Tetesi: Watumishi waliogombea Ubunge roho mkononi

Tetesi: Watumishi waliogombea Ubunge roho mkononi

mkalamo

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2013
Posts
340
Reaction score
359
Ikiwa kesho tarehe 25 ndiyo siku ya Tume ya Uchaguzi kuwathibitisha wagombea wa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani kwa vyama mbali mbali nchini, hali ya ajira ya watumishi wa Umma waliojitosa katika kinyang'anyiro hicho imebaki kuwa ni kitendawili kisichokuwa na mteguaji.

Kwa mujibu wa taarifa zilizowasilishwa kwa maafisa utumishi katika halmashauri mbali mbali nchini, pamoja na taasisi za umma, wale wote waliogombea pasipo kujali kama waliteuliwa na vyama vyao au la wanatakiwa waandike barua upya ya kuomba kurejea kazini huku wakisubiri majibu kama wataruhusiwa kuendelea na kazi au ndiyo mwisho wa ajira zao.

Agizo hilo linawahusu wote waliogombea kwa nafasi ya kata, jimbo na viti maalum ambayo mpaka sasa vyama kwa asilimia 90 zimeshawatambulisha wagombea wao wa nafasi hizo pamoja na wale wa Viti Maalum.

Mpaka sasa wengi wa wagombea walioshindwa kupitishwa na vyama vyao wameshindwa kurejea kazini wakisubiri hatma ya Agost 25
 
mkalamo,

Nawapa pole zao. Baada ya kukosa mishahara miezi miwili bado hawajui hatima yao. Sikuona kosa lao kujaribu bahati zao kisiasa kama Watanzania wengine waliotia nia mwaka huu. Kama kungekuwa na waraka wa kuwakumbushia / kuwaonya wasijitumbukize huko (Endapo wangekuwa wanavunja sheria) , wengi wao wasingethubutu kutia nia ila kwa sababu ilizoeleka chaguzi zilizopita hakukuwa na tatizo baada ya kuomba ruhusa, nao wakajaribu bahati zao.

Siasa inalipa nchi hii kuliko taaluma yeyote ile ndiyo maana mwamko wa watendaji wa Serikali kwa ngazi mbalimbali kutimkia huko ni mkubwa sana.

Lakini kwanini haya yamejitokeza mwaka huu? Sheria ya Utumishi wa Umma inasemaje? Je, watumishi wa Umma waliotia nia walifuata sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma? Mbona wanasiasa wengi wenye majina makubwa walikuwa watumishi wa umma na wakabadili mwelekeo na kujiunga na siasa, waliwezeshwa na sheria gani?

Naomba nisaidiwe na wataalamu wa sheria za kazi ili kukuza ufahamu wangu.
 
Back
Top Bottom