Wazanzibari bado wanataka OIC, Watanganyika tubariki tuyaone maendeleo

Kweli kabisa 🙌
 
Muungano uvunjwe haraka
 
Wazo sio baya, ila limetolewa katika maudhui ya kidini sana ambayo ni mabaya kuliko hata shutuma wanazokabili wasanii kama Nay wa Mitego. Lugha kama hii huleta machafuko katika nchi.

Na hivi kwa nini waislamu mara zote wanaona uwepo wa raisi muislamu Tanzania ni fursa kwao dhidi ya wakristo?
 
Hapana, hapa tunaongelea uhusiano. Halafu kujiunga na OIC kwa lengo la kupata misaada sio akili nzuri, ni kujifanya omba omba. Tunataka tuwe donor country!😀
Unadhani akina Nchimbi, Bashe na Rostam Aziz walienda Vatican kuzurura? 😂😂😂
 
Kwa nini Zanzibar ilijiunga kimyakimya mwaka 1993 kisha ikajiondoa kwa nguvu ya Bunge?
 
Changamoto ni kwa Watanganyika ambao hawataki muungano huu uvunjike lakini Wazanzibari wako tayari kuvunja muungano.

Wacha tuendelee kupigwa mpaka akili itukae sawa!
 
Kwa nini Zanzibar ilijiunga kimyakimya mwaka 1993 kisha ikajiondoa kwa nguvu ya Bunge?
Katiba ni ngumu sana kwa walio wengi, kwa vile Zanzibar ina uhuru wa mambo yake ya ndani yasiyo ya muungano, hivyo wakadhani wanaweza kujiunga tuu, hivyo wakajiunga.

Kumbe Zanzibar sio nchi, OIC ni ya nchi. Ilipofika Bungeni wabunge wakachamaa ikalazimishwa kujitoa kwa ahadi ya Tanzania kujiunga.
Kitendo hicho ni kuionea Zanzibar kama tunavyowaonea Waislamu kuwanyima mahakama ya kadhi.

Zanzibar waachwe wajiunge OIC.
Mwisho unapomkosea mtu kwa kumtukana bila kