Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

Watakuwaje na akili ndogo wakati wanamtumikia Mungu wa Dunia hii? Mbona hujiulizi mlokole au msabato wa kweli anajua maandiko sawasawa kuzidi askofu mwenye PhD wa Roma ?? Ni mgawanyo tu. Wa mbiguni Wana wana tunu za mbiguni na Wa Dunia Wana tunu za duniani.
Kwa kweli Kuna Raha.
Eti msabato na Mlokole wanaijua Biblia kuliko waliowaletea.

Maajabu hayajawahi kuisha duniani.
 
Nenda kamsome ni moja ya mashehe wakubwa Sana kwa sasa , Kuna zakirinaiki na uthaman
Muangalie kidogo hapa , ila najua kingereza kwako ni shida jitaidi tafuta mtu akufanyie translation


Kuna vitu kabla hujaviandika fanya utafiti. Zakiri Naik na Huyo uliye mtaja si wasomi katika wasomi wa Dini ya Kiislamu.

Namfahamu kiasi ila kwa jinsi navyo mfahamu hawezi kusema hicho ulichokidai wewe.
 
Kunakutengeneza sanamu na kuziabudu.
Mungu alikataa kutengeneza samu na kuziabudu. Ndiyo maana hapo chini alimwamuru Musa atengeneze nyoka sanamu ya nyoka wa shaba. Ili atakaemuangalia kwa Imani atapona. Hii haikuwa na maana ya Kuwa walikuwa wanaabudu na kusujudu Sanamu ya Nyoka wa shaba.

Hesabu 21:8-9
[8]Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.
[9]Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

Pia Mungu alimwamuru Mussa atengeneze sanamu za Makerubi(Malaika) na kuziweka mahara Patakatifu PA Patakatifu lilipokaa Sanduku la Agano. Je Mungu alikuwa anavunja Amri yake aliyoitoa mwenyewe ya kutengeneza sanamu???. Jibu ni laaa Bali hataki kuabudu sanamu siyo kutengeneza tu.
Wakatolic hatuabudu sanamu Ila tunasanamu mbalimbali katika kanisa Kama ilivyo sanamu katika Sanduku la Agano la Mussa.

Kutoka 25:18-20
[18]Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku.
[19]Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.
[20]Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema.


Tumekatazwa kuabudu sanamu na kuzisujudia ndivyo amri ya kwanza ya Mungu inamaana Usiabudu miungu mwingine. Miungu mingine ndiyo sanamu, na vitu vingine vinavyopewa Nafasi ya Mungu. Na wakatolic hatuzipi sanamu Nafasi ya Mungu wetu.

Kwa kufundishwa kwa kupotoshwa.
Tumsifu Yesu Kristo.
Yaani kutokufundishwa Bible kumewafanya waroma mmekuwa wahanga wakubwa wa maandiko matakatifu Mungu awasaidie yaani unaandika matakataka yote hayo kutetea misanamu??
 
Kuna vitu kabla hujaviandika fanya utafiti. Zakiri Naik na Huyo uliye mtaja si wasomi katika wasomi wa Dini ya Kiislamu.

Namfahamu kiasi ila kwa jinsi navyo mfahamu hawezi kusema hicho ulichokidai wewe.
Ndio maana nimekuwekea link YouTube
Ila nimekwambia kwa sababu hujui kingereza tafuta mtu akuelezee , na asiwe muongo
 
Yaani kutokufundishwa Bible kumewafanya waroma mmekuwa wahanga wakubwa wa maandiko matakatifu Mungu awasaidie yaani unaandika matakataka yote hayo kutetea misanamu??
Acha ujinga bila wakatoliki hakuna ukristo

Jibu wewe ungetokea wapi bila katoliki?

Ndio maana nimeweka ukristo ni kuamini Yesu ni Mungu na kuamini utatu mbali na hapo hakuna ukristo

Kuna vitabu watu hawakukubali ila msingi umebaki pale pale Yesu ni Mungu na kuna utatu

Wakristo vitabu vyake vipo ila kwa waislamu walivichoma moto na wakaweka wanavyo kubaliana

Alie fanya kazi ya kuchoma Koran anaitwa Othman, mpaka leo haijukani Koran ipi alichoma
 
Nimesoma , wanaelezea jiwe halina maana , na kwamba Umar ndio yupo sawa Kuliko muhammad , alipo sema jiwe halina maana yoyote

Kwenye hili Mimi nampinga Umar na namaupport Muhammad kwamba jiwe linamaana
Tukikubali halina maana tunampinga mpaka Allah alielishusha
Nadhani nimeshakujibu. Hata shetani ameumbwa na Mungu, makafiri wameumbwa na Mungu na vinginevyo. Wote hawana maana.
 



