Tetesi: Watumishi waliogombea Ubunge roho mkononi

Tetesi: Watumishi waliogombea Ubunge roho mkononi

Yeah,ukiamua kuingia kwenye siasa,lazima ujiuzulu nafasi yako ya kazi ya umma,ubaki na siasa tu......wengi hawakuzingatia na kupitia pitia sheria za kazi na kujua status yao baada ya kwenda kugombea
Anajihuzulu akiteuliwa mkuu, hiyo ilikuwa ni kuomba ridhaa na siyo kugombea
 
mkalamo,

Watumishi wa Umma waliokosa kuteuliwa na ccm wamekosa mishahara miezi miwili,wamekosa nafasi zao za kazi waliokuwa, wako majumbani hawajui hatima Yao, Sasa wale waliopitishwa kugombea wanawaomba Wasaidie Tena kufanya kampeni ili waweze kushinda Oct,28. Watumishi hai Ni zaidi ya 7,000 na wanaogopa hata kuvaa kofia na mashati ya CCM. Na Bila kuwatumia waliokosa Kura za maoni Hali za walioteuliwa kisiasa Ni mbaya kwani waliokosa mishahara wameonekana wasaliti ndani ya jamii na wafanyakazi wenzao.

Kwa mantiki hiyo tunaomba wale wote waliokosa utumishi na mishahara Yao waachane na kuwafanyia kampeni na waonane kwenye box la Kura October 28.
Hio mishahara inaenda kumalizia SGR,tuwe wazalendo mkuu.
 
Inawezekana,ila nijuavyo nasisitiza mtumishi wa umma hatakiwi kuwa na kadi ya chama au kugombea ndani ya utumishi wake......ndiyo maana kamanda Shana watu walimpigia kelele sana
Hizo ni story tu boss.
tapatalk_1577354951190.jpg
 
Ikiwa kesho tarehe 25 ndiyo siku ya Tume ya Uchaguzi kuwathibitisha wagombea wa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani kwa vyama mbali mbali nchini, hali ya ajira ya watumishi wa Umma waliojitosa katika kinyang'anyiro hicho imebaki kuwa ni kitendawili kisichokuwa na mteguaji.

Kwa mujibu wa taarifa zilizowasilishwa kwa maafisa utumishi katika halmashauri mbali mbali nchini, pamoja na taasisi za umma, wale wote waliogombea pasipo kujali kama waliteuliwa na vyama vyao au la wanatakiwa waandike barua upya ya kuomba kurejea kazini huku wakisubiri majibu kama wataruhusiwa kuendelea na kazi au ndiyo mwisho wa ajira zao.

Agizo hilo linawahusu wote waliogombea kwa nafasi ya kata, jimbo na viti maalum ambayo mpaka sasa vyama kwa asilimia 90 zimeshawatambulisha wagombea wao wa nafasi hizo pamoja na wale wa Viti Maalum.

Mpaka sasa wengi wa wagombea walioshindwa kupitishwa na vyama vyao wameshindwa kurejea kazini wakisubiri hatma ya Agost 25
Pole yao
 
mkalamo,

Nawapa pole zao. Baada ya kukosa mishahara miezi miwili bado hawajui hatima yao. Sikuona kosa lao kujaribu bahati zao kisiasa kama Watanzania wengine waliotia nia mwaka huu. Kama kungekuwa na waraka wa kuwakumbushia / kuwaonya wasijitumbukize huko (Endapo wangekuwa wanavunja sheria) , wengi wao wasingethubutu kutia nia ila kwa sababu ilizoeleka chaguzi zilizopita hakukuwa na tatizo baada ya kuomba ruhusa, nao wakajaribu bahati zao.

Siasa inalipa nchi hii kuliko taaluma yeyote ile ndiyo maana mwamko wa watendaji wa Serikali kwa ngazi mbalimbali kutimkia huko ni mkubwa sana.

Lakini kwanini haya yamejitokeza mwaka huu? Sheria ya Utumishi wa Umma inasemaje? Je, watumishi wa Umma waliotia nia walifuata sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma? Mbona wanasiasa wengi wenye majina makubwa walikuwa watumishi wa umma na wakabadili mwelekeo na kujiunga na siasa, waliwezeshwa na sheria gani?

Naomba nisaidiwe na wataalamu wa sheria za kazi ili kukuza ufahamu wangu.
Sheria ya utumishi iko wazi kwamba unaomba likizo isiyo na malipo. tatizo utekelezaji wale ni mgumu kwa sababu, kama ilivyotokea mwaka huum mawaziri walikuwa kazini na bado wako kazini na waligombea nafasi ya ubunge. Kwa maana nyingine ni hasira ya wanasiasa kutotaka watumishi wengine waingie kwenye mchakato huo.

Kama ni likizo, basi hata mawaziri waliogombea ambao pia hulipwa mishahara, wote wangeondoka na kuwa nje hadi uthibitisho wa wagombea.
 
Sheria ya utumishi iko wazi kwamba unaomba likizo isiyo na malipo. tatizo utekelezaji wale ni mgumu kwa sababu, kama ilivyotokea mwaka huum mawaziri walikuwa kazini na bado wako kazini na waligombea nafasi ya ubunge. Kwa maana nyingine ni hasira ya wanasiasa kutotaka watumishi wengine waingie kwenye mchakato huo.

Kama ni likizo, basi hata mawaziri waliogombea ambao pia hulipwa mishahara, wote wangeondoka na kuwa nje hadi uthibitisho wa wagombea.
Kwenye muundo wa utumishi mawaziri wanatambulika kama public servants?
 
Kwenye muundo wa utumishi mawaziri wanatambulika kama public servants?
Unaweza ukaipa definition yoyote ile, hata wabunge lakini ukishapokea pesa toka serikalini lazima utii conflict of interest. Hiyo sheria undani wake ilikuwa ni kukomoa watumishi wa serikali wanaoingia opposition parties.

Hesabu ni wangapi wameingia opposition? Dr Lukanima aligombea Chato baada ya hapo hakupewa tena nafasi ya kurudi utumishi wa umma. That is how we go! Hakuna sheria wala logic ni mapenzi ya watu.
 
Back
Top Bottom