Hivi wewe ulipitia michakato ya ajira au kuna mtu alifanya hiyo michakato kwa niaba yako?
Hetu tuletee mtu humu na taasisi aliyopo ambayo katika mchakato wa ajira/ utumishi hakujaza ni Dini au Kabila gani.
Kama wewe ni kijana wa juzi basi uliza hata Wazee wako.
AU KUNA KITU UNAHOFIA HAPO ULIVYOONA DETAILS ZA UTUMISHI ZINAHITAJIKA
Acha uzwazwa.Bwashee umepatwa weye. Ukitajiwa neno dini au kabila wewe waona ni dhambi. Lkn maneno hayo mawili yapo ndani ya katiba.
Kwa ufupi ni hivi siasa za SSH anautashi wa kupenda siasa jumuishi. Kwa maana dini, ranging, kabila, ambayo ndio makundi makubwa yenye maono tofauti yanatambuliwa na kujumuishwa.
Kwa tz kumjua Hutu ni dini gn anatoka wapi utambuzi huo ni rahisi kwa 80%. Sasa hakuna tatizo badala ya kubahatisha serikali ije na mfumo ulio wazi.
Dini, kabila, mtaa unakoishi ni mambo ya kawaida kuulizwa ktk baadhi ya ofs za serikali. Mwenye damu iliyopatwa na ubaguzi tu ndio itakayoona kuombwa taarifa za dini yako ni udini.
Plz relux
Yawezekana kuna mpango mkakati ambao wengi hatuujui.Naambiwa fomu za kwanza zilijazwa na kupelekwa Ikulu!!!
Japo hatujui wanapanga nini lakini kabila na dini sio vitu vya kutukuzwa hata kidogo.Huenda wengine wakalikuchua jambo hili kama si serious vile. Ila ukiangalia between the lines utaona kuna nia na kusudi baya ambalo SSH angependa alitimize kabla ya 2025. Ila ni lazima tumkumbushe kuwa Tanzania Bara si Zanzibari ambapo kuanzia mwenyekiti wa mtaa hadi Mawaziri ni DINI moja. Hivo basi Tanzania Bara ni tofauti sana na Zanzibari Akiendelea hivi naona anatupeleka pabaya.
Huo uwiano unaoupigania bara mbona huupiganii uwepo Zanzibar?kama kweli takwimu zako ziko sahihi, nakubaliana nawe, Mimi ni mkristu safi huwa sipendi unafiki wala uzandiki, ni ukweli usiopingika kuwa ndugu zetu waisilamu walikuwa "marginalized" ktk nafasi mbalimbali za Serikalini, iwe na sababu za kihistoria au vyovyote vile kwa sasa sio sio hoja bali jambo la msingi kwa zama hizi za sasa ni kuwepo uwiano ili kujenga Taifa lenye Umoja na Nguvu zaidi.
I
Sisi sote tutakufa lkn Nchi yetu bado itaendelea kuwapo miaka zaidi ya 100 ijayo, hivyo viongozi wetu hawana budi walitambue hilo, tusione aibu wala tusiogope, tuweke uwiano ktk nafasi mbalimbali za Serikalini ili kuimarisha umoja wa Taifa letu, vinginevyo kama tutaendelea kuficha ukweli tutatengeneza tatizo kubwa huko mbele ya safari.
Asiyeona hatari ya kupalilia ukabila, udini,. Hivyo viwili vikimea, hakuna Taifa moja. Hata kidogo!Baba wa Taifa ktk moja ya hotuba zake zenye upeo wa juu sana, alisema suala la kujua Dini za Watanzania, waachiwe Maaskofu na Mashehe huko Makanisani na Misikitini. Na pia alisisitiza kuhsu Ukabila, na kusema ktk mipango ya Serikali au Utumishi wake, masula ya DINI na UKABILA hayana mashiko kuyajua. Alisisitiza, wanao-angaliwa ni WATANZANIA.
Sasa hao wanaotaka kujaribu kumwaga kimiminika cha Petrol kwenye moto...acha waendelee...
Na watu wakianza kuchokonoa haya. Tunajikuta pabaya sana.Huo uwiano unaoupigania bara mbona huupiganii uwepo Zanzibar?
Kweli kabisa hii ni mbaya. Mie kwenye Dini na Kabila nimeacha blank!
