Wauguzi walimwambia anawasumbua akajifungua sakafuni, kichanga chafariki

Chanzo zaidi huwa nini mtoto kufia tumboni? Na je mama anaweza kujua kua mtoto kafa tumbon? I.mean zile movements za mtoto
Yes, mtoto asipocheza within 8 hours tu unatakiwa uende hospitali haraka..

Vyanzo vya watoto kufia tumboni ni vingi tuu ikiwemo kasoro za kimwili za kichanga, damu kubadili mkondo kutoka kwa mtoto kwenda kwa mama (feto-maternal hemorrhage), maambukizi ya kichanga,ugonjwa wa maumbile ya kichanga, maambukizi ya mama, placenta iliyotenganishwa na ukuta wa ndani wa uterasi nk.
 
Hii kada imevamiwa na watu wenye tamaa wakidhani Kuna tofauti kubwa na kada nyingine shida inaanzia hapo wakikuta walivyo dhani sio
 
Lile jinga Sabaya limeacha nuksi ni vyema wazee wa mila wafanye tambiko kuondoa nuksi za yule kenge.
 
Kuna wauguzi wenye roho mbaya, sijui ni kwa nini wanampa cheti mtu wa namna hiyo. Maelezo yanasikitisha, ona mtoto alivyoanguka kwenye sakafu. Ni unyama uliopitiliza. Wachukuliwe hatua kali.
 
Hii cervical tear ni kuchanika msamba?

Naomba unieleweshe kwenye hizo mismanagement
 
Hivi sababu ni nini hasa?
 
Ni evil spiritual au?
 
Duuh [emoji24][emoji24]so many complications
 
Bad experience. Dah pole na pole kwa huyo mama jamani inauma sana kukosa mtoto wakati angezaliwa vzr tuu
 
Hospital za serikali hizi hazifai kabisa. Mke wa kaka angu na yeye mtoto ake alifariki hivo hivo yeye alitereza akadondokea ndoo ya maji machafu, nesi akamwambia deki mpumbavu ww akadeki.
Akamuomba nesi apande kitandani nesi akamwambia em nitoleee ujinga basi mim. Yule dada akaenda kupanda kitanda kibovu akadondoka nacho..
Ile kusimama tu anaomba msahada nesi amsaidie apande kitandani nesi hata ageuzi shingo kumuangalia mtoto akadondoka akavunjika shingo.
Nesi akaja akaanza kusema unaona umeua mtoto ako mwenyewe. Yule dada alilia eeeeh akuweza hata kuongea yule nesi akampa kitanda akamuacha na maiti ya mtoto wake usiku mzima.

Kesho yake kesi ikawa kesi
 
Ni Tanzania au?🙌 mie nadhan.labor wangeruhusiwa kuingia na waume zao ujinga ujinga ungepungua..maana wangekatwa kelebu za kutosha na waume zao
 
Ni Tanzania au?🙌 mie nadhan.labor wangeruhusiwa kuingia na waume zao ujinga ujinga ungepungua..maana wangekatwa kelebu za kutosha na waume zao
Ni hapa hapa TZ kwanza hyo hospital niliwai enda muona mtu kajifungua yani ni chafu sijawai ona aiseh. Alaf kitanda kimoja wazazi wawili na watoto wao hapo uchague kulaza mtoto au kulala ww.
 
Zamani wakunga walifanya kazi ya kuzalisha akina mama kwa mafanikio makubwa na hizi aibu ilikuwa nadra kuzisikia.
 
Hawa manesi oldschool, bado hawa wapenda insta wanaomalizia huku semester zao.
 
Kwani kakosea nini? (kuna lipi baya alilozungumza kuhusu huyo mama?)

Mbona mimi naona kama kaenda kujipanga kuwasema vibaya hao manesi au wewe mwenzetu umeelewaje?

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Ukimsoma vizur utagundua kwamba amemaanisha hao manesi huenda Wana maslahi madogo hivyo hawez kuwalaumu Sana kwa hicho walichkifanya.
 
Inaelekea ni hivyo mkuu, manesi mara nyingi sana wanaponzwa na kauli zao na kwenye hilo hawajifunzi, very poor customer care and unnecessary arguments na wagonjwa, sijui kwa vile wengi wao ni wanawake bse wanawake wenyewe kwa wenyewe huwa wanazinguana katika hali ya kawaida. Ukishamjibu mama mjamzito vibaya then yakatokea hayo lazima moto uwake. Kitu kingine ni ishu ya DENIAL, incase mtoto amefariki kwa mama ni ngumu kuadmitt kwamba amechangia chochote may be hakutoa ushirikiano inavyostahili so atatafuta loophole yoyote iliyojitokeza lawama ziende kwa manesi na hapo unakuta mtu ameshaongea utumbo wake kwa mgonjwa.
 
Manesi hua wanateteana sana...!!!hao watahamishwa tu wanapelekwa vijijini hukooo baasi hakuna kufukuzwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…