Acha ukiazi unanitisha kuniblock na usilazimishe niamini unachokisema ati ndio kuelewa.
Kama hiyo ndio maana yako ya kuelewa basi mimi sio kukuelewa tu bali sikubaliani na wewe...
Waislam mna namna ya ibada zenu? Kwanini mnatofautiana na baadhi ya misikiti? Kuna Shia kuna Sunni?
Kuna wale wanaofata ratiba na matangazo ya Bakwata, kuna wale wasioyaamini wala kufuata maagizo yao.
Kwenye mfungo pia mnatofautiana za kuanza na kumaliza ,hapa hapa bongo, kuna wale hivi na wengine vile ila nyote mnaamini katika kitabu kimoja.
Kuna uzi humu mdau (muislam) aliuleta kua hakuelewa jinsi watu wanaswali baadhi ya misikiti na wadau wakamshauri misikiti anayopaswa kwenda isiyo na mkanganyiko kwake kwa jinsi yeye anavyoswali (nautafuta huu uzi nikiupata nakuletea au si ajabu hata wewe ulichangia)
Sikutishi nakuelewesha na kukuambia ukweli POPOMA wewe.
Suala la mwezi muandamo ni suala pana linahitaji maelezo mapana.
Ila kiufupi wale wanaofuata BAKWATA wako sahihi na wale wanaofuata mwezi wa kimataifa wako sahihi.
Tanzania BAKWATA ndio chombo cha kiislam,na sheria ya uislam kiongozi ndio anaetakiwa atoe tamko kuhusu na masuala ya kidini ila akiwa ndani ya mstari wa dini.
Qur'an surah ya 2 inasema"ukionekana mwezi basi na watu wafunge,na ukionekana na watu wafungue".
Katika kuuona mwezi inahitajika watu/mashahidi watakaothibitika mwezi kuwa umeonekana,kesha mwenye haki ya kuutangaza mwezi sio mtu yeyote isipokua ni MUFTI wa eneo husika.
Hivyo MUFTI hajakosea na pia wale wanaofuata mwezi wa kimataifa pia hawajakosea wote wamefunga kwa ithbati ya kuuona japo yupo anaetaka kuuona ndani ya mipaka na yupo ambae hata akiuona nje ya mipaka anaukubali.
HIVYO SUALA LA MWEZI HAKUNA SHAKA WOTE WAMEFUATA QUR'AN INAVYOSEMA.
Walipotofautiana wao ni kuwa wapo wanaufuata mwezi muandamo wa kimataifa(Answar) na wapo wanaotaka mwezi wa kitaifa ndio waukubali(BAKWATA).
Hawajatoka nje ya maandiko wote wako sahihi maana miandamo yote inakubalika.
Kuhusu ibada ya swalah kuna nguzo za swalah ambazo wote tunatakiwa tuzifuate,na kama ikatokea kuna kundi likaenda kinyume na nguzo za swalah basi WAMEKUFURU.
Mfano SHIA na AHMADIA wamekufuru kwasababu tatu mpaka nne zifuatazo;
1)Shahada wameongezea maneno yao ambayo hayatakiwi,shahada ya uislam inasema"Hakuna Mola apasaye kuabudiwa isipokua Mungu,na Muhammad ndiye mja wake na Mtume wake".Shia shahada yao wanasema"Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokua Mungu,na Ally ni mjumbe wa Mungu na Muhammad ni mtume wa Mungu".
Shahada ya mashia ni shahada YA UONGO NA KUKUFURU.
2)Mashia wanapinga viongozi wakubwa walioongoza baada ya mtume ilhali uislam umewatukuza hao viongozi na atakayewapinga ji sawa kampinga Mungu na Muhammad.
3)Mashia wanakosea kwenye ibada zao hawafuati nguzo za swalah ambazo Muhammad alizielekeza.
Na hao AHAMADIA ndio MAKAFIRI kabisa kwasababu wamemkataa mtume MUHAMMAD wanaamini wana mtume wao anaitwa AHMAD.
Ndio maana wanajiita AHMADIA.
Tukija kwa sunni hili ni dhehebu ambalo wao wamejinasibisha na kuzitunza na kuzihifadhi sunnah za MUHAMMAD ambazo ni Hadithi na historia yake kwa ukamilifu.
Hivyo hawa hawana shinda yoyote hawajakufuru.
Point yangu iko palepale,uislam una sheria zake za kila kitu hadi za KUABUDU,ukizikiuka basi UMEKUFURU.
Na huyo jamaa hajakosea kuuliza maana ametaka kujua ili asije akafanya vitu ambavyo vitamkufurisha na akatoka katika uislam bila ya yeye kujua.