Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Hii issue ni sensitive! Ila wewe, mimi na yeye, tuna juwa kwamba Lilihitaji nani amfunge paka kengele! Bila hivyo hakuna uwiano wa kuridhisha! Kuna makundi yamekuwa ya kila makombo ya keki ya Taifa wakati mengine yana bwia keki nzima. Let's be realistic /honest.
Kwa hiyo unaamini huu ni mkakati maalumu?
Mfano mkigundua Wakristo ni wengi, mnaanza kubana wao wasiingie kazini, muweke Dini zingine?
Au kama waislamu ni wengi, wazuiwe kuajiriwa, hata kama wao ndio wana sifa zaidi za kielimu, kimafunzo, kiutendaji. Unawaza hivyo?!
 
Unawaza kujua Kabila na Dini ya mtu Kwa ajili ya maziko??? Kweli...
You are so myopic. Una upeo mfupi sana.
Kama vipi tuondoe hata majina ya mikoa wilaya tarafa kata Kijiji mtaa kitongoji uwe inaandikwa kuwa unaishi na umezaliwa Tanzania inatosha ama shida ni Nini lakini.mbona unaogopa.
Hata usipoandika unajulikana
 
Sio lazima kujaza dini kwenye hiyo CV, hauwezi kufanywa chochote kwa kutokua na dini. Pia watu wengi tu wanaishi pamoja na wakiwa na familia bila kuoana na zipo ndoa za kiserikali ambazo sio lazima kuwa na dini.
Hizo ni nadharia tu za ndoa za boma lakini sababu ya uwepo wa ndoa za serikali ni kwa sababu tu wazazi wa Amina wamekataa kufungisha ndoa ya binti yao kwa Peter na hivyo amina peter kuhalalisha ufuska na ukaidi wao kwa wazazi wameamua kwenda kwa baraza la wilaya ili kuruhusiwa waishi kama mama na baba kwa wanao.
Hizi dini na makabila yapo kikanda na wilaya. Mfano Ruvuma Mbinga wakristo na wamatengo, Songea wakristo na wangoni, Namtumbo waisilamu na wandendeule, Tunduru Waisilamu na wayao. Umkute mmatengo muisilamu lazima akupe sababu kwa nn yeye muisilamu hivyo hivyo ukikutana na Myao mkristo lazima akupe sababu ya yy kuwa mkristo. Leo hii ukienda Mbeya wanyakyusa waisilamu wapo ila wachache sana na wanasababu za kuwa huko ila 98% wakristo.
Sababu hizo zinazotolewa kwa sababu tu sio athiri yao kuwa dini hizo. Tanzania dini zipo na makabila yapo na ukitaka idadi nitakupa
 
Mimi nasubiri nione 'dodoso' ya sensa kama itakuwa na kipengele.

Nacheka lakini naopgopa.
 
Mama anataka kufanya usawa wa kidini kwenye uteuzi.

Huoni leo akiteua mkirito lazima ateue na musilamu, akiondoa mkiristo anaweka muislamu.

Angalia baraza la mawaziri toka ameingia, ameondoa wakristo 7 akateua waislamu 7 ila akawawekea wasaidizi wakristo.

Yeye mama akiteua boss muislamu basi msaidizi wake ni mkiristo.

Kwa sasa anataka dini zenu ili anapofanya uteuzi ajue wewe ni dini gani akupe ama ampe mwingine.

Wanasema wanataka kuvunja mfumo kristo.
Ukiteua huku unafikiria dini badala ya uwezo na utayari wa mtu ni hatari sana. Maana badae watu wataenda mbali zaidi hadi kwenye madhejebu. Utwaridhisha watu kweli kwa jinsi hii?
 
Kwani serikali inafanya matambiko? Serikali inaswalisha? Kuna kitu gani cha kiimani au kikabila serikali inafanya kwenye hizo dharula?
Hii acting smart ya baadhi ya watu ni hatari sana. Kama mtakumbuka malumbano haya yalianza wakati wa sensa ya 2012 mpaka, then kipengele hicho kikaondolewa.

