Watumishi wengi wa Umma tumeachwa Kimaisha na Wajasiriamali wadogo

Watumishi wengi wa Umma tumeachwa Kimaisha na Wajasiriamali wadogo

Ubora ni nini ? na Watumishi ni Watu gani na Wajasiliamali ni watu gani....

Ubora; mwisho wa siku kila mtu yupo kwenye pursuit of happiness; kwahio ukiishi within your means basi utumishi unafaa (sababu una security na mwisho wa siku retirement plans - yaani Pension) Pili kwanini unafanya unachofanya ?, nina-assume wewe umekuwa Bwana Afya; Daktari au Mwalimu kutokana na Wito au kupenda kazi yako (hivyo you are living your dream) kwahio hata usipolipwa pesa nyingi wewe kama mwalimu ku-impact knowledge kwa watoto nadhani itakuwa a job worth while (living your purpose); Lakini tatizo ni kwamba watu wanafanya kazi fulani sababu ina ujira zaidi au hawana sehemu ya kwenda hence they are in the wrong occupation; pili kutokana na Sera mbovu wananchi wengi hawana disposable income.....

Watumishi: In the actual sense of the word, Mawaziri, Rais hadi waalimu madaktari wanajeshi n.k. wote hao ni watumishi experts wote kwenye hata big private companies bado ni watumishi kwahio utaona hao ni sehemu muhimu sana katika jamii tatizo they are on the wrong jobs (ni kama wamelazimishwa hivyo not enjoying the ride) na ukitoa wale wa juu wengi hawalipwi enough income kitu kinachopelekea kufanya kazi part time na ndio hao hao wenye vimiradi mtaani (yaani tunawalipa watutumikie ila bado ndio hao wachuuzi kitaa)

Wajasiliamali:hili neno tunalishusha sana maana yake, Bongo wengi ni wachuuzi na wabangaizaji; According to a Definition from Online: Mjasiriamali ni mtu ambaye anaandaa, anapanga au anasimamia biashara fulani, akikubali kukabiliana na hatari za kibiashara zinazoweza kujitokeza ilhali analenga kupata faida. Mjasiriamali mara nyingi huonekana kama mbunifu, chanzo cha mawazo anzilishi, mwenye kuvumbua bidhaa au huduma mpya na biashara (Now you tell me hao Bongo ni wangapi ? au kila Trader, Hawker na retailer ameshakuwa Mjasiliamali)? au kila Self Employed ni Mjasiliamali ?
Unenifungua kitu mkuu.. lakini ukiishi maisha mtaani, na ukiwa kwenye familia za hali ya kawaida tu, Kitaa ni kugumu sanaa mkuu... mimi kabla sijapata ajira nilipambana sanaa mtaani but changamoto ilikua pesa/Mtaji kufanya mishe za mtaa.. But nipo job now ninamishe mtaa ila mishe/Biashara, pesa yake haina uhakika wa %, Yaani unaweza pata leo elfu 3 kesho elfu50..
Kuna kauli niliambiwa na mfanyabiashara mmoja alisema "Bora nyie walau mnaokota senti kila mwisho wa mwezi" But hajui nyakati ngumu zinampata kila mtu, haijalishi entrepreneurs au Mtumishi wa umma. Wote tunapitia changamoto.. kikubwa mkuu ni kuishi unacho kiishi...
 
Hi!

Si Wajasiriamali wote kwamba wana maisha mazuri kuliko Watumishi wa Umma ila nataka kusema kuwa wapo Wajasiriamali wengi tu ambao hata leseni ya biashara hawana, Kodi hawalipi kabisa na Serikali haiwatambui lakini wana pesa kuliko wenye maduka ambao hulipa Kodi kwa VAT.

Kuna Jamaa anauza Ugali nyama choma, huyu bwana akiondoa gharama zote za uendeshaji anapata faida ya TZS 200,000/- mpaka TZS 300,000/- kwa siku. Maana yake huyu kwa mwezi amefeli amepata faida ya TZS 5,000,000/-. Pesa ambayo wanalipwa Watumishi Waandamizi Wizarani. Hapo ameshatumia pesa ya kutosha ndani ya huo mwezi mwisho wa mwezi ana TZS 5,000,000/- .

Mtumishi Mwandamizi akipata hiyo TZS 5,000.000/- ndipo aanze kutumia, atasave Million Moja au Laki 5 tu. Kuna dogo anauza chips Mwenge kwa siku analaza Laki 3.5. Huyu baada ya matumizi yake yote mwisho wa mwezi akichungulia akiba yake hakosi Milioni 7. Faida ya Milioni 7 kwa mwezi ni Watumishi wa Umma wangapi wanaipata? Labda majizi tu ambayo hawana amani maana jela inawaita kila siku.

Kuna muuza chips Keko kwa siku anapata faida ya Laki 4 . Na jinsi alivyo bahiLi yule kwa mwezi analaza mpaka Milioni 10. Halipi kodi hata mia, kajenga mjengo Madale nahisi hata baadhi ya Wabunge hawana Nyumba kama ile.

Tisidharauliane ndugu. Kuna Watumishi wengi tu wa chini wamewazidi maisha mabosi zao.

