Imani sahihi ni kumuabudu Mungu katika roho na kweli huku ukijiepusha na ibada za sanamu.
Kuwa na masanamu yaliyojaa makanisani mwenu ni ibada ya kishetani.
Kumuamini Mariam ni ibada ya kishetani. Mariam anaitwa Malkia wa Mvinguni katika Ukatoliki. Hii title ya Malkia wa Ulimwengu imekatazwa kutumika katika Biblia.
Yeremia 7:18
[18]Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.
Vile vile ukisoma Yeremia 44 :17-19
17 Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya. 18Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa. 19 Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimwandalia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mimiminiko, waume zetu wasipokuwapo?
Hizo ndizo ibada za sanamu zinazokatazwa.