Uthaman kachomoa betri, Kuna msemo unasema , ukesema ukweli hautaji kuwa na kumbukumbu

Ila ukiwa unaongea uongo kumbukumbu inatakiwa iwe juu Sana ndio kilichomkumba uthaman

Sasa haujaelewa nini? Mfano wewe umezaliwa kwenye familia ya kikafiri. Ukawa haufati ibada zao bali unaona. Unajua kamba Ibrahim alikuwa kwenye jamii ya makafiri kabla ya hapo lakini hashirikiani kuabudu masanamu? Usiwe unaropoka.
 
Kwa kweli Kuna Raha.
Eti msabato na Mlokole wanaijua Biblia kuliko waliowaletea.

Maajabu hayajawahi kuisha duniani.
Sijawahi kumuona mu R.C akienda kanisani na note book na kalamu kutake note ya doctrine kama wapo ni wachache saana. Wengi huenda kanisani wakilenga kukomunika tuu, average R.C member wanaijua bible kidoogo saana. Kupata ma sakramenti kama ubatizo, komunyo na kipaimara sharti ufunzwe sala uzielewe kama kanuni ya imani na Q&A za katekisim yetu. Mpaka napata hizo sakramenti sikuwahi kufunuliwa bible ktk mafundisho. Leo hii ukimchukua mtoto wa Sunday school wa Kiprotestant na jamaa mwenye level ya kufuata mafundisho ya ndoa uwaweke ktk bible literacy utashangaa mtoto wa Sunday school alivyomeza vifungu vya bible na kufanya uchambuzi wakti mwenzangu na mimi mtu mzima Mrumi umuambie tu afungue kitabu cha Yuda ktk bible nakuambia atakitafuta toka saa mbili hadi saa tano. Sisemi haya kwa ubaya bali ni kwa namna nilivyo experience. Nafikiri falsafa za Ki R.C na kiprotestanti zinatofautiana kiasi mfano R.C ibada zake ziko ktk ratiba kabisaa inatoka misa ya neno inakuja misa ya sadaka n.k ilhali huku kwenye uprotestanti misa anaongoza Roho mtakatifu..Pastor anaweza panda altareni na somo aliloandaa jana lakini akaambiwa na Roho mt hakuna kufundisha ulichoandaa jana ila utafundisha nitakachokupa muda huu huu. Naiheshimu R.C kwa maana lilikua ni daraja katika kumjua Kristo.
 
yaan watu kama huyu.... ukute form 4 failure ... elimu ya dini amefundishwa na wahuni wataka sadaaaka ambao wameunganisha mabati na matulu bai baada ya kugombani sadaka kanisa fulani anakuja kujimwambafai hapa anajua kila kitu..... ukiacha madhaifu ya kibinadamu hv unajua upadre unasomwa miaka mingap?????? na baada ya kupta ufaulu gani form six???? msipende ubishano wa vijiwe vya kahawa kwenye imani za watu?????? imarishe huku mnako kuamini watu waone ubora wenu waungane nanyie sio kuhubili mambo ya kanisa jingine ambayo uyajui zaidi
tunasikia mnasoma miaka 7. lakini bado hamumjui Mungu, na mnakataa wokovu na nguvu za Mungu. ndio kitu cha kushangaza. hautakuja kulijua hili hadi utakapokubali kuokoka na kubadilika, utajilaumu kwanini ulipoteza muda.
 
Wanaona aibu kuita na kuandika Roman siku hizi
Cijajua hasa lini ilikua inaitwa Roman instead of Catholic as far as I know the ancient apostolic Creed named it as Catholic and not otherwise
 
Watakuwaje na akili ndogo wakati wanamtumikia Mungu wa Dunia hii? Mbona hujiulizi mlokole au msabato wa kweli anajua maandiko sawasawa kuzidi askofu mwenye PhD wa Roma ?? Ni mgawanyo tu. Wa mbiguni Wana wana tunu za mbiguni na Wa Dunia Wana tunu za duniani.
Samahani apa umeongelea uwezo wa kusoma maandiko na kuyakariri Kisha kunukuu Kama vitabu vya kina kiyosaki au unaongelea uwezo wa kuinterpreti kile kilichokusudiwa kuandikwa .Kama unaongelea kuhusu kukariri naungana na wewe
 
Back
Top Bottom