Wauzaji wa matofali badilikeni

Mkuu umesomeka lakini sio kila kitu lazima ufanye wewe.
Mbona unakuwa selfish kiasi hicho.. hapo mbona hujaweka risk ya kuibiwa na mafundi. Umeme wa hizo machine na ujue site nyingi zinakuwa hazija unganishwa na Tanesco. Mkuu jifunze kutawanya majukum
 
Nimepata jamaa kaniuzia faster fastet kwa 950/= hadi site! Na nyie acheni hizo!! Nilijua ningepata! Ngangania 1,200 usawa huu???
Mkuu unaweza kupata kwa hiyo bei lakini ukauziwa matofali yenye viwango hafifu.
 
Nunu cement na mchanga ufyatue mwenyewe. tatizo mnapenda kutafuniwa , kwanza utakuta tofali zenyewe ni biscut
Hapo sasa!!!!!!!!!!! Unadhai wauzaji nao wanapenda ujinga?
 
ndugu zangu naombeni kuuliza bei ya matofali (paving blocks)

1.je wanauza kwa tofali moja moja au kwa seti
2.ikiwa wanauza kwa moja moja ni kw sh ngapi na pia na kama ni kwa seti ni sh ngapi
3. Na seti moja inakaa matofali mangapi
4.Na mwisho naombeni tathmin kwa eneo la square metres 20 zinaweza kuingia paving blocks ngapi
Asanteni
 
Mara ya mwisho niliuliza ilikuwa kitofali kimoja 300-400. Square meter moja 15,000
 
Duh unalalia sana mkuu,wenyewe walishapiga hesabu hapo ndo mana wakapanga hyo bei
 
Biashara ya tofali kipindi cement ilikuwa 12000 kwa ile ya plus....Standard mfuko mmoja ni tofali 35.
Weka gharama za:-
-Maji
-Umeme
-Mashine
-Wapigaji(wachanganyaji)
-Mchanga
-Upangaji tofali.
Unit cost kwa tofali huwa minimum 780 na maximum 820. Sasa akiuza kwa bei ya Chini ya 1000 ni rahisi sana Ku breakEven au Kupata hasara kidogo. Maana hapo hatujaweka contingency kama
-Wizi wa mafundi
-Tofali kuvunjika
-Mashine huwa inazingua sometimez so matengenezo.
-Maji kukatika au kuisha sehemu unayo chukua
N.K
 

Sio uselfish ;nilikuwa najaribu kumpa elimu kama njia mbadala kwake make ameonekana analalamika kuhusu bei ya kununua; pia jua machine nyingne hazitumii umeme na zinafyatua tofali nzuri mkuu; kuhusu kuibiwa hayo ni mengineyo kama usimamizi utakuwa legevu.
 
Mkuu unaweza kupata kwa hiyo bei lakini ukauziwa matofali yenye viwango hafifu.
Hapana ni mazuri kabisa. Matofari mazuri nayafahamu! Muuzaji alisema hata angeuza 800 angepata faida. 150 ilikuwa ya usafiri kwasababu kuna umbali kama 1.5km
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…