Wazamani (wahenga) tukutane hapa

Wazamani (wahenga) tukutane hapa

Khantwe ndoa ni zaidi ya kusema "I do" au "huyu ni Mke/Mume wangu" ndoa ni maisha baada ya kuoana. Ndiyo maana kufumaniwa ni kosa linalostahili mtu kushitakiwa. Mnaweza kwa nje kuwa kama Mume na Mke lakini kwa ndani huo mfumo haupo.
 
Hahahaha, na samaki
Posta yote bandarini imejaa meli mbovu tu

au enzi za Kununua kadi tahfif na ice cream pale snow cream
Utoto raha, tulikuwa tunaiba majaladio pale Tahfif walikuwa wanayaweka kama kwenye ndoo hivi mlangoni.

Zile meli ilikuwa kabla biasha ya Scrap haijaanza.

Pia tukitoka shule tunaenda kunywa maji Hotel ya Salamander. Wakati mwingine tukipata bahati tunapewa juice wakati mwingine ndio hivyo.

Mabasi tulikuwa tunapanda Shela Beach, Kaka Trans kwa njia ya Ubungo Posta, Chai Maharage zilikuwa Mwenge - Stesheni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulikiwa tunatoka Sinza hadi Mikocheni kwa baiskeli, tunazungumka Beach yote. Wazazi walikuwa wanachukulia poa.

Ila cha kushangaza siku hizi mwanangu haruhusiwi hata kwenda mtaa wa pili kucheza.
Mountain bikes, kuna zile tukaita dilela nadhani, walinzi ndio walikua na phonex ,Shanghai
Halafu zamani baiskeli tulikua tunaendesha sana tu watoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijuj kama unafahamu hii maana ya neno Daladala.

Dala ilikuwa ni shs 5. Sasa Nauli ya maeneo mengi ilikuwa ni shs 5, kama ilivyo shs 400 siku hizi.

Wapiga debe walikuwa wanasema nauli dala dala. Ndio jina lilipopata umaarufu.


Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante muhenga..shikamoo
 
Sana. Nakumbuka Manzese yote, Mburahati, Mabibo, Sinza, Tandale, na magomeni yote vituo vya polisi vilikuwa viwili tu. Urafiki na Magomeni. Kote huko wananchi walikuwa wanajilinda wenyewe na kuendesha maisha yao kwa jinsi wanavyoona!!
Sinza tulikuwa tunatumia Mabatini ni cha zamani pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini kila mmoja wetu anachukua tahadhari kujikinga na COVID 19.

Je, mhenga mwenzangu unakumbuka dMt, Co cabs, MORETCO, TADECO, CORETCO?

Je, unakumbuka magazeti gani ya zamani, ambayo ukiwa nje ya mikoani gazeti la leo unalisoma baada ya siku mbili?

Je unakumbuka majumba ya sinema na picha zake zilizohit?

Je unakumbuka kumbi gani za starehe zilizokuwa zinawaka moto weekend?

Je unakumbuka Taarifa ya Habari ya saa mbili usiku ilivokuwa muhimu kwa watu aidha kutumbuliwa au kuteuliwa?

Je unakumbuka jinsi vijana walivyokuwa mashujaa wanavyozamia meli kwenda nje?

Wadada wa zamani mnakumbuka mlivyokuwa mnachoma nywele ili kukonga nyoyo za wanaume?

Hebu tukumbushane, ya kale ni dhahabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
4BA814DA-A39C-4512-A098-81583C0738B2.jpeg

Hizo za tundu ndio sikuziona.
 
Back
Top Bottom