Nini kipimo cha usahihi? Wewe umewahi ku challenge unachoamini? Umewahi kutafiti vizuri ( Acha zile seminar zenu za makuzi kiroho) historia ya Kanisa? Historia ya Bible? Imani ya mababa wa awali wa Kanisa walau Karne ya kwanza na pili? Ibada zao? Tatifi huko ulipo, tafuta facts kupitia sites rasmi za Kanisa Katoliki, ukiweza Lutheran n.k walau makanisa yenye at least 500 years.
Tatizo umeona mchungaji wako anatoa pepo kwa jina la Yesu, ujumbe wake ni kutoka kwenye biblia tu! Ukaamini pia mafundisho yao juu ya imani zingine. Ukaamua facts zipo huko na imani zingine ukaamini za uongo.
Nimewahi kuhudhuria hizo seminar Ufufuo na Uzima, lengo kuona bases za facts zao lakini ilikuwa aibu! Hapo nilibaki kumuuliza Mungu, why such lies anaziacha zijenge ngome kwa watu wake.
Kwa ufupi wengi mnawaamini watumishi sababu ya ile nguvu mnayoamini anayo na kupitia kibali hicho mnaamini anasema kweli ya Mungu! Na vile anaweka na mistari ya biblia mnajua ndio ukweli wenyewe! Private interpretation, Very dangerous!