Mungu aliumba watu and sio robots! Kuwepo na free will ni kuruhusu watu kuchagua mema na mabaya!
Kuumba watu na kutaka wafanye moja tu ni kama kuwalazimisha! Kama hatuwezi kutenda mabaya ila mema tu tungeitwa robots! Mungu hakuumba maovu soma kuhusu Adam na hawa,
Mungu hachunguziki! Kwa akili za kibinadamu huwezi ukamuelewa! Tusijihesabie sana haki na kujitweza kujiona tunaakili kuzidi kila kitu! Tujifunze kujishusha sisi bado sana, sijui kipi kinatupa kiburi! Hata katika jamiinzetu kuna mambo mabaya tu ukifanya lqizmq uadhibiwe, ata ile inner self inakuhukumu ukitaka kufanya jambo baya! Tumefundishwa upendo, amani n.k lakini bqdo tunataka kucriticise tu! Ndio kazi yetu.. hatuna jema!!
Upo uhuru wa kuchagua kile unachokiamini
Mkuu hivi “siku ya hukumu” wale msio na dhambi tunaambiwa eti mtakwenda “peponi” kula bata la milele maana huko hakutakua na kutenda dhambi tena na wenye “dhambi” tutakwenda “jehanamu” kwenye moto wa milele na hakutakua na kuongoka tena
Najiuliza je hao mtakao kwenda peponi mtageuzwa kama MAROBOTI ili msifanye dhambi?
Huyu Mungu alishindwa nini kutufanya hivyo toka alipo tuumba hadi atupitishe kwenye dunia ya dhambi na mateso yote haya?
Inamaana Mungu muweza na mjuzi wa kila kitu alikua hajui MADHARA ya kutupa free will watoto wake wapendwa anaotupenda kama mboni ya jicho lake?
Yaani alipotupa free will akatuandalia kabisa na moto wa jehanamu kwaajili yetu, kana kwamba haitoshi akazinguana na Shetani huko aliko akaona atutupie sie duniani ili acheze na free will zetu ili apate sababu ya kutuchoma milele?
Kana kwamba haitoshi kupitia “maneno yake matakatifu” akathibitishwa watakao kwenda kula bata ni wachache na njia yao nyembamba kuliko waovu
Tu assume wakristo ndio wametumia free will yao vizuri kwa kumuamini Mungu yesu roho mtakatifu… hawa ni 26% tu watu wote duniani
Na hapo tu assume wakristo sahihi ni walokole ambo ni kama 7% ya watu wote duniani
Hapo ukitoa walikole faki kama akina mzee wa upako unakuta walio sahihi ni chini ya 1% ya walio sahihi
👆kwa mchanganuo huo hapo juu japo sio sahihi sana utapata picha huyu mungu alidhamiria kabisa kutupitisha kwenye dhama ya kidunia na jehanamu milele
Hakuna mungu anaweza kuwa mjinga kiasi hicho mkuu