Mambo kama haya huanzishwa kwa akili na kwa utaratibu ili kuleta division na kuwadi wa haya yote huwa external people. Africa imeshindwa kujiendeleza kipengele kikubwa kikiwa hicho, Tanzania imekuwa tofauti na mara kadhaa wameshindwa kutuviruga kwasababu ya integration iliyofanya na baba wa taifa na makatazo fulani. Miaka ya nyuma ilikuwa ni kosa hata kutaja kabila publicly nakumbuka nilikemewa nilipotaja kabila la wafugaji kwenye workshop fulani. So sad to see haya yanaanza kuwa introduced slowly and carefully....Mungu isaidie nchi yangu
 
Habari wana JF ..

Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata kufikiri yanaweza kufanyika kwa karne hii.

Mimi niwaombe Serikali, niwaombe CCM, niwaombe washauri wa Rais, kama mmechoka, mtuachie hili Taifa.
Wengine bado tunataka kuliona Taifa letu likiwa moja.

Vyombo vya usalama, basi mshaurini mheshimiwa Rais vizuri, msijisahau sana mkaiacha nchi kwenye auto-pilot.
Niwakumbusheni Taifa hili halikujengwa kwa matofali, la hasha!

Mpitisheni Mh. Rais katika historia ndogo ndogo zile njema, zilizotufanya Watanzania japo tukawa wamoja, potelea pote na umaskini wetu.

Sasa hamuwezi amini, leo hii Hazina inaomba taarifa za watumishi (CV), na miongoni mwa taarifa wanazotakiwa kujaza hao watumishi ni:-
1. Kabila lako .....
2. Dini yako .......

Zipo taarifa zingine, za kipuuzi zinazoombwa, ila haina haja sana kuzitaja, kwani hazina athari sana kama hizi mbili.

Hivi kweli, leo mnataka DINI ya mtumishi, iwasaidie nini?
Hii taarifa mnaitumia kuboresha nini?
Udini wa nini katika Tz ya leo.
Tuna ajenda gani na Dini za watu, (watumishi). DINI, DINI.....DINI...!!!!?....,leo tunauliza DINI yako ni ipi? Kweli mh. Rais Samia.

Halafu mnataka na KABILA, kabila la mtumishi litumike kuboresha nini?
Mna ajenda gani huko?

KABILA, leo mnamuuliza mtu KABILA. Kweli mh Rais Samia , ulisema wewe huna kabila, sijui ni Mzanzibar, sasa hawa watumishi, karne ya 21, mwaka 2022, wawajazie makabila yao, muyajue, myafanyie nini?!

Mh Rais Samia, hebu kataa mambo mengine.

Siku Taifa hili likiparaganyika mikononi mwako, hao unaowaona, watakukataa.

Mfumo wa CV (format) na taarifa zinazotakiwa nimeambatanisha hapa.
denooJ , MTAZAMO , barafu , Tindo , Chige , shige2 , Malcolm X5 , MALCOM LUMUMBA ,

View attachment 2095758
Rais anahusika vipi hapo?
 
Mbona hizi taarifa za dini na kabila hazijaanza leo, labda kama ww ndio umeanza kuziona awamu hii ya sita ila toka muda ukienda polisi au hosipital walikua wanauliza kabila na dini yako
Mtumishi aliyepo kazini, Kabila linakusadia nini? Kupandisha mshahara, au cheo?
 
Habari wana JF ..

Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata kufikiri yanaweza kufanyika kwa karne hii.

Mimi niwaombe Serikali, niwaombe CCM, niwaombe washauri wa Rais, kama mmechoka, mtuachie hili Taifa.
Wengine bado tunataka kuliona Taifa letu likiwa moja.

