RESOLVED KERO Watumishi Wapya VETA: Miezi 2 Bila Kazi Wala Mshahara

RESOLVED KERO Watumishi Wapya VETA: Miezi 2 Bila Kazi Wala Mshahara

Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
VETA
Habari za wakati huu. Mimi ni mmoja wa watumishi wapya walioajiriwa na Veta tarehe 19/02. Baada ya kufika makao makuu Dodoma na kukamilisha zoezi la kusaini mikataba ya ajira, tuliombwa kusubiri maelekezo ya kupangiwa vituo vya kazi.
Hata hivyo, hadi sasa zimepita takribani miezi miwili bila mrejesho wowote, na hatujaanza kulipwa mishahara yetu licha ya kuwa na mikataba halali. Hali hii imetuweka kwenye wakati mgumu sana kiuchumi na kisaikolojia kwa sababu zifuatazo:
  1. Kufungiwa kwenye Mfumo wa Ajira Portal: Mfumo unatuonyesha kuwa tayari tumeajiriwa, jambo linalotunyima fursa ya kufanya usaili (interviews) mwingine wa kazi.
  2. Kukwama Kimaisha: Hatuwezi kutafuta kazi mbadala wala kuongeza mikataba sehemu tulizokuwa mwanzo, kwa hofu ya kuitwa Veta ghafla na kushindwa kuvunja mikataba mipya kwa urahisi.
Tunaomba uongozi wa VETA Makao Makuu utupatie majibu ya mambo haya mawili:
  • Ni lini hasa tutapangiwa vituo vyetu vya kazi?
  • Ni kwa nini malipo ya mishahara yanasuasua wakati mikataba ilishasainiwa na mfumo umetufunga?
Tunaomba mamlaka husika itusaidie kupata ufumbuzi wa jambo hili.

Majibu haya hapa ~ Madai ya Ajira Mpya VETA walioitwa Dodoma ‘kutelekezwa’, VETA yasema “Wanaandaliwa mafunzo elekezi 21-22 Mei 2026”
 
Tayari mlishapata ajira, kinachochelewesha inawezekana ikawa ni mambo ya bajeti.
 
Back
Top Bottom