big up sana mkuu wa boma kwa huu uwekezaji! hii ni hatua kubwa sana katika kuelekea uchumi wa viwanda! Roma haikujengwa kwa siku moja! hii nchi ilioza mno na wachache waliishi kama malaika kwa jasho na damu za wenzao , nchi ya kijamaa ilijaa matabaka ( "wajua mi nani" kibao! maofisa wa serikali wengine wanaua raia ( Dito) , huyu mkuu wa boma wa sasa ni jiwe , namuunga mikono na miguu! ni wakati sasa tuishi kwenye uchumi halisi sio kuwa na "mawe" ya kuiba! matajiri watajirike kihalali si kupiga dili tu na kukwepa kodi! big up sana mkubwa wa boma, namshauri aweke pamba masikioni, akaze nati maradufu, vyuma vikaze for the rest of his reign, mimi nina shahada ya pili ya maendeleo, anachofanya mkuu wa boma is 100% right, yuko katika right passage ila wengi wetu ni mabishoo na tuko nje ya mstari ndo maana mayowe na kizunguzungu tupu! kimsingi anapaswa akaze nati bila kuachia kwa miaka kumi hadi kila bishoo na na kila bitoz nyangema alime hata bustani na akatwe kodi hata kama anaingiza buku alipe kodi mia mbili, akikaza bila kuachia hapo ndo atawin, akiachia japo kidogo tu katikati tumekwisha, tutarudi nyuma miaka alfu lela ulela! ( miaka 1001)! uchumi gani nchi ilijaa madalali, wavivu wanaoshinda vijiweni kazi kuomba omba wavuja jasho wenzao, vijana nguvu kazi ya nchi kazi kuimba bongofleva na kuetki muvi badala ya kuingia mashimoni mererani kupiga nyundo miamba, wasichana kazi kujiremba na kujiuza mitandaoni badala ya kufanya kazi hata saluni , ujangili ndio ilikuwa maisha yetu, tembo hawana raha ya maisha! twiga , simba na zebra wanakimbizwa tu na kukamatwa wanatiwa kwenye ndege Kia hao dubai na malaysia (kuna jamaa mmoja msouth afrika leo kasema ameona wanyama wa bongo kwenye Zoo huko malaysia wanaonekana "wanyonge sana" sababu hawako pori lao la Serengeti!), ujambazi ndo kazi, ufisadi , rushwa na wizi ndo ulikuwa utamaduni wa mtanzania, hii nchi ingehitaji millenium kupiga hatua moja! mimi namshauri kitaalamu, nimesoma kuhusu maendeleo ya nchi , ili nchi iendelee huanza na vitu viwili tu, umeme na reli, mengine huja yenyewe! mkuu wa boma pesa ya nchi awekeze kwa kujenga reli za umeme kuunganisha nchi nzima na atengeneze vyanzo vingi kama hivi vya ndani vya umeme ikibidi akope Japan waje wajenge kinu cha nyuklia cha kutoa umeme (uranium) imejaa tele Mtwara, umeme uwe cheap na ujae nchini maradufu, viwanda vyake vitashuka venyewe kama uyoga! ninaishi nchi iliyoendelea miaka kibao tu sasa, ninayosema nayaona nikitoka uani tu! mkuu wetu namuomba tu asiongeze muda wake, miaka kumi si mchezo , miaka kumi inatosha, sote tutakuwa tumeshanyooka!