Wauguzi walimwambia anawasumbua akajifungua sakafuni, kichanga chafariki

Wauguzi walimwambia anawasumbua akajifungua sakafuni, kichanga chafariki

Umeongea kweli yot
Jinsi mimba zinavyotesa jamani mtu umeteseka miezi 9 eti unampoteza mtoto wako kwa uzembe wa watu eeeh Mungu tusaidie jamani. Manesi baadhi wamekuwa na roho mbaya sana sijui kwanini ingawa wenye roho nzuri wapo.

Kama unajijua unaroho mbaya kwanini usomee sekta ya afya?? Hatua zichukuliwe kina mama wanateseka sana hasa hospitali za serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeongea kweli yote

Uishi Maisha marefu
 
Report ya Dr iliandika Hivyo au mama yako ndo alikuambia.

Unajua issue ya maternal and fetal complications.

Unajua abnormal labour zinazojitokeza mwanamke akiwa Labour.
Mkuu hizo code kama hufungui unatuacha njiani
 
Hai. Mkazi wa Wilaya ya Hai, Happiness Massawe (39), amegoma kuchukua mwili wa kichanga hospitalini kwa wiki moja akidai kifo cha mtoto wake kimetokana na uzembe wa baadhi ya wauguzi.

Happiness, aliyejifungua katika Hospitali ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro alisema Oktoba 31 mwaka huu alipohisi dalili za uchungu alikwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua na alipofika alipokewa na wauguzi.
Hata hivyo, alisema alipopata uchungu hakupewa ushirikiano badala yake alijifungulia sakafuni.

Juzi, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Hai, Itikija Msuya alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo akisema ameunda kamati ya kuchunguza ili kubaini kilichotokea siku hiyo.

“Kwa taarifa nilizopewa mtoto alizaliwa zero beating (akiwa amekufa) japo kuna dalili za uzembe ulifanywa na watoa huduma. Nimeunda kamati kuchunguza na watakaobainika hatua za kisheria zitachukuliwa,” alisema Dk Msuya.

Akizungumzia hali ilivyokuwa, Happiness alisema baada ya kupokewa hospitalini hapo alifanyiwa vipimo vyote ikiwamo ultra sound na kuambiwa itabidi alazwe asubiri wiki moja iishe kama hatojifungua kawaida, basi atafanyiwa upasuaji.

Hata hivyo, alisema Novemba 2 mwaka huu hali ilipobadilika alitoa taarifa kwa muuguzi aliyekuwa zamu, alimpima na kumjibu hasikii mapigo ya moyo ya mtoto na kumpeleka kwenye chumba cha ultra sound tena.
“Tulipofika huko yule muuguzi alimwambia mwenzake nisaidie kumpima huyu mama kwa kuwa sisikii mapigo ya mtoto na ana dalili za kujifungua. Akamjibu mnasumbua; huyu jana si alikuja hapa na nilimpima,” alisimulia Happiness.

Alidai muuguzi aliyempeleka akamwambia, “wewe mpime nataka uhakika, ndio yule muuguzi akanipima huku akisema mnasumbua. Akamuita (muuguzi) njoo usikilize si mtoto anacheza na unasikia mapigo yake. Yule (muuguzi) niliyeenda naye akaniambia nifanye mazoezi ya kutembea, nikawa nafanya hivyo, baadaye hali ikabadilika damu zikawa zinatoka mabongebonge huku nikiwa na uchungu mkali.”

Alisema alipoona hali hiyo alikwenda chumba cha kujifungulia na kumwambia muuguzi aliyekuwepo kuwa anasikia kusukuma mtoto na anatokwa damu nyingi. “Yule muuguzi alinijibu umeweka pamba usije chafua kitanda, nikamwambia ndio nimeweka pamba lakini akaniambia niache kusumbua niendelee kutembea.”

Alisema wakati anarudi wodini kwenye kitanda alichokuwa amelala alishindwa kutembea na kumlazimu kukaa chini huku akiomba msaada kwa kuwa alikuwa akisikia dalili zote za mtoto kutoka na damu ziliendelea kumtoka.
“Manesi walikuja wakaanza kuniambia sukuma huku nikiwa chini sakafuni, nilijitahidi lakini nikawa nasikia nguvu zinaniishia, mmoja wa wauguzi akawa anamwambia mwenzake pokea mtoto si unaona kichwa kile pale.

“Mwenzake akamjibu hapana huyu hasukumi napokea nini? Nikiwa nimelala pale chini wao wako kwa pembeni wananiangalia huku wakiniambia sukuma kwa zaidi ya nusu saa nikajitahidi mtoto akatoka akaanguka chini ndipo wakamnyanyua na kuniwekea kifuani huku wakiniambia niheme kwa kuwa mtoto hakulia alivyotoka ila alianguka chini sakafuni.”

“Baada ya dakika tano bado nikiwa chini sakafuni wakaenda kumuita daktari, huku wanaendelea kumkagua yule mtoto baada daktari kuja ndio akawambia wanitoe pale chini ndipo wakaniweka kitandani na kuanza kunifanyia usafi.”

Mwanamke huyo aliiomba Serikali kuwachukulia hatua wauguzi hao akidai kifo cha mwanaye ni uzembe wa wakunga na angepewa msaada wangeokoa mtoto huyo.

Mwananchi
Hospitali ni ya wilaya, nesi anayetuhumiwa kufanya uzembe ni wa hospitali ya wilaya, anayeunda tume ni mganga mkuu wa hospitali ya wilaya....!!! Yaani mtuhumiwa anaunda tume kujichunguza..!! Halafu kabisaa tunangoja majibu ambayo yakiwa mabaya yanaweza yakala kichwa cha muunda tume..!!! AJABU NA KWELI
 
Naunga mkono wafanye uchunguzi wa kina ili HAKI ipatikane kwa wote, nina maswali machache najiuliza:
1. Circumstance zipi zimepelekea mama kujifungulia sakafuni?
2. Kuanguka kwa mtoto ndio chanzo cha kufariki kwa mtoto?
3. Nurse kwanza hakusikia mapigo ya mtoto na akapelekwa ultrasound ikaona mapigo which information we should rely?
4. Kutoka kwa damu mabonge-mabonge na uchungu mkali je haikuwa tatizo kama abruptio placenta?
5. Kunaonekana kulikuwa na changamoto ya kusukuma, je second stage of labor ilikuwa vipi?
6. Kulikuwa na barrier yoyote ya mawasiliano yaliyosababisha kifo or any abuse of words kwenda kwa mama?
Mkuu naomba kuuliza hivi unaweza kusikia mapigo ya moyo kupitia ultrasound?
 
Ni kuona mkuu sio kusikia
Hata hivyo, alisema Novemba 2 mwaka huu hali ilipobadilika alitoa taarifa kwa muuguzi aliyekuwa zamu, alimpima na kumjibu hasikii mapigo ya moyo ya mtoto na kumpeleka kwenye chumba cha ultra sound tena.
“Tulipofika huko yule muuguzi alimwambia mwenzake nisaidie kumpima huyu mama kwa kuwa sisikii mapigo ya mtoto na ana dalili za kujifungua. Akamjibu mnasumbua; huyu jana si alikuja hapa na nilimpima,” alisimulia Happiness.

Alidai muuguzi aliyempeleka akamwambia, “wewe mpime nataka uhakika, ndio yule muuguzi akanipima huku akisema mnasumbua. Akamuita (muuguzi) njoo usikilize si mtoto anacheza na unasikia mapigo yake.

inafikirisha
 
Hela kila kitu ni hela ni Hilo tu kama wolper atapataje shida na anahela ??

Mnasema oh wanawake hawataki kutolewa na watu wakawaida ona Sasa shida ndio hizi unacheza na maisha je angeenda??
Kama ndio mawazo yako haya basi ndowa kwako itakuwa ni fungu la kukosa....ila pia siwezi kukuraumu kwa sababu ndio maisha uliyoyachgua,,chondechonde haya mawazo uliyonayo usiwaambukize wanao wa kike utatengeneza kizazi cha ma single mother.........
 
Kinakera kaka..

Yaani sisi vijana wadogo tumeamua kusoma uuguzi na kumeadapt mazingira mtaani kwa kupenda au kutopenda.

Ila hawa wakina nitingale wanakera Sana wanaona wamemaliza maisha.

Wanairudisha sana nyuma kada yetu ya uuguzi hii kada ikitaka iendelee.

Itoe mijimama yote ile kwenye Uongozi wa juu pale ...

Iwaweke fresh zenye Experience hawa Vijana kutoka Muhimbili,bugando,kcmc wenye Skilled na Accuracy katika kazi
Haisee kuna majimama yuko pale dodoma kwenye ofisi za baraza la wakunga ni shida...mbaya zaidi elimu zao ni ndogo na mengi yamepata zile nafasi kwa kubebwa
 
Kama ndio mawazo yako haya basi ndowa kwako itakuwa ni fungu la kukosa....ila pia siwezi kukuraumu kwa sababu ndio maisha uliyoyachgua,,chondechonde haya mawazo uliyonayo usiwaambukize wanao wa kike utatengeneza kizazi cha ma single mother.........
Mungu aliyehai atadili nawewe nahutokaa kuongea huo ujinga Tena
 
Walimwambia tu samahani,mtoto ametushinda.....yeye ni C-section....alipojisikia uchungu akakimbilia hospital njian alijisikia kupush,lakini Mwenyezi Mungu alimfikisha hospital salama,wauuguz wakampokea ingali anaendelea kupiga kelele kuwa anataka kupush,kumwingiza leba nesi mmoja akasema huyu ni C-section akapasuliwe nadhani baada ya kuona ule mshono....wakaleta kitanda chao apelekwe chumba husika ...kile kitendo cha kunyanyua mguu apande mtoto akazaliwa na kudondoka chini kwa kuangukia kichwa(mwisho wa siku wakaishia kusema sema "samahani mtoto ametushinda).....ukitaka kisa kingine nikuhadithie nilichoshuhudia mtoto wa kilo 5 alivyokufa mbele ya macho yangu kwa uzembe wa manesi wakati nikijisubiria leba(usiwe mkali tu,kila sekta haikosi watu wazembe ndugu)
Hebu tupee kidogo bibie. Halafu most wa kg 5 wanazaliwa wana kisukari
 
Haisee kuna majimama yuko pale dodoma kwenye ofisi za baraza la wakunga ni shida...mbaya zaidi elimu zao ni ndogo na mengi yamepata zile nafasi kwa kubebwa
Yanajiona Yamemaliza maisha...

Na ndo Yanafanya hii kada ionekane utumbo.
 
Mkuu naomba kuuliza hivi unaweza kusikia mapigo ya moyo kupitia ultrasound?
Kwenye ultrasound unaona ila ukipima local itabidi usikilize kwa kutumia kifaa maalum unachoweka tumboni mwa mama mjamzito kinaitwa Fetal scope.

So kama Unasikia mapigo ya mtoto chini ya 120b/min unaweza kugundua ni Dalali ya mbaya inayoashiria mapigo ya mtoto yako chini sana so mara zote huyu mama ataishia Ceaserean section...au kama Yuko stage ya Pili ya Labour unaweza kumzalisha ila lazima uandae Resuscitation machine mapema maana Anaweza kuzaliwa na Shida ya upumuaji
 
Naunga mkono wafanye uchunguzi wa kina ili HAKI ipatikane kwa wote, nina maswali machache najiuliza:
1. Circumstance zipi zimepelekea mama kujifungulia sakafuni?
2. Kuanguka kwa mtoto ndio chanzo cha kufariki kwa mtoto?
3. Nurse kwanza hakusikia mapigo ya mtoto na akapelekwa ultrasound ikaona mapigo which information we should rely?
4. Kutoka kwa damu mabonge-mabonge na uchungu mkali je haikuwa tatizo kama abruptio placenta?
5. Kunaonekana kulikuwa na changamoto ya kusukuma, je second stage of labor ilikuwa vipi?
6. Kulikuwa na barrier yoyote ya mawasiliano yaliyosababisha kifo or any abuse of words kwenda kwa mama?
Unajua shida mtu anakimbilia kulalamika ..

Mimi nishawahi kuzalisha mtu sakafuni ni circumstances zinatokea bila kuplain yaani mwanamke amekuja labour namwambia apande kitandani kwa ajili ya kumpima suddenly nakuta mtoto anaanguka chini shukuru Mungu Akuanguka nilimdaka maana nilikuwa tayari nina Gloves
 
Pole sana kwa huyo dada.

Ila kuna saa wanakuwaga sana na kauzembe hao manesi.
 
Unajua shida mtu anakimbilia kulalamika ..

Mimi nishawahi kuzalisha mtu sakafuni ni circumstances zinatokea bila kuplain yaani mwanamke amekuja labour namwambia apande kitandani kwa ajili ya kumpima suddenly nakuta mtoto anaanguka chini shukuru Mungu Akuanguka nilimdaka maana nilikuwa tayari nina Gloves
Hatari sana
 
Walimwambia tu samahani,mtoto ametushinda.....yeye ni C-section....alipojisikia uchungu akakimbilia hospital njian alijisikia kupush,lakini Mwenyezi Mungu alimfikisha hospital salama,wauuguz wakampokea ingali anaendelea kupiga kelele kuwa anataka kupush,kumwingiza leba nesi mmoja akasema huyu ni C-section akapasuliwe nadhani baada ya kuona ule mshono....wakaleta kitanda chao apelekwe chumba husika ...kile kitendo cha kunyanyua mguu apande mtoto akazaliwa na kudondoka chini kwa kuangukia kichwa(mwisho wa siku wakaishia kusema sema "samahani mtoto ametushinda).....ukitaka kisa kingine nikuhadithie nilichoshuhudia mtoto wa kilo 5 alivyokufa mbele ya macho yangu kwa uzembe wa manesi wakati nikijisubiria leba(usiwe mkali tu,kila sekta haikosi watu wazembe ndugu)
Huyo wa kilo tano ilikuwaje mkuu
 
Unajua shida mtu anakimbilia kulalamika ..

Mimi nishawahi kuzalisha mtu sakafuni ni circumstances zinatokea bila kuplain yaani mwanamke amekuja labour namwambia apande kitandani kwa ajili ya kumpima suddenly nakuta mtoto anaanguka chini shukuru Mungu Akuanguka nilimdaka maana nilikuwa tayari nina Gloves
Abnormal labour ni zipi mkuu?
 
Kwa maelezo hayo mtoto alifia tumboni 90% japo ngoja tusubir uchunguzi
 
Back
Top Bottom