Wazaliwa wa mkoa wa Tanga tukutane hapa

Wazaliwa wa mkoa wa Tanga tukutane hapa

0ab45068cf518bb76cf89c60ac5ea521.jpg
watanga katika suala hili tupo spesho
Spesho
 
Sasa tuzungumze la maana hapa.

Tanga ni mkoa unaoweza kujijenga vizuri sana kiviwanda. Ipo katika uwezo wetu wana Tanga na Watanzania wengineo kuzitumia fursa zilizopo mkoani hapa kujikwamua kiuchumi. Aghalab sio uvivu bali ni kukosa muongozo wa kibiashara tufanye nini.

Nitatoa mifano ya fursa za kibiashara na viwanda zilizopo Tanga. Nikitambo kidogo tangu niwe nyumbani kwa hiyo mifano mingine inaweza kuwa tayari inafanyiwa kazi. Kama ni hivyo nijuze. Pia unakaribishwa kuongeza mifano mingine unayodhani inaweza kutusaidia kibiashara au kiviwanda.

Mifano:
1. Kusindika samaki karibu na bahari.
2. Kusindika nazi (tui la makopo) pamoja na bidhaa nyingine za minazi, kama vile pombe ya mnazi ndani ya kopo.
3. Kusindika matunda (maembe, machungwa, matufaa, n.k.), kutengeneza pombe ya matunda kama hard-cider kutokana na matufaa.
4. Kusindika mboga (kukausha-wanafanya hii sasa, kutia kwenye makopo, n.k).
5. Kutengeneza bidhaa za maziwa kama cheese, shikirimu, n.k.
6. Kutengeneza pombe kali (spirits) kutokana na mkonge (Taquila), kutokana na mnazi (distillery ya pombe ya mnazi), kutokana na pombe ya muwa (boha), kutokana na pombe ya mapumba ya mahindi (kangara).

Nimejaribu kutoa mifano ya kibiashara tunayoweza kiijengea viwanda nayo. Tunashindwa na nini ndugu zangu? Ama kweli penye miti hapana wajenzi. Tuibadilishe hii dhana jamani.

Pengine baadae tunaweza kuweka vichwa chini na kutengeneza Business Plans za baadhi ya hizi fursa.

WAKAYA TEVANA?
mji umedorora mno kiuchumi, licha yakua navitu vyote ulivyoongelea apo lakin bado kwakias kikubwa vimekua sio tija latika kusogeza uchumi wawakazi.
nahisi tatizo lipo kwenye mindset zetu naelimu hafifu juu yajinsi gani tunaweza kutumia rasilimali zilizopo kujinufaisha
 
Back
Top Bottom