wakristo walihudumia mioyo na pia walijaribu sana ktk kubadilisha MAISHA ya Wenyeji waliokuwa wakiwapa dini.
Hii ni kusema nini? Wengi wa wasomi ni Wakristo kutokana na sababu nilizozieleza hapo juu. Nafikiri inajieleza yenyewe. Shukrani.
 
mnarefusha mjadala buree, historia imeeleweka vyema.
sasa tuangalie wakati uliopo je? bado kuna tatizo na kama lipo linasababishwa na nini kwa sasa?
nini kifanyike ili sasa tuijenge Nchi yetu kwa nguvu ya pamoja?
maana kama wasomi wa dini zote sasa wapo wengi tu, hakuna tena kisingizio..
 


Umeandika vizuri lakini hapo itabaki swala la kimahesabu tu ya uwiano na uchambuzi (ratio analysis , interpretation and application ).

Kule kwenye wasomi wengi zaidi zikitangazwa nafasi za kazi chances ya wao kujitokeza kuomba hizo nafasi ni kubwa na obviously chances za idadi yao kuweza kupata hizo nafasi zikawa kubwa pia.

Na kinyume chake kitakuwa sahihi pia .

Swala hapo ni kuweka kanuni thabiti na uwazi katika usaili.

Kuwepo na ushindani huru na siyo kutafuta hisani kwa visingizio ambavyo ha ipo.

Haki ionekane kutendeka kwa uwazi.

Udini usiwepo kabisa.
 
Siyo 50/50 kwa wakristo na waislamu. Hi nchi siyo ya wakristo na waislamu peke yao.

Kila mtu ana kwa imani yake awe Rastafarian, budha, mpagani, Hindu n.k haki ya 50 kwa 50
 
Shinge2,
Unajadili somo usilolijua.

Unaijua historia ya kuvunjwa kwa EAMWS 1968?

Unajua kwa nini ilivunjwa na serikali kuunda BAKWATA?

EAMWS 1968 ilikuwa inajenga shule nchi nzima na jiwe la msingi la Chuo Kikuu liliwekwa na Julius Nyerere.

Waislam wanajenga Chuo Kikuu?
Hili halikubaliki.

Waislam wanajenga shule na wanajenga Chuo Kikuu sisi hatuna Chuo Kikuu!

Hii EAMWS lazima tuivunje kabla haijajenga Chuo Kikuu.

Unaijua historia hii?

EAMWS ikavunjwa na miradi yake yote ya elimu ikaenda na maji.

Je, unawajua waliotenda haya ndani ya serikali ya Tanzania?

Hii ndiyo hatari ya kutaka kujadili mambo usiyoyajua.

Nani kakufunza kuwa Waislam hatukuwa na mipango ya elimu?

Tupiganie uhuru hadi upatikane tusijue tutafanya nini tukishapata uhuru?

Soma historia ya Muslim Congress 1962 na 1963 utajifunza historia ya Waislam wa Tanganyika.

Kiongozi wa Waislam alikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir.

Unaujua mchango wa Sheikh Hassan bin Ameir katika TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika?

Umepata kusoma popote!
Hujiulizi kwa nini?

Baada ya uamuzi kupitishwa kuwa EAMWS ivunjwe Sheikh Hassan bin Ameir alikamatwa usiku wa manane akarudishwa Zanzibar na akapigwa marufuku asitie mguu wake Tanganyika.

Soma historia ya Waislam wa Tanganyika utajifunza mengi na sababu kwa nini mimi niliamua lazima historia hii niiandike ijulikane na vizazi vitajavyokuja baadae.
 
Siyo 50/50 kwa wakristo na waislamu. Hi nchi siyo ya wakristo na waislamu peke yao.

Kila mtu ana kwa imani yake awe Rastafarian, budha, mpagani, Hindu n.k haki ya 50 kwa 50
Ndio maana sio sahihi kwa Christians kuhodhi nafasi nyingi kwa 80%,what about the rest?
 
Naelewa sana. Swali? Kwa hiyo unataka kusema nini mkuu? Pointi yako ni ipi?
 
Elimu ipi unaongelea mzee?

Hi Boko Haram ya mzungu???
 
