Watumishi wengi wa serikali mnatia huruma mno, ni katikati ya mwezi ila nimepokea zaidi ya simu 10 mkiomba msaada wa pesa

Hao watumishi nafikiri ni hawa WA kawaida ambao hawana michongo hata humo ndani ya serikali na inajulikana kwann wanakuwa hvyo Ila maboss wao wako poa Kwanza wakisikia unasema hvyo wanakushangaa utumishi wa umma Kwa wenye vyeo sehem kubwa kubwa huwa raha asikwambie mtu.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Umeahazungumzia ma boss, posho ya mkurugenzi huwezi linganisha na mtumishi wa kawaida mimi nawazungumzia watumishi wa taasisi kubwa kubwa ambapo pia wanalipwa pesa ndefu na posho zao bado ziko juu tofouti na hawa wa TAMISEMI
 
Pongezi za dhati kutoka kwangu, mna nidhamu ya fedha sana pia ndoa nyingi ambazo zinahusisha mwalimu huwa zinadumu sana sijajua mna siri gani ya kipekee kiasi hicho?
Kuhusu ndoa hapo tuna %chache sana....ila sababu kuu ya kudumu kwa baadhi ya ndoa ni wenzi kuwaza sana namna ya kupata pesa than kufikiria mapungufu ya mwenzio eti sijui kachepuka,oo Mara bajeti ya kuku imetoka wapi wakati niliacha ya dagaa(kikubwa ushibe) ....kiufupi mmoja lazima ajifanya bwege.Ha ha haaa,ndoa hiz
 
We tukopeshe tu bwana, maisha kusaudiana. Tusipokulipa atakulipa Mungu.
 
Wewe ni mjinga na mshamba!!! Yan unadhalilisha watu?? Kwan MTU akitaka msaada ndio upeperushe mitandaoni!??amakweki wahenga walusema masikini akipata matako huliaaa mbwataaaaa
 
Hapo kama umenilenga mie asee dah we acha mastaer
 
Miaka saba hao watumishi mishahara haijapanda na wengine hawajapandishwa madaraja kutokana na roho mbaya za maafisa utumishi, kumbuka mtumishi akibaniwa na afisa utumishi kuwekwa kwenye orodha ya wanaotakiwa kupandishwa daraja hayo maumivu atayasikilizia kwa mwaka mzima kabla ya kusubiri bahati nyingine ya kuingia kwenye orodha......watumishi hao hao wanabanwa na waajiri kutumia muda wao wote kazini, huo muda wa kusimamia biashara zingine atautoa wapi? na nyie mnaowananga watumishi mkija kupata huduma mkakuta ofisi hazina watu mnaanza kutoa mapovu utafikiri sabuni ya omo.............waacheni watumishi wapumue, hii ya kuwananga mitandaoni kisa wameomba uwaazime pesa kidogo siyo poa........​
 
Ni watumishi wa serikali kutoka idara tofouti tofouti nyeti na zisizo nyeti, watumishi hawa wa Mama Samiah Suluhu Hassani wanatia huruma mno kila ifikapo katikati ya mwezi.
Mimi ni mtumishi wa umma na hapa nina akiba, na tena kuna allowance nyingine iko bado uhasibu inakuja, ni ya kuwa nje ya kituo cha kazi kwa siku sita, si haba. Sasa sijui unazungumzia akina nani hao
 
Mimi ni mtumishi wa umma na hapa nina akiba, na tena kuna allowance nyingine iko bado uhasibu inakuja, ni ya kuwa nje ya kituo cha kazi kwa siku sita, si haba. Sasa sijui unazungumzia akina nani hao
Unajitambua, hongera sana ukiendelea hivyo utafika mbali sana
 
Mkuu, au unakopesha kwa riba?!!
 
Walimu tuna haiba ya ustaha na aibu kuombaomba lakini siyo kwamba hatuishiwi ni ile tu tunatumia kwa level yetu ya salary ndogo yenye kulengwa na machoz
Tena nyie ndio wajinga mnaweka kadi kwa mruga chacha Myra mnakopa kwa riba.
 
Vijana wanatia huruma mno, unakuta kijana anapokea zaidi ya 2M posho humo humo ila katikati ya mwezi hana kitu na hapo wiki mbili alikuwa anakunywa pombe za laki 7 kwenye lounge huku akizungukwa na wanawake wa mjini.

Wanasikitisha sana
Dsh, hizi taarifa zingine zinatutesa sisi wengine tunaopokea 500k isiyo na posho yoyote katikati
 
Mkuu unajua mshahara wa VEO aliyefanya kazi kwa miaka 10 ana mshahara gani na unajua ukisema 45% savings atabakiwa na kiasi gani? Hongera kwa kuwa wewe unazo baada ya kupora na kupiga dili fulani.Maisha ya watumishi wa umma hasa wa serikali za mitaa waliopo katika ofisi za kata, vijiji na Miata ni Mungu ndo anajua wanavyoishi.Huwa ninawaoneaga huruma sana ila Sina namna nawatia moyo tu.Wengi wa wadada katika hayo maeneo ni chakula cha wafanyabiashara na viongozi fulani.Mungu awasaidie na akuhurumie na wewe kwa kujitutumua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…