Vyombo vya usalama, basi mshaurini mheshimiwa Rais vizuri, msijisahau sana mkaiacha nchi kwenye auto-pilot.
Niwakumbusheni Taifa hili halikujengwa kwa matofali, la hasha!

Mpitisheni Mh. Rais katika historia ndogo ndogo zile njema, zilizotufanya Watanzania japo tukawa wamoja, potelea pote na umaskini wetu.

Sasa hamuwezi amini, leo hii Hazina inaomba taarifa za watumishi (CV), na miongoni mwa taarifa wanazotakiwa kujaza hao watumishi ni:-
1. Kabila lako .....
2. Dini yako .......

Zipo taarifa zingine, za kipuuzi zinazoombwa, ila haina haja sana kuzitaja, kwani hazina athari sana kama hizi mbili.

Hivi kweli, leo mnataka DINI ya mtumishi, iwasaidie nini?
Hii taarifa mnaitumia kuboresha nini?
Udini wa nini katika Tz ya leo.
Tuna ajenda gani na Dini za watu, (watumishi). DINI, DINI.....DINI...!!!!?....,leo tunauliza DINI yako ni ipi? Kweli mh. Rais Samia.

Halafu mnataka na KABILA, kabila la mtumishi litumike kuboresha nini?
Mna ajenda gani huko?

KABILA, leo mnamuuliza mtu KABILA. Kweli mh Rais Samia , ulisema wewe huna kabila, sijui ni Mzanzibar, sasa hawa watumishi, karne ya 21, mwaka 2022, wawajazie makabila yao, muyajue, myafanyie nini?!

Mh Rais Samia, hebu kataa mambo mengine.

Siku Taifa hili likiparaganyika mikononi mwako, hao unaowaona, watakukataa.

Mfumo wa CV (format) na taarifa zinazotakiwa nimeambatanisha hapa.
denooJ , MTAZAMO , barafu , Tindo , Chige , shige2 , Malcolm X5 , MALCOM LUMUMBA ,

View attachment 2095758

Ina maana hujui umuhimu wa sherehe za Kichifu na Makabila zinazopigiwa chapuo kila uchao? Mbona kwenye nyumba za wageni unaulizwa Kabila lako na huhoji!
 
Ina maana hujui umuhimu wa sherehe za Kichifu na Makabila zinazopigiwa chapuo kila uchao? Mbona kwenye nyumba za wageni unaulizwa Kabila lako na huhoji!
Tunatakiwa kuondoa haya maswali. Hayana tija, yanatumika isivyopaswa.
 
Mambo mengine ni ya kipumbavu kwa wajinga
Mimi ni mimi niulize mimi na kosa nikifanya ni mimi
Hiyo sheria ya kuuliza majina matatu ya mzazi ipo wapi duniani kama sio kwetu tu

Hawajui kuwa wengine hawawajui wazazi wao?
Wengine hata kabila hawajui unataka adanganye?
Acheni kabisa ujinga huu
 
Habari wana JF ..

Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata kufikiri yanaweza kufanyika kwa karne hii.

Eti " Trible " sic ni ujinga tu 😡 😡 😡
 
Napata taabu kuamini kama hili suala ni kweli, na kama ni kweli basi aliye-propose na kulipitisha wote ni viumbe wapumbavu kupita maelezo! Na kama SSH analifahamu hili, na anaacha liendelee, basi nitamdharau sana kwa sababu ni jambo ambalo haliwezi kuwa justified kwa tafsiri yoyote ile!!

I wish hii thread nisingeiona mapema kwa sababu imeniharibia mood sana!
Ninaweza nikakuwekea Waraka wa ndani wa Taasisi moja ya Umma, hiki ni kiambatanisho tu.
Nimeacha hizo nyaraka za Taasisi, zilizosainiwa. Na deadline ya kuwasilisha taarifa hizi ni tarehe 07 February 2022.
Nasita kuweka hizo nyaraka, kulinda watoa taarifa.
 
Back
Top Bottom