Ndio maana sio sahihi kwa Christians kuhodhi nafasi nyingi kwa 80%,what about the rest?
Mkuu hiyo EAMWS baada ya kuhamia Tanganyika ikitokea Mombasa, thumuni lao kuu ilikua ni kueneza Uislam. Na tangu liliopoundwa 1945 pamoja ma kuwa lilikuwa na mawazo ama nia ya kuinua Waislam ndani yake kulikuwa na kitu kilichojificha ambacho hakikuwa wazi. Nyerere akashituka. Si kwa sababu walikuwa na UWEZO wa kufanya uliyoyasema bali ilikuwa ni cover tu ya sinister motive. Mbona huko Mombasa walikoanzia bado Waislamu wengi hawakutaka shule? Tukubaliane kuwa tusitupe lawama kuwa kutosoma kwa Waislam wengi kulisababishwa na Wakristo ama viongozi watawala wa Kikristo. Kwa kuwa umekuwa Marekani kama ulivyosema, najua umekuwa na wamarekani weusi. Lawama zao zote ni kulaumu watu weupe kwa kila matatizo yao. Na ukiangalia kwa makini wengi hawataki kusoma wanataka waishi ktk social Welfare. Nafasi wanapewa nyingi tu ni wavivu. Ndo ilivyo wenzetu hapa Tanzania.
 
Kwa nini sasa kipengele cha dini kwenye sensa hamkitaki?.
 
Ndio maana sio sahihi kwa Christians kuhodhi nafasi nyingi kwa 80%,what about the rest?
kama kweli takwimu zako ziko sahihi, nakubaliana nawe, Mimi ni mkristu safi huwa sipendi unafiki wala uzandiki, ni ukweli usiopingika kuwa ndugu zetu waisilamu walikuwa "marginalized" ktk nafasi mbalimbali za Serikalini, iwe na sababu za kihistoria au vyovyote vile kwa sasa sio sio hoja bali jambo la msingi kwa zama hizi za sasa ni kuwepo uwiano ili kujenga Taifa lenye Umoja na Nguvu zaidi.
I

Sisi sote tutakufa lkn Nchi yetu bado itaendelea kuwapo miaka zaidi ya 100 ijayo, hivyo viongozi wetu hawana budi walitambue hilo, tusione aibu wala tusiogope, tuweke uwiano ktk nafasi mbalimbali za Serikalini ili kuimarisha umoja wa Taifa letu, vinginevyo kama tutaendelea kuficha ukweli tutatengeneza tatizo kubwa huko mbele ya safari.
 
Kwa hiyo saivi watu wataajiriwa kwa vigezo pia vya dini na sio uwezo wa mtu? Haya yatakuwa maajabu.

Tukumbuke kuna wasio na dini kabisa. Sasa hawa sijui placement yao itakuwaje.

Ni hatari kuingiza udini kwenye mambo kama ajira.

Dini tuwaachie maaskofu, mashehe na marabi.
 
Hapana wala sio sahihi kuajiri kwa kigezo cha dini isipo kuwa sifa/uwezo na uzoefu,

nadhani kinacho lalamikiwa hapa ni dini moja kuhodhi kwa asilimia kubwa ktk kila taasisi za Serikali...hilo halina ubishi ni kweli sisi wakristu tumehodhi, sasa kifanyike nini? Badala ya kuendelea kujaza watu wa dini moja ni muhimu kuzingatia uwiano ili kubalance vinginevyo italeta shida kama sio sasa baadae.
ni vyema kuuziba huu ufa badala ya kujidanganya na kuendelea kujenga tabaka ambalo litaleta shinda mbeleni.
Tuipende nchi yetu tuijenge sisi sote ndipo kila mmoja atajua thamani ya Nchi yake.
Taifa imara litajengwa na watanzania wote kwa pamoja sio baadhi.
 
Hivi wewe ulipitia michakato ya ajira au kuna mtu alifanya hiyo michakato kwa niaba yako?

Hetu tuletee mtu humu na taasisi aliyopo ambayo katika mchakato wa ajira/ utumishi hakujaza ni Dini au Kabila gani.

Kama wewe ni kijana wa juzi basi uliza hata Wazee wako.

AU KUNA KITU UNAHOFIA HAPO ULIVYOONA DETAILS ZA UTUMISHI ZINAHITAJIKA
 
Je hiyo asilimia kubwa kwa dini moja ulikuwa ni mkakati wa makusudi au imetokea hivyo tu. Hivi mfano unaitangaza nafasi za kazi halafu wanaoomba 80% ni dini moja na ndio wenye sifa zaidi ya wenzake,utasema ngoja ni balance Dini!!!

Tusiipeleke nchi huko. Kuna ambao Kipaumbele Chao sio Elimu Dunia na ndio maana ktk shule za Msingi kuko balanced, lakini unapoanza kwenda juu kundi moja linaanza kupungua na ukifika vyuoni ndio kabisa. Na sio kama hawana uwezo wa kufika huko laa hasha Bali background ktk familia zao inakuwa haichukuliwi kwa uzito Mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…