Wanachokijenga hakina afya kwa nchi yetu.
Dini na Kabila vitawaongezea nini ktk utumishi? Hadi viwe vigezo vya ajira!!Kweli kabisa hii ni mbaya. Mie kwenye Dini na Kabila nimeacha blank!
I agreeBunch of incomptetent individuals on the wheel.
Hao wakristo waliosoma mwanzo bado tu wako hai? Hawajakufa?Kwa kusoma ulichoandika ni kwamba unaafiki kile nilichoandika mimi.
Kwamba ni kweli gap au pengo la walosoma wakristo na waislam sababu zake ni za kuhistoria.
Sasa kama unasema elimu ya irabu ilifutwa na wakoloni wakaingiza za kirumi na baadae kuja wamisionari na masharti ya anayetakiwa kusoma awe Mkristo au abadili dini anatizwe ili asome na kupata kazi unazani kwa waislam ilikuwa rahisi kuitikia hilo kwa wakati?
Kwa hiyo ni wazi kwa wakristo ilikuwa rahisi kwa wao kwenda kusoma na kupata kazi kutokana na kwamba waendeshaji walikuwa wa imani moja.
Sasa kwa nini hamtaki kukubali ukweli badala yake mnaleta nongwa?!
Sasa mnawalaumu watanzania wenzenu ambao ni wakristo kana kwamba wao walikuwa sehemu ya wakoloni walokomesha elimu ya kiarabu ?
Je wakristo wakitanzania ndio waloweka masharti ya kimisonari ya kubatizwa?
Hizo zilikuwa external forces ambazo ilikuwa kuziitikia kwa kukubali na kupata matunda au kukataa usipate matunda yake.
Nani wa kulaumiwa.?!
Wewe ndio huna hoja kabisa yaani mtoto azuiwe kusoma kisa kuna watu wa dini yake huko nyuma walisoma!Kadiri wasomi waislam wanavyoongezeka kuwa wengi fahamu kuwa wasomi wakristo wanaongeza kuwa wengi maradufu .
Kutokana na ile historia ilivyokuwa.
Wewe unaposema waislam wasomi phd , masters n.k wapo kibao ni wazi kwa wakristo wapo kibao zaidi maradufu kutokana na historia.
Labda ifike mahali ikatazwe wakristo waache kusoma kwanza kufidia gap Yani pengo lililopo ambalo ni la kihistoria sijui itachukua karne au miongo mingapi kisha idadi ikishakuwa sawa ndipo Wakristo waruhusiwe kuanza kwenda kusoma tena.
Lakini bila hivyo wakristo wataendelea kuwa na wasomi wengi zaidi kuliko waislam kutokana na sababu za kihistoria .
Swali kubwa ni: Inakuwaje hoja za Dini na Kabila zinahusika na mambo ya ajira?Wewe ndio huna hoja kabisa yaani mtoto azuiwe kusoma kisa kuna watu wa dini yake huko nyuma walisoma!
Kwanza uelewe kuna koo kibao tena za kikristo hata leo hii hazina mtu aliyefika University . Sio makabila yote yaliyonufaika kwanza shule zilikuwa chache sana enzi hizo. Pili makabila ya wafugaji yote hayakuona umuhimu wa kupeleka watoto shule na makabila hayo baadhi walikuwa wapagani wala sio waislamu.
Inasikitisha sana kila kunapokuwa na rais muislamu chokochoko za kidini zinaibuka.
Wewe ndio huna hoja kabisa yaani mtoto azuiwe kusoma kisa kuna watu wa dini yake huko nyuma walisoma!
Kwanza uelewe kuna koo kibao tena za kikristo hata leo hii hazina mtu aliyefika University . Sio makabila yote yaliyonufaika kwanza shule zilikuwa chache sana enzi hizo. Pili makabila ya wafugaji yote hayakuona umuhimu wa kupeleka watoto shule na makabila hayo baadhi walikuwa wapagani wala sio waislamu.
Inasikitisha sana kila kunapokuwa na rais muislamu chokochoko za kidini zinaibuka.
Acha uzwazwa.
Nioneshe kifungu chochote cha Katiba, kinachosema Kabila?!
Upambe usikutoe akili.
Sipotezi muda wangu kubishana na mazuzu. Ukitaka kuona download katiba halafu search neno "kabila" then rudi hapasoma hapa.
