Waumini wa kikristo mnafuata muongozo gani? Nijibu maswali haya

Yesu wa kwenye biblia ninae mjua mimi ni sawa na nabii Issa aliyeumbwa na Mungu tokea tumboni mwa mama yake Mariam.
Huyo mwingine aliyekuwepo kabla ya Ibrahim sijawahi msikia, na kama alikuwepo basi hakuwa anaonekana.
 
Kaujue uislamu baada ya kuujua ukristo
 
Sio marufuku kusoma biblia... ila wakristo kusema Qur'an kipengere
 
Yesu wa kwenye biblia ninae mjua mimi ni sawa na nabii Issa aliyeumbwa na Mungu tokea tumboni mwa mama yake Mariam.
Huyo mwingine aliyekuwepo kabla ya Ibrahim sijawahi msikia, na kama alikuwepo basi hakuwa anaonekana.
So huyu Yesu anayeongea kwenye injili ya Yohana ni yupi? Na amesema kwa ujasiri mkubwa kuwa ALIKUWEPO kabla ya Ibrahimu.
Tena anaendelea kusema hivi
Yohana 6:61-62
[61]Naye Yesu akafahamu nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanalinung’unikia neno hilo, akawaambia, Je! Neno hili linawakwaza?
When Jesus knew in himself that his disciples murmured at it, he said unto them, Doth this offend you?
[62]Itakuwaje basi, mmwonapo Mwana wa Adamu akipaa huko alikokuwako kwanza?
What and if ye shall see the Son of man ascend up where he was before?

YESU ANATHIBITISHA KWA MARA YA PILI KUWA ALIKUWAKO KABLA YA KUJA HAPA DUNIANI.
ISA HAKUWEPO KABLA YA KUJA DUNIANI ILA ALIUMBWA KAMA ADAMU KATIKA TUMBO LA MAMA YAKE.

BIBLIA IKO WAZI, MARA MBILI YESU ANATHIBITISHA KUWA NI TOFAUTI NA ISA BIN MARIAM, UKISOMA PIA SURAT MARIAM UTAGUNDUA HILI.
 
We umbishi aisee. Acha kusoma biblia kama gazeti. Umezaliwa kwa ukristo so ujui chochote
 
Mleta mada ivi ushawahi jiuliza kwanini vitabu vya wanasayansi wakubwa au vitabu vya sayansi havijawahi kutafsiriwa katika lugha yako lakini vitabu vya dini mpaka lugha za makabila wanavyo...
 
Mleta mada ivi ushawahi jiuliza kwanini vitabu vya wanasayansi wakubwa au vitabu vya sayansi havijawahi kutafsiriwa katika lugha yako lakini vitabu vya dini mpaka lugha za makabila wanavyo...
Kama kitabu gani hakina tafsri na wanasayansi wote wamekopy kwenye Quran.
 
We umbishi aisee. Acha kusoma biblia kama gazeti. Umezaliwa kwa ukristo so ujui chochote
Ok sawa unayejua mambo yote.
Ila Mimi Yesu ni wa mwisho na hakuna mwingine.
Maandiko yako wazi kabisa, haitaji uingie Rohoni Ili uelewe, Injili ya Yohana sio kama Ufunuo wa Yohana, au kitabu Cha Danieli.
YESU WA INJILI YA YOHANA NI TOFAUTI NA ISA BIN MARIAM.
MIMI SITABISHA KAMA UTATUMIA KITABU CHA QUR'AN TAKATIFU KUFUNDISHIA, MAANA HAINIHUSU.
ILA MAANDIKO MATAKATIFU YA BIBLIA NILIYOYASOMA KWA ZAIDI YA MIAKA 10 TOKEA NIKIWA MDOGO YAKITUMIKA VIBAYA, NITASIMAMA KUITETEA.
I END MY CASE, NO MORE ARGUMENTS.
YESU ANAKUITA LEO AKUOKOE, USIFANYE MOYO WAKO KUWA MGUMU, NYAKATI ZINAKUJA UTAJUTA KWANN HUKUAMINI HABARI SAHIHI ZA YESU NA HAKUTAKUWA NA MSAADA.
 
Waliotuletea dini walituweza kwakweli
Imani ni bora kuliko dini.

Maoni yangu!
 
alitumwa kwa Wayahudi na hakutumwa kwa mataifa, lakini baada ya ufufuo wake, mitume wake walianza kusambaza ujumbe huo kwa mataifa yote duniani.
He kumbe!! Basi hapa ngoja niingie chimbo ila nitarudi
 
Unateseka nini labda? Acha kuwashwa na imani za watu, kama unaona yako ni bora kaa nayo. Ata mashoga wanaona wanachofanya ni sahihi kwa akili zao, na nyie mnaona mpo sahihi sasa ni hivi ishi na li imani lako kimpango wako, wala hakuna mtu atakusumbua labda wala uwalazimishe wewe.
 
Sawa kwa hiyo tushike lipi?? La kristo mtume au mungu?
Kwa Wakristo, Yesu Kristo si tu mtume, bali pia ni Mungu aliyekuwa na mwili wa kibinadamu. Kwa mujibu wa imani ya Kikristo, Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu, aliyekuwa na asili ya kimungu kabla ya kuzaliwa kama mwanadamu. Wakristo wanakiri kuwa Yesu ni Mungu aliyejifunua kwa mwanadamu na alitolea dhambi za ulimwengu. Hivyo, Yesu Kristo anachukuliwa kama Mungu na mtume kwa pamoja katika imani ya Kikristo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…