Wazabuni 66 wajitokeza mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge

Marry Ngowi kwanza nakupa hongera maana nimekuona mtu kutoka kaskazini kama jina la mwisho linavyojieleza kumuunga mkono na miguu mheshimiwa rais.
 
LNG haijatelekezwa. Zinahitajika 30bil USD kuweza kujenga kiwanda. Wawekezaji lazima wajihakikishie wanawekeza sehemu ambapo hela zao zitarudi. Engineering ya kutoa na kuchataka gas yetu itakuwa complex maana gesi imepatikana kwenye visima tofauti tofauti na viko mbali mbali.
Kwa kiwango hicho cha pesa tunatakiwa tutulie maana kilio chake kama tukikosea cha madini mtoto
 
Hiyo imekula kwako, msipokuwa positive ili mpate nafasi ya kumshauri, kulima lia hakutakwisha
Watu wanafikiri wanamkoa mtu kwa kuwa negative. Kusema kweli wanajikomoa wenyewe
 
Baba, sio kila kitu unajua.. gharama za huo mradi ni kubwa ukilinganisha na kuweka mitambo ya gesi, lakini weshafanya study na wanajua kabisa huo mradi ni reliable na cheap in long run.. kwanza jiulize umeshawahi kuona mto Rufiji umekauka??

Tatizo lenu ni kutopenda kujisumbua kufanya investigation ata kidogo kujiridhisha kile mnachotetea kwa facts na mara nyingi ni watu wa sentiments kwenye hoja badala ya economical facts.


I doubt kama unachosema kina ukweli wowote you do know there are scores of credible sources ranging from international institutions which provide leadership on global energy policies such as IEA to nations own energy policies. All of which offer perspectives on viable economical investment in the sector with highlights the cost benefit of these type of investment na hakuna ata moja utakayokuta inasema hydro power; is reliable, cheapest nor profitable in the long terms based on ‘Levelized Cost of Energy’ (LCOE) calculations.


Manufaa pekee ya Hydro power ni kuwa environmental friendly; ndio maana nchi nyingi duniani makaa ya mawee ndio njia kuu, ikifuatiwa na gesi; na sisi hizo carbon fuel tunazo kwa sasa zimezagaa tu kwa mujibu wa Energy Policy yetu ya mwaka 1992 Coal, solar and wind account for less than 1% of energy used. And this is probably the case today na katika nchi zilizoendelea makaa ya mawe mpaka leo bado yanachukua between 50%-75% that is despite billions of investment in renewable energy. Sasa wewe unadhani hawana mito au source za maji ya kuzalisha huo umeme; kuna mjadala mpana sana wa kiuchumi ndio maana mtu kama Trump anataka kuitoa nchi katika Paris agreement.


Tatizo la msingi la hydro power remain the same na ata Energy Policy ya mwaka 2015 imeliongelea tena this is the global concern as mentioned “Hydro: Despite huge potentials of 4.7GW, only 12 percent of this resource has been utilised. Challenges in developing hydro systems include vulnerability to hydrology and climate change; capital intensive; relocation and resettlement of affected persons; long lead time; inadequate hydrological data; and conflicting and competing land and water uses between various sub-sectors of the economy”


Sasa anatokea tu mtu ambae ajali concerns za wataalamu wala hakuna economic viability ya kutetea hydro power tunajenga tu; sitaki ata kuongelea huo upuuzi niliokutana nao humo kwenye 2015 energy policy yetu tena imeandikwa na Professor Muhongo. My god this country is a mess kama mtaalamu tuliekuwa tuna mtegemea anaandika plan simple vile hakuna ata targeted quotas wala means of funding of those projects aisee.
 
Wakija huku mi nawatandika risasi za kwenye nyonga na miguuni..wakatibiwe nairobi
Are you proud mkuu and you want to tel the world that you did that?!. You are not in kisiwa you will not be allowed to land in any good country you dream off
 


Mkuu, nafasi ya uwaziri wa nishati na madini inakufaa sana.


Kama washamba na malimbukeni wa madaraka ndio waotuendesha maendeleo katika sekta ya nishati itakuwa ni ndoto.
 
Kuna kampuni kongwe inaitwa CMC kutoka Italy.

Ndo waliojenga Kidatu... Wamejenga power plant China majuzi kati.
Wanatakiwa wapewe kama Kweli tunataka kitu cha uhakika.
 
Umeeleza vzur mie kura yangu ni Brazil.

Na napata hisia kampuni ya Brazil itashinda tenda kwanza kabisa wana experience nzur ya ujenz wa mabwawa makubwa na katika suala zima la mazingira kwa ujumla wake.

Pili, tofaut na mabeberu wengine like USA ambao wanatukodishia mitambo ya gharama kubwa ili hali sie tuendelew kukosa umeme na wao waendelee kutuuzia kwa gharama kubwa huenda wakafanya sabotage katka ku deliver project under expectations na tusiwafanye kitu.

Kwa hisia hizi naona brazil ambao hatuna "figisu" nao naona watashinda huu mradi na sio hvo tu ndege nyingne kama ipo itakayonunuliwa basi itakua brazil Embraer ni hisia tu.
 
Umeme wa gharama nafuu za uzalishaji ni hydro nenda popote
 
Upo sahihi hata solar ni cheapest
 
Umeme wa gharama nafuu za uzalishaji ni hydro nenda popote
Pitia kwanza elements of energy policies uone zinavyo influence decision, gharama za investment, reliability, return etc. Ndio utaona kwanini coal remains the leading contender followed by gas.
 
