Tetesi: Watumishi waliogombea Ubunge roho mkononi

Leo tukifuata hiki wanachofanyiwa hawa watumishi, nadhani hatutakuwa na mwanasiasa hata mmoja.

Tutaanza kumfuta Magufuli kwenye hii nafasi yake, maana ilitokana na yeye kuwa mtumishi wa umma. Majaliwa naye hatabaki salama.
 
mkalamo,

Watumishi wa Umma waliokosa kuteuliwa na ccm wamekosa mishahara miezi miwili,wamekosa nafasi zao za kazi waliokuwa, wako majumbani hawajui hatima Yao, Sasa wale waliopitishwa kugombea wanawaomba Wasaidie Tena kufanya kampeni ili waweze kushinda Oct,28. Watumishi hai Ni zaidi ya 7,000 na wanaogopa hata kuvaa kofia na mashati ya CCM. Na Bila kuwatumia waliokosa Kura za maoni Hali za walioteuliwa kisiasa Ni mbaya kwani waliokosa mishahara wameonekana wasaliti ndani ya jamii na wafanyakazi wenzao.

Kwa mantiki hiyo tunaomba wale wote waliokosa utumishi na mishahara Yao waachane na kuwafanyia kampeni na waonane kwenye box la Kura October 28.
 

Walionywa na waraka!
 
Hakuna kitu kibaya kama kuwa maskini wa akili, unashangilia wenzako kufukuzwa kazi badala ya kusikitika na kushauri, sisi maskini huwa tunaombea aliyenacho akose tukose wote badala ya kuomba uwe kama yeye.
Wakati wengine wanasota na yeye pia alikuwa anashangilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…