Kiuwezo wa kimahesabu yaani kuangalia uwezo wake wa engine na uzito anauobeba kimahesabu inakubali kabisa kupanda na 80km/hr.
Kwenye uhalisia haiwezi ikashindana na benz au scania kwa power (uwezo) wa kuinuka na zote mlimani hapo ndipo Sauli anapowaacha zaidi,ukija kukaa sawa mwenzio ameshafika mbali kutokana na uwezo wake wa kuinuka mlimani.
Kila gari ina sifa zake kwa maeneo yake,achana na scania mlimani labda umvizie sehemu za tambarale hapo kamtafutu tu na hiyo michana sehemu hizo za tambarale nayo iache iende mkuu,inamwagika sio kitoto na ndio maana Kureed/Hunters ya Mwanza japo ni gari lenye uwezo mkubwa au Phonex DVD wote hao wanageuka/wanaagukia kwenye kundi la mizaha kwa njia ya Mwanza,Kureed kuwamwaga watu Nyegezi saa tisa za usiku kawaida sana kwake wakati Ally's anawaleta chini ya saa sita usiku tena hadi saa 4 akivurugwaga vizuri sababu njia ya kati sehemu kubwa ni tambarale,pale michina ina shine mkuu kwakuwa hawana miinuko mingi inayowafanya washindwe kuchanganya haraka.
Kureee hiyo hiyo ingeenda Mbeya ingekuwa kwenye topthree za juu kila siku.
Hiko ndicho kilicho kwenye Sauli
Sent from my SM-A107F using
JamiiForums mobile app