Mradi kama huo ni vizuri wakapewa watu kutoka ulaya, namaanisha Ulaya Magharibi au USA. Project kubwa kama hizi kumpa Mchina kwa kigezo cha low cost zina madhara makubwa sana siku za usoni, Mchina kwenye project kama hizi hususani kwenye nchi kama zetu hizi hutia hasara kubwa sana ambayo ni ngumu kuiona kwa jicho la kawaida..
Kuwapa watu wa Ulaya Magharibi na USA project kama hizi inaweza kuwa na gharama kubwa kifedha lakini faida yake ni kubwa kwa mapana zaidi, uhakika zaidi wa utendaji wa mradi kwa miaka mingi, ajira zenye malipo mazuri na usalama kwa watu wetu, Watu wetu ni rahisi kujifunza teknolojia na kuwa na msaada kwa Taifa siku za usoni, Muuingiliano kwenye jamii zetu ni rahisi kwa wazungu kuliko wachina, supplier wazawa watapata kazi kirahisi kuliko kwa wachina ambao uzoefu unaonyesha wanaagiza kila kitu kutoka kwao, Uboreshaji wa mazingira husika ambapo uzoefu unaonyesha wachina hujenga mabanda ambayo hubomoka baada ya ujenzi.. Hydro-plant zote ambazo tunazo ujenzi kwa kiasi kikubwa kama sio chote ulifanywa na makampuni kutoka ulaya..
Kwenye ujenzi wa barabara kwa kiasi kikubwa tumejionea kazi chafu kutoka kwa Wachina kuliko kazi ambazo zimefanywa na makampuni kutoka Ulaya kama BAM, SOGEA SATOM, na Green Accre LTA. Pia uzoefu kwenye ujenzi wa barabara nyingi zilizojengwa awamu ya pili na ya kwanza umeonyesha ugumu wa hizi barabara ambazo nyingine mpaka leo zinadunda ukifananisha na zile za awamu ya tatu na nne ambazo kwa kiasi kikubwa zimetekelezwa na mchina kwa kigezo cha Unafuu..
Tutoe mawazo mbadala kulikomboa Taifa letu...