Ikumbukwe watu hawajazwi tu, unaangaliwa uwezo. Kwa waislamu wengi elimu ya madrasa ni bora kuliko nyingine unategemea nini hapo? Na ni kwa nini tuanze kulinganisha uwiano kwa mizania ya kidini? Tukianza na ukristo na uislam hata waki balance 50/50 kwenye wakristo wataanza kuangalia wa RC, wasabato, walutheri etc kwa waislamu hali napo itakua hivyo hivyo mwisho wa siku tunatengeneza taifa lenye mpasuko kwa misingi ya kidini, Hizi dini sio bora kuliko u raia/uTanzania wetu.Hapana wala sio sahihi kuajiri kwa kigezo cha dini isipo kuwa sifa/uwezo na uzoefu,
nadhani kinacho lalamikiwa hapa ni dini moja kuhodhi kwa asilimia kubwa ktk kila taasisi za Serikali...hilo halina ubishi ni kweli sisi wakristu tumehodhi, sasa kifanyike nini? Badala ya kuendelea kujaza watu wa dini moja ni muhimu kuzingatia uwiano ili kubalance vinginevyo italeta shida kama sio sasa baadae.
ni vyema kuuziba huu ufa badala ya kujidanganya na kuendelea kujenga tabaka ambalo litaleta shinda mbeleni.
Tuipende nchi yetu tuijenge sisi sote ndipo kila mmoja atajua thamani ya Nchi yake.
Taifa imara litajengwa na watanzania wote kwa pamoja sio baadhi.
Mfanyakazi wa serikali hafukuzwi.Wakristo mbona mna hofu Sana,au kwakuwa mmejazana kwenye maofisi mnajishtukia, muacheni Rais apige kazi,hizi kelele mngezipiga kipindi kile Cha dikteta
Makafiri mna tabu SanaIkumbukwe watu hawajazwi tu, unaangaliwa uwezo. Kwa waislamu wengi elimu ya madrasa ni bora kuliko nyingine unategemea nini hapo? Na ni kwa nini tuanze kulinganisha uwiano kwa mizania ya kidini? Tukianza na ukristo na uislam hata waki balance 50/50 kwenye wakristo wataanza kuangalia wa RC, wasabato, walutheri etc kwa waislamu hali napo itakua hivyo hivyo mwisho wa siku tunatengeneza taifa lenye mpasuko kwa misingi ya kidini, Hizi dini sio bora kuliko u raia/uTanzania wetu.
Mbele ya Muarabu wewe mtu mweusi unayejipambanua kwa uislamu ni Kafiri tu.Makafiri mna tabu Sana
Misaada ya kipesa tunaomba Marekani, Mikopo- Marekani (IMF), Jamani hata hizi Takwimu za kwetu tuvuke masafa mpaka Marekani kujua idadi ya wakristo/waislam wangapi nchini kwetu. Ni aibu!!!!!!!!!!! Kwanini tusijipange na kupata Takwimu zetu wenyewe katika SENSA tunazofanya humu nchini?Nashukuru sana kwa kueleza kwa kirefu kuhusu uhalali wa CIA Factbook ya idadi ya hizi dini mbili kubwa. Ni kweli kule Kusini wakati wa vita vya Majimaji wengi walikuwa ni Waislam. Lakini unajua ni kwa nini?
Sehemu ya ukanda wa PWANI yote ambako Waarabu walianzia kufanya biashara zao na wenyeji, hilo liliwafanya wengi kuikumbatia dini hii mpya kwao. Ndo hapo mpaka leo wengi ni Waislamu.Hivyo basi Wakristo hawakuwa wengi vile. U kristo uliongezeka baada ya Wamissionary wa CMS na Katoliki kuingia na kuanza kazi yao. Ndo hapo hapo tunakuta Peramiho nk.
Kama nilivyosema Waislamu wengi walikuwa na wako mwambao wa Pwani. Ila Bara Wakristo ni wengi sana. Na hivyo no kusema kuwa CIA Factbook wanatumia data zilizo Factual kulingana na utafiti wao. Hili halina mjadala. Ratio ni 64.1 % Wakristo vs 34.1% Waislam. Kando ya hizo data za Wa Marekani, bado kuna data zingine zinazokubaliana na hizo za Wa Marekani. Maana dunia ni kijiji kwa Karne hii. Nashukuru mkuu.