Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Habari wana JF ..

Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata
Waasisi wa "Génocidaires" huko Rwanda, Burundi, Yugoslavia, Myanimar, Germany na kwingineko walianza mdogo mdogo kwa kuweka vigezo vyenye viashiria vya kibaguzi kwenye taasisi wanazozimudu, kisha kufanya "Lobbing" kwenye taasisi nyingine nyeti ngumu kwa kuwalainisha viongozi wa juu ili azma Yao itimie..

Ngondo itakuja pale wale wanaohujumiwa watakapoanza kujipanga kujibu mapigo.....

Kama kuna harakati hizo za hovyo zinaendelea, zikomeshwe mara moja kabla ya mambo kuharibika.
 
Kuna watu wanatetea wanasema ni kawaida.
Mimi najiuliza Dini, Kabila vinasaidia nini ktk utendaji wa mtumishi.?!
Tunataka kujua Kabila lake, leo, na yupo kazini miaka, tulishamuajiri kwa vigezo vya elimu, uzoefu, ujuzi,n.k.
Kabila la nini leo? Tumpandishe Cheo kwa kabila, au tupime utendaji wake kwa Dini?
 
Nahisi utakuwa unahusika na zile meseji za "ndagu" na "tuma kwa namba hii" kwenye hiki kiswaswadu changu.
 
Kuna watu wanatetea hili.
Nashangaa sana.

Nimewaambia jambo moja. TAIFA halijengwi kwa matofali, zege, na nondo.

Mnapalilia msioyajua.
 

Labda hawataki tena kuwapa kazi wenye asili za nchi jirani
Ila sijui nimewaza tu
 
Mbona mahakamani police unaulizwa dini yako kabla ya kutoa ushahidi au maelezo uhoji inasadia ata wkt wa teuzi kubwa kujua ili wakt wa kiapo usimpe shida k/kiongozi akupe kitabu gani msaafu au biblia wkt wa kuapa au ata utakapokufawajue uzikwe kwa dini gani au uandaliwe kwa dini gani
 
Hahahaha lkn Samia yeye ni Mzanzibari hana Kabila, ila ninyi backward, uncivilized tribes mnapangwa kwa Makabila mkapige ramli na kuzindika.
 
Nahisi utakuwa unahusika na zile meseji za "ndagu" na "tuma kwa namba hii" kwenye hiki kiswaswadu changu.

Sijakuelewa kabisa hapo
Ila tuangalie hii hoja wewe ni mhutu?
Labda mnalengwa nyie
 
Mbona hii Document nilijaza mwaka ambao nilihamia Taasisi/Shirika la Umma ila sikumbuki kama nilijaza wakati naajiriwa ajira ya kwanza Halmashauri.
 
Ukishamjua Dini yake, ndio utendaji wake na ujuzi kazini unaongezeka?
itasaidia kwenye kujua kama kazi zitaendelea siku ya ijumaa au la kama wote wataenda kusali msikitini

Pia kuna packages za mikopo ya iddi na Christmass kwa watumishi wa umma, itasaidia taasisi za serikali kujipanga na kuzuia upigaji

Pia kuna masuala ya kijamii kama vile vifo, ndoa, haki za urithi za warithi wa marehemu katika mafao yaliyoko huko kazini

Lakini pia ili serikali iweze kuondoa udini, maana kama watu wa dini moja ndo wanaonekana wanapata hizi ajira, au wamejazana kwenye taasisi moja lazima serikali iweze kukusanya data na kujua kwa nini, hii inaweza kuifanya serikali ichukue hatua za kuaddress hilo tatizo ili harmony ipatikane katika nchi la sivyo grievances zinaweza kupelekea katika chuki na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe, naamini hutaki hilo litokee.
 
Unaweza kukuta ata hakuna cha maana wanachoenda kufanya na hizo taarifa.wanaacha kuboresha maslahi ya watumishi wao kazi kujaza madocument yasiyo na msingi.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Umeandika ujinga mtupu
 
Hatari hii🙄
 
Labda wanataka kutambika. Mimi nasubiria mei mosi mama aseme kitu kuhusu ongezeko la mtonyo.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…