Wauzaji wa matofali badilikeni

Atlast nimempata

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
386
Reaction score
680
Siku hizi biashara ya kuuza matofali imeshamiri sana kutokana na watu wengi kununua mashine za kutumia umeme katika kuchanganya cement na mchanga.

Tatizo ni kuwa wafanyabiashara ya matofali wote ni kama wanakariri bei ya soko ni 1,000 au 1,100 au 1,200. Sasa unakuta kila mmoja ana matofali kibao yamemdodea kutokana na usawa mgumu; hata wajenzi hawawatumi mafundi wanaenda kununua wenyewe kwa kubargain.

Mimi nilikuwa nataka kama tofali 3,000 hivi nikapitia wauza tofali kama 5 hivi wote wanakomaa kwa bei moja ya 1,100? Mimi nilikuwa nahitaji kwa 800 au 900 kwa kulipa 2.4m au 2.7mil.

Sasa wewe unakomaa na bei yako alafu tofali zinakudodea, si ungechukua hiyo 2.7 kwa vile nanunua mengi ukazungushia hiyo hela hata kama faida ni kidogo kuliko kukomaa na ndizi bei 200 wakati zinaanza kuoza? Hata tofali zikikaa sana hupoteza uimara wake.

Wanajanvi nisaidieni hili limekaaje?
 
Njoo nikuuzie tofali bora na imara kwa bei sawa na bure.
 
Umasikini wako....tu
Tofali zetu hazichachi
Endelea kupanga....kujenga wewe bado
Au ndo unajifunza...
Oook Samahani kumbe una migholofa

Karibu tena...
Tofali za kuchoma zipo tshs 30 moja
Hapa Msata
 
ukienda kununua kitu chochote unabidi....utende haki usipende umuumize muuzaji au muuzaji akuumize wewe nyie wapenda kitonga mnazingua maana ukiona sahv vyuma vilivyokaza then mtu bado anakukomalia basi ujue iyo pesa yako aimlipim
 
Umewahi kuzalisha Tofali ndugu? Na bei ya mbagala na mbezi hazilingani na ukiona bei njoo tukuuzie Mashine za Tofali utengeneze zako
IPO Mashine ya laki tano
 
Kwa hiyo wewe mkuu unawapangia watu bei kuwa wauze unavyotaka wewe sio
Nilikuwa na bajeti ya 2.7mil nikitaka tofari si chini ya 3,000. Sikutegemea ningekosa ndo maana nikatafuta mwenye chini ya hapo na sababu hasa inayowafanya wakomae na bei ili hali wakilia vyuma vimekaza
 
Siyo biashara tena kama mnunuzi ndiyo anapanga bei.
Bei si maelewano? Mimi mfanyabiashara pia! Kuna wakati naclear store kwa bei ya kutupa ili nipate nafasi ya kuweka vitu vinavyoenda kwa spidi kwenye soko. Sasa wewe unakomaa na matofari yako wakati eneo hilohilo wako watu zaidi ya 100 wanafanyabiashara hiyo hiyo? Uone probability ya kuuza inashuka? Pia ujue tofari zikikaa muda mrefu hupoteza uimara. Nawasahihusha wanaosema zikikaa muda mrefu ndo zinakuwa imara. Tofari zina muda maalumu wa kukaa baadaye zikianza kuota fungus zinamengenyuka
 
 
Wana uhakika wa kuuza pia haziozi,Tatu sio zinadoda ufyatuliwa kila siku,
 
Umasikini wako....tu
Tofali zetu hazichachi
Endelea kupanga....kujenga wewe bado
Au ndo unajifunza...
Oook Samahani kumbe una migholofa

Karibu tena...
Tofali za kuchoma zipo tshs 30 moja
Hapa Msata
Hio bei ya SHAMBA ujaweka usafir
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…