Tetesi: Watumishi waliogombea Ubunge roho mkononi

Unaweza ukaipa definition yoyote ile, hata wabunge lakini ukishapokea pesa toka serikalini lazima utii conflict of interests. Hiyo sheria undani wake ilikuwa ni kukomoa watumishi wa serikali wanaoingia opposition parties.

Hesabu ni wangapi wameingia opposition? Dr Lukanima aligombea Chato baada ya hapo hakuopewa tena nafasi ya kurudi utumishi wa umma. That is how we go! Hakuna sheria wala logic ni mapenzi ya watu.
Kwa mwaka huu kwasabab makada wengi ambao ni watumishi bila shaka watarejeshwa. Ole kwa wale wenye kadi ya kile chama kingine mwajiri anaweza sema sina nia ama nafasi yako tena subiri mpaka utakapo itwa.

Hapo ndipo kutakuwa na kilio na kusaga meno
 
Hivi ni kweli wamekosa mishahara ya miezi miwili?
Kwani mshahara wa mwezi Agusti kwa watumishi wa umma umeshatoka?
 
Bila Shaka Hao Wote Wataendelea Na Majukumu Yao
 
mkalamo,

Nawapa pole zao. Baada ya kukosa mishahara miezi miwili bado hawajui hatima yao. Sikuona kosa lao kujaribu bahati zao kisiasa kama Watanzania wengine waliotia nia mwaka huu. Kama kungekuwa na waraka wa kuwakumbushia / kuwaonya wasijitumbukize huko (Endapo wangekuwa wanavunja sheria) , wengi wao wasingethubutu kutia nia ila kwa sababu ilizoeleka chaguzi zilizopita hakukuwa na tatizo baada ya kuomba ruhusa, nao wakajaribu bahati zao.

Siasa inalipa nchi hii kuliko taaluma yeyote ile ndiyo maana mwamko wa watendaji wa Serikali kwa ngazi mbalimbali kutimkia huko ni mkubwa sana.

Lakini kwanini haya yamejitokeza mwaka huu? Sheria ya Utumishi wa Umma inasemaje? Je, watumishi wa Umma waliotia nia walifuata sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma? Mbona wanasiasa wengi wenye majina makubwa walikuwa watumishi wa umma na wakabadili mwelekeo na kujiunga na siasa, waliwezeshwa na sheria gani?

Naomba nisaidiwe na wataalamu wa sheria za kazi ili kukuza ufahamu wangu.
Mbona ni kawaida mfanyakazi akiamua kwenda kugombea nafasi za kisiasa lazima achukue likizo bila malipo!! Pia waraka ulitolewa mapema tu kama hujui uliza walioko kwenye ajira za Umma. Unataka usiwepo kazini na bado uendelee kulipwa pesa kweli??!!
 
Ila wanajisahau Sana baadhi ya watumishi wa umma,nikweli kila mtu anahisia na chama fulani ila wengi wanashindwa kujizuia
Unadhani wana hisia basi mkuu ni vile tu hua wanazuga tu,wale wote wanawaza kujipendekeza na kupata vyeo tu.
 
Mbona ni kawaida mfanyakazi akiamua kwenda kugombea nafasi za kisiasa lazima achukue likizo bila malipo!! Pia waraka ulitolewa mapema tu kama hujui uliza walioko kwenye ajira za Umma. Unataka usiwepo kazini na bado uendelee kulipwa pesa kweli??!!
Hivi unawezaje kutoka Ofisini kwenda kuomba uwakilishi Eneo wala watu waishio hapo huwafahamu? Kutia Nia ni Mchakato wa Muda mrefu. Ndio maana wameishia kupata Kura '0'.
 
mkalamo,

Nawapa pole zao. Baada ya kukosa mishahara miezi miwili bado hawajui hatima yao. Sikuona kosa lao kujaribu bahati zao kisiasa kama Watanzania wengine waliotia nia mwaka huu. Kama kungekuwa na waraka wa kuwakumbushia / kuwaonya wasijitumbukize huko (Endapo wangekuwa wanavunja sheria) , wengi wao wasingethubutu kutia nia ila kwa sababu ilizoeleka chaguzi zilizopita hakukuwa na tatizo baada ya kuomba ruhusa, nao wakajaribu bahati zao.

Siasa inalipa nchi hii kuliko taaluma yeyote ile ndiyo maana mwamko wa watendaji wa Serikali kwa ngazi mbalimbali kutimkia huko ni mkubwa sana.

Lakini kwanini haya yamejitokeza mwaka huu? Sheria ya Utumishi wa Umma inasemaje? Je, watumishi wa Umma waliotia nia walifuata sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma? Mbona wanasiasa wengi wenye majina makubwa walikuwa watumishi wa umma na wakabadili mwelekeo na kujiunga na siasa, waliwezeshwa na sheria gani?

Naomba nisaidiwe na wataalamu wa sheria za kazi ili kukuza ufahamu wangu.
Mkuu, kuwa mpole tuu. Kama ulitia nia ikabuma tafuta kazi ingine
 
Back
Top Bottom