Nawapa pole zao. Baada ya kukosa mishahara miezi miwili bado hawajui hatima yao. Sikuona kosa lao kujaribu bahati zao kisiasa kama Watanzania wengine waliotia nia mwaka huu. Kama kungekuwa na waraka wa kuwakumbushia / kuwaonya wasijitumbukize huko (Endapo wangekuwa wanavunja sheria) , wengi wao wasingethubutu kutia nia ila kwa sababu ilizoeleka chaguzi zilizopita hakukuwa na tatizo baada ya kuomba ruhusa, nao wakajaribu bahati zao.
Siasa inalipa nchi hii kuliko taaluma yeyote ile ndiyo maana mwamko wa watendaji wa Serikali kwa ngazi mbalimbali kutimkia huko ni mkubwa sana.
Lakini kwanini haya yamejitokeza mwaka huu? Sheria ya Utumishi wa Umma inasemaje? Je watumishi wa Umma waliotia nia walifuata sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma? Mbona wanasiasa wengi wenye majina makubwa walikuwa watumishi wa umma na wakabadili mwelekeo na kujiunga na siasa, waliwezeshwa na sheria gani?
Naomba nisaidiwe na wataalamu wa sheria za kazi ili kukuza ufahamu wangu.