Mimi ni Mwajiriwa ila nakiri kuwa utajiri nitasikilizia redioni tu. Kwa mishahara hii tusubiri kifuta machozi cha kustaafu labda au tuibe tunawiri na mwisho tukafungwe.
Uongo
 
Kamdanganye anae MLA 0713 mazaako
 
Kudhibitisha kuwa husemi.uongo ambatanisha ushahidi wa malipo yake ya Mapato ya Kodi ya TRA sababu Kodi huendana na kipato ukitupa tu document ya Kodi anazolipa TRA tutajua unachoongea sahihi

Lete ushahidi wa Kodi za Mapato analipa TRA
Amesema halipi kodi TRA
 
Amepanga uchochoro kati ya nyumba na nyumba analipa laki 1 kwa mwezi.

Hakuna kodi ya serikali anayolipa.

Viazi na mkaa anabajaji zake 2 fasta tu kutoa soko kuu ni kama mita 100 tu.

Mafuta, kuku na nyama wanaleta wenyewe huku wanakimbi kwakuwa ni soko la uhakika.

Wafanyakazi anawalipa 40,00 kwa siku wapo 10.

Vitu vingine vidogovidogo madogo wanafata sokoni,nyanya,kabeji,vitunguu,n.k

Wafanyakazi chakula wanakula viewed.

Haya endelea kupiga hesabu zako uchwara nimekwambia watu wanapiga hiyo pesa bila wasiwasi! au nikuongezee wengine 2 pale Uhuru dampo?

1.anauza yeboyebo za mtumba anapiga faida 150,000 kwa siku.

2.anauza nguo za mtumba retail and wholesale anauza 2.5 million kwa siku utajua mwenyewe faida yake kiasigani.
Kifupi wahi tu mirembe hospitali ya vichaa Kwa kuandika vitu vya kuota .Eti nipige hesabu uchwara.Nitapigaje hesabu wakati huhaweka bei za vitu .Kuwa mfano hizo boda boda zinatumia mafuta shilingi ngapi? Mkaa bei Gani na anatumia kiasi Gani Kwa siku,Hao kuku na viazi, ,kabichi nk ananunua shilingi ngapi na kuuza anauza shilingi ngapi Kwa sahani Kwa wateja wangapi Kwa siku?

Hujaweka hizo bei kwenye maelezo Yako uchwara
Kifupi wahi hospitali ya mirembe kichaa Huwa kinaanza hivyo hivyo mtu unaanza kuwaza vitu hewa visivyokuwepo
 
Kuna jamaa anauza miguu ya kuku na vichwa huku mbagala anaingiza laki sita kwa siku
Asante motivation speaker Kwa uongo Kuna mwingine huko huko mbagala tuliambiwa na motivation speaker kuwa alianza biashara ya ujasiriamali Kwa kuuza punje moja ya Mchele ulioiva akauza na kuwa mvumilivu Sasa hivi biashara imekua na ana mahoteli makubwa Jiji zima la Dar es salaam na mengine ulaya😂🤩🤩
 
Weeee bwana! Unajua faida ya laki 2 hadi 3 kwa siku? Nenda ukalale!
Si ndio hapo mkuu?!!,Ina maana kwa mwezi ni km 6,000,000 hadi 9,000,000;Mara miezi 12 ni km Milioni 72 hadi Mil.108.Kwa miaka mitatu tu huyu mtu anakiwa awe anamiliki Hotel yake kubwa tu na Vitega uchumi kibao.Kweli za kuambiwa changanya na zako.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Heading na Content ni Maji na Mafuta.....

Heading (Watumishi Wengi wanazidiwa kimaisha na Wajasiriamali Wadogo) Content; (Kuna wajasiriamali wadogo wanawazidi kimaisha Watumishi Wengi) !!!!

Ukishaweka kuna; wapo hata watu wasiofanya kazi yoyote na wanamzidi kimaisha hata baadhi ya marais wa nchi..., Ukishaweka kuna, technically anything is possible..., Ila kufahamu ni vipi maisha ni magumu kwa majority wewe leo achia kazi yako yenye security(income na pension at the end of retirement) uone ni hao so called wajasiriamali wadogo watapambana wachukue hio kazi yako ili wapunguze madeni ya Vikoba (The Grass is Always Greener on the other Side)
Kweli kabisa mkuu.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Japo faida ulizoziweka ni kubwa sana labda unazungumzia mauzo...
Lakini mtaani kweli pesa ipo ukiwa mchapa kazi...
Wengi faida ni 20k-50k...sasa mtu anaepata 20k per day( bodaboda) kwa mwezi si ana 600k..huu ni mshahara wa mtumishi kabla ya matumizi
Mjini panahitaji akili, ukiwa mvivu utakuwa mtu wa makasiriko
 
Weeee bwana! Unajua faida ya laki 2 hadi 3 kwa siku? Nenda ukalale!
Ni kweli halijui hilo mkuu,, kwa faida hiyo atakuwa ametumia mtaji wa sh ngapi!? Wengine wana vyanzo vingine vya mapato tofauti na hizo chips inabidi afanye uchunguzi wa kutosha!
 
Ila kweli kuna mama ni mjasiriamali anuza tu supu hii ya kongoro na ndizi plus chapati n vikorokoro vyingine vya kula faida. yake si chini ya 30_40 kwa siku toa kila kitu ila ukiwaangalia hivi kama hawana hela
 
Back
Top Bottom