Wauguzi walimwambia anawasumbua akajifungua sakafuni, kichanga chafariki

Wauguzi walimwambia anawasumbua akajifungua sakafuni, kichanga chafariki

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Hai. Mkazi wa Wilaya ya Hai, Happiness Massawe (39), amegoma kuchukua mwili wa kichanga hospitalini kwa wiki moja akidai kifo cha mtoto wake kimetokana na uzembe wa baadhi ya wauguzi.

Happiness, aliyejifungua katika Hospitali ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro alisema Oktoba 31 mwaka huu alipohisi dalili za uchungu alikwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua na alipofika alipokewa na wauguzi.
Hata hivyo, alisema alipopata uchungu hakupewa ushirikiano badala yake alijifungulia sakafuni.

Juzi, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Hai, Itikija Msuya alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo akisema ameunda kamati ya kuchunguza ili kubaini kilichotokea siku hiyo.

“Kwa taarifa nilizopewa mtoto alizaliwa zero beating (akiwa amekufa) japo kuna dalili za uzembe ulifanywa na watoa huduma. Nimeunda kamati kuchunguza na watakaobainika hatua za kisheria zitachukuliwa,” alisema Dk Msuya.

Akizungumzia hali ilivyokuwa, Happiness alisema baada ya kupokewa hospitalini hapo alifanyiwa vipimo vyote ikiwamo ultra sound na kuambiwa itabidi alazwe asubiri wiki moja iishe kama hatojifungua kawaida, basi atafanyiwa upasuaji.

Hata hivyo, alisema Novemba 2 mwaka huu hali ilipobadilika alitoa taarifa kwa muuguzi aliyekuwa zamu, alimpima na kumjibu hasikii mapigo ya moyo ya mtoto na kumpeleka kwenye chumba cha ultra sound tena.
“Tulipofika huko yule muuguzi alimwambia mwenzake nisaidie kumpima huyu mama kwa kuwa sisikii mapigo ya mtoto na ana dalili za kujifungua. Akamjibu mnasumbua; huyu jana si alikuja hapa na nilimpima,” alisimulia Happiness.

Alidai muuguzi aliyempeleka akamwambia, “wewe mpime nataka uhakika, ndio yule muuguzi akanipima huku akisema mnasumbua. Akamuita (muuguzi) njoo usikilize si mtoto anacheza na unasikia mapigo yake. Yule (muuguzi) niliyeenda naye akaniambia nifanye mazoezi ya kutembea, nikawa nafanya hivyo, baadaye hali ikabadilika damu zikawa zinatoka mabongebonge huku nikiwa na uchungu mkali.”

Alisema alipoona hali hiyo alikwenda chumba cha kujifungulia na kumwambia muuguzi aliyekuwepo kuwa anasikia kusukuma mtoto na anatokwa damu nyingi. “Yule muuguzi alinijibu umeweka pamba usije chafua kitanda, nikamwambia ndio nimeweka pamba lakini akaniambia niache kusumbua niendelee kutembea.”

Alisema wakati anarudi wodini kwenye kitanda alichokuwa amelala alishindwa kutembea na kumlazimu kukaa chini huku akiomba msaada kwa kuwa alikuwa akisikia dalili zote za mtoto kutoka na damu ziliendelea kumtoka.
“Manesi walikuja wakaanza kuniambia sukuma huku nikiwa chini sakafuni, nilijitahidi lakini nikawa nasikia nguvu zinaniishia, mmoja wa wauguzi akawa anamwambia mwenzake pokea mtoto si unaona kichwa kile pale.

“Mwenzake akamjibu hapana huyu hasukumi napokea nini? Nikiwa nimelala pale chini wao wako kwa pembeni wananiangalia huku wakiniambia sukuma kwa zaidi ya nusu saa nikajitahidi mtoto akatoka akaanguka chini ndipo wakamnyanyua na kuniwekea kifuani huku wakiniambia niheme kwa kuwa mtoto hakulia alivyotoka ila alianguka chini sakafuni.”

