Watumishi wengi wa Umma tumeachwa Kimaisha na Wajasiriamali wadogo

Watumishi wengi wa Umma tumeachwa Kimaisha na Wajasiriamali wadogo

Na mtazidi kuachwa sana tu na wajasiriamali pamoja na wakulima hata wadowadogo. Tulisoma ili tuajiriwe tupate hela ila mambo yamebadilika waajiriwa tunaaibika kwa kuzidiwa kipato na wanaofanya shughuli ndogondogo na hawana elimu
 
Kifupi wahi tu mirembe hospitali ya vichaa Kwa kuandika vitu vya kuota .Eti nipige hesabu uchwara.Nitapigaje hesabu wakati huhaweka bei za vitu .Kuwa mfano hizo boda boda zinatumia mafuta shilingi ngapi? Mkaa bei Gani na anatumia kiasi Gani Kwa siku,Hao kuku na viazi, ,kabichi nk ananunua shilingi ngapi na kuuza anauza shilingi ngapi Kwa sahani Kwa wateja wangapi Kwa siku?

Hujaweka hizo bei kwenye maelezo Yako uchwara
Kifupi wahi hospitali ya mirembe kichaa Huwa kinaanza hivyo hivyo mtu unaanza kuwaza vitu hewa visivyokuwepo
Wewe ni mjinga kabisa! nimesema mwanzoni kabisa kuwa jamaa mauzo yake sio chini ya 1.5 million nikasema ukitoa gharama ya manunuzi ya vitu vyote faida anapata zaidi ya hiyo pesa laki 2 yenu.

Halafu unanambia habari za kodi! muuza chips na kodi wapi na wapi jamaa amepata gape analitumia wewe unadhani ni ndoto endelea kuota na ushamba wako.

Acha kunichosha kenge mweusi wewe! nimesema mwamba mauzo yake ni 1.5 + million kwa siku kama hauamini endelea kutokuamini unadhani mambo hayawezekani.
 
Endeleeni kushangaa tu watu wanapiga pesa! kuna jamaa pale Mwanza Uhuru dampo anauza chips mauzo ya million 1.5 kwa siku day and night sasa kwa mauzo hayo anakosaje hiyo faida kwa mfano.
Hawa hawajui kinachoendelea huko Mitaani
Watazame ile video ya mch. Kimaro wa Kijitonyama akilalamika mshirika wake kuuwawa ambaye alikuwa anafanya mauzo ya chips zaidi ya milioni 1 kwa siku.
Pesa ziko mtaani.
Mshahara wakevmtu anapiga siku mbili tu ashaupata
 
Acha ubishi wa kijinga wewe! unapajua Uhuru dampo kwanza? yule mwamba chips haziishi pale unazikuta kwenye kabati kama chapati.

1.Anawafanyakazi wanashift mchana na usiku.
2.kuna watu kazi yao ni kumenya viazi tu.
3.kuna watu kazi yao ni kuandaa Mishikaki tu.
4.kuna watu kazi yao ni kuandaa kuku tu.
5.kuna watu kazi yao ni kukaanga viazi tu.
6.kuna watu kazi yao ni kuchoma chips tu.
7.kuna mtu kazi yake ni kuhudumia vinywaji tu.
8.Ana watu 3 kazi yao ni kupokea pesa tu.
9.Anabajaji 2 zimepaki kwaajili ya kufata mkaa stoo ukiisha.

Tembea uone acha ubishi wa hovyo! yule jamaa ananyumba 3 amejenga, watu wanachukua take away pale kama hawana akili nzuri.
Kwa maandilizi hayo na hizo pilikapilika jamaa anapiga pesa zaidi ya wakuu wa mikoa.
 
Weeee bwana! Unajua faida ya laki 2 hadi 3 kwa siku? Nenda ukalale!
Elimu yake haijamsaidia, tungepata mamilionea wa kutosha kwa kuuza ugali nyama mtaani.

Ugali huo huo wa kuuzwa buku buku uzalishe faida ya laki tatu kwa siku, yaani kwa kifupi awauzie watu zaidi ya mia sita kitu ambacho hakiwezekani.

Kama anaona rahisi hivyo, aajiri kijana wa kumuuzia huo ugali 😀
 
Tena mbaya zaidi mtumishi ukijitahidi kuwa mjasiriamali unarudishwa nyuma hatua buku moja hata kwa uchawi mpaka uchakae
Tatizo wanajiingiza kwenye ujasiliamali kifarafara..,Kuna mwalimu mmoja hapa kafungua duka la spare parts za pikipiki karibu kabisa na duka langu linalouza hizohizo spare parts.., huyu anachofanya ni kuharibu biashara kwa sababu Bei za spare zinashuka sana na ninauza kwa panick,

Na kitu kingine kashindwa kuelewa ni kwamba mtu unapofungua duka na kukaa muda mrefu unakuwa umeshajijengea wateja wako wa kufa na kupona, hivyo kuwahamisha wateja hao kuwaleta kwako si kazi rahis hata kama utakuwa umeweka duka lako sehemu nzuri kimkakati,kazi ya kutengeneza wateja si kazi rahis,

Kitu kingine Mimi Ninazo Hadi store,yeye ndio kwanza anaanza,

Huyo mwalimu hata baiskeli ya usafir Hana..,na hii inanipa uhakika kwamba katika kufungua Hilo duka mkopo unahuska!

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Ninachojua kuna vita baridi kati watumishi wajasiriamali na wajasiriamali wasio watumishi.Watumishi hawapendwi kabisa.
 
Ninachojua kuna vita baridi kati watumishi wajasiriamali na wajasiriamali wasio watumishi.Watumishi hawapendwi kabisa.
 
Mtumishi maana yake MTUMWA,,,so hakuna mtumwa ambaye yupo financially free, unless otherwise.
 
Mtumishi maana yake MTUMWA,,,so hakuna mtumwa ambaye yupo financially free, unless otherwise.
 
Hakika mtu akiwa na kazi anaona asieajiriwa ana maisha mazuri.
 
Back
Top Bottom