Pitia kwanza elements of energy policies, gharama za investment, reliability, return etc. Ndio utaona kwanini coal remains the leading contender follwed by gas.
Upo sahh mkuu ila coal not renewable ikiisha imeisha ingawa haitaisha kesho na coal ni affordable ingawa kimazingira makaa ya mawe ni hatar zaid ingawa hata maji ni hatar iwapo itatokea bwawa kubomoka.

Uzur wa hydro ni kwamba ina life time ndefu ingawa pia investment yake c ndogo.

Ila kwa nchi kama yetu ambayo hayo yote yapo na tunahtaj umeme haraka then hydro is the best to start with kabla ya zote hzo

America ndo mtumiaj mzur wa coal ila anazalisha 22% ya umeme wake kutoka kwenye makaa ya mawe pamoja na kwamba kimazngira anakua challenged had juz ameamua kujtoa kwenye ule mkataba wa mazingira, wakanada wao like 57% ya umeme wao ni hydro

So both ways are good we need to utilise them all
 
Kwenye mradi wa ujenzi consultant (msahuri wa mradi) ni muhimu sana.Unaweza kuwapa hao uliowataja lakini kama consultanta ni mlegevu mradi utaoza tu.
Kwa hiyo hata akipewa mchina,lakini kama akiteuliwa consultant makini na mahiri mradi utafanikiwa tu,kwani huko kwao si ndio wameijenga nchi yao na kuwa nzuri kuzidi nchi zingine za ulaya?
 

Tayari wachina hawa hawa wameshajenga barabara tofauti tofauti hapa Tanzania lakini kila mtu ameona namna kazi zao zilivyo chafu na Wazungu hawa hawa kupitia consultant hawahawa wamejenga barabara kadhaa na tumeona namna kazi zao zilivyo nzuri.. Ubora wa kazi huangalia ni namna gani hautaharibu jina la kampuni yako kwa kazi nzuri na sio kuangalia Consultant, kwa maana Consultant akiwa dhaifu wewe ndio ufanye kazi chafu bila kuangalia heshima ya kampuni yako?

Kuna kampuni ya kichina inaitwa SINOMA, hawa ni maspecilist wa Cement industry na ndio wamejenga kiwanda cha DANGOTE MTWARA na kufanya Extension za baadhi ya viwanda vingine vya Cement Tanzania kama Tanga na Mbeya Cement, Mkuu nenda kafanye research kwenye hivyo viwanda ujionee utumbo walioufanya, kuna kiwanda kimoja cha Cement kina plant iliyojengwa na Mzungu toka 1970 huko lakini mpaka leo kinadunda na ndio plant wanayoitegemea na nyingine ni mpya imejengwa 2016-2017 na mchina nenda kawaulize balaa wanalolipata... Dangote mpaka sasa anastruggle na kile kiwanda cha mtwara, breakdowns kila kukicha..

Mchina akiwa china lazima afanye vizuri maana tayari kuna sheria inawaadhibu wakifanya utumbu na tena ni adhabu kali mno, Mchina akienda ulaya anafanya vizuri maana kule akifanya vibaya atarudia huo mradi kwa gharama zake na akifanya masihara hiyo kampuni itafungiwa milele, pili ulaya tayari wanauzoefu wa hivi vitu kwa kuvijua physically na sio makaratasi hivyo ukianza kuvuruga tayari wanajua na si ajabu michoro na design ni vya kwao ila kwa mchina wanafuata cheap labour na low production cost..
 

Wabrazil sio wabaya, technological wabrazil ni wazuri na wanafanya kazi standard na pia wanaishi karne ya 21.
Ni vizuri nao wakawekwa kwenye mzani na wazungu wa ulaya na USA..
 
Ukweli kaka, watu wanafikiri miradi kama hii ni kama kujenga choo au barabara, hii miradi ni risk sana na inahitaji umakini mkubwa kuianzisha. Kuna sheria za Tanzania kama ile ya local content ambayo inataka wataalamu wa kiTanzania wawepo katika uendeshaji wa hii miradi, ina maana inabidi uwapeleke shule kwanza wawe na ujuzi halafu wakusanye experience ili waaminiwe katika uendeshaji, hili sio jambo la kutimiza ndani ya miaka 2 au 3 bali ni zaidi ya mitano.

Sasa ukiwa na haraka ili ikamilike utasikia watu wanalalamika mbona hamna waTanzania kwenye huo mradi? Vilevile uwekezaji wa 30B USD unategemea sana hali ya soko la dunia, maana thamani ya gesi yetu inategemea sana na mahitaji ya soko, hapa karibuni bei ya bidhaa za petroli ilishuka sana na hivyo ikabidi wawekezaji waende taratibu.

Tusijisahau, sio kila kitu jinsi unavyokiona ndio jinsi kilivyo, watu wanajiropokea tu huku hawajui chochote..
 
Kuijenga hiyo dam sio kwamba ndio itakuwa tegemeo kubwa, ndio maana sasa hivi serikali inawekeza kwenye Geothermal energy.

Kikubwa ambacho serikali inalenga ni energy diversification, tusitegemee sana gas wala maji bali tuwe na vyanzo vingi ambavyo tutakuwa na uwezo wa ku switch kutokana na mahitaji, bei na dharura, hata gesi ina shida zake, kama unakumbuka kuna kipindi mitambo ya Songas ilifungwa ili isafishwe na ikapelekea ukosefu wa umeme sehemu kubwa ya nchi, hiyo ilidhihirisha kuwa sio jambo jema kutegemea vyanzo vichache vya nishati hata kama vinatosheleza mahitaji.
 
Mimi ni Tomaso wa kwenye bibilia. Wala sio ufipa wala sio Lumumba. Wala mabasha.. Simo kwenye lingi za bongo. Naangalia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…