“Baada ya dakika tano bado nikiwa chini sakafuni wakaenda kumuita daktari, huku wanaendelea kumkagua yule mtoto baada daktari kuja ndio akawambia wanitoe pale chini ndipo wakaniweka kitandani na kuanza kunifanyia usafi.”

Mwanamke huyo aliiomba Serikali kuwachukulia hatua wauguzi hao akidai kifo cha mwanaye ni uzembe wa wakunga na angepewa msaada wangeokoa mtoto huyo.

Mwananchi
 
Hai. Mkazi wa Wilaya ya Hai, Happiness Massawe (39), amegoma kuchukua mwili wa kichanga hospitalini kwa wiki moja akidai kifo cha mtoto wake kimetokana na uzembe wa baadhi ya wauguzi.

H

Mwananchi
Daah nimesoma hii habar mpaka mwili umenisisimka Kuna baadhi YA manesi Ni mashetan Ila wako kwenye umbo la binadamu.Imagine dada wa watu kateseka na mimba miez 9 alafu anakuja kupoteza mtoto kizembe namna hiyo.

Hili litapita kama mengine tu na wala hakuna hatua yoyote itachukuliwa maana nchi haieleweki iko kwenye muelekeo upi kila mtu Ni bosi kwa nafasi yake hakuna uwajibikaji kabisa.
 
Jinsi mimba zinavyotesa jamani mtu umeteseka miezi 9 eti unampoteza mtoto wako kwa uzembe wa watu eeeh Mungu tusaidie jamani. Manesi baadhi wamekuwa na roho mbaya sana sijui kwanini ingawa wenye roho nzuri wapo.

Kama unajijua unaroho mbaya kwanini usomee sekta ya afya?? Hatua zichukuliwe kina mama wanateseka sana hasa hospitali za serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah nimesoma hii habar mpaka mwili umenisisimka Kuna baadhi YA manesi Ni mashetan Ila wako kwenye umbo la binadamu.Imagine dada wa watu kateseka na mimba miez 9 alafu anakuja kupoteza mtoto kizembe namna hiyo.

Hili litapita kama mengine tu na wala hakuna hatua yoyote itachukuliwa maana nchi haieleweki iko kwenye muelekeo upi kila mtu Ni bosi kwa nafasi yake hakuna uwajibikaji kabisa.
Hivi habari kama hii Mtu kama Rais au Waziri Mkuu hawaioni, au ni habari ndogo sana kwao?
Hawajui Manesi kama hawa wamesababisha vifo vya watoto wangapi!?

Kwa habari kama hii ndo nnapomkumbuka Magufuri, japo sikuwahi kukubaliana nae kwa baadhi ya mambo lakini ikija habari ya mwananchi Masikini kunyanyasika, alikubari kusemwa kuwa hafati utawala wa sheria.
 
Comment ya ovyo sana hii emu jaribu kuvaa viatu vya huyo mama alafu ndio ungekuwa mume wake na huyo mtoto ndio mlikuwa mnamtarajia kwa hamu ungeandika hivi kweli?
Nchi hii kila taasisi imeoza tujiulize kama taifa hivi Hali hii hadi lini?Nani anahusika ?Tukipata majibu kama taifa ndipo tuanze kulaumu
 
Hai. Mkazi wa Wilaya ya Hai, Happiness Massawe (39), amegoma kuchukua mwili wa kichanga hospitalini kwa wiki moja akidai kifo cha mtoto wake kimetokana na uzembe wa baadhi ya wauguzi.
Nimesoma uuguzi ila sitamruhusu mwanangu asomee hii course.

Mimi nikienda kusoma bachelor hii course ya uuguzi nitabadilisha na ndo nilichokiamua.

Uuguzi hawa wamama watu wazima ndo wanaouharibu sana mimi nimeshawahi kufanya kazi HC moja ya serikali kiukweli nilikuwa nagombana sana na hawa mama nurse watu wazima wana majibu ya ovyo kwa wagonjwa na hawana utu.

Yaani mimi ni muuguzi ila sijivunii kuwa muuguzi.

Kwa sasa nafanya biashara tu
 
Hiko kizazi cha hiyo mijimama kinaenda kuisha very soon...
 
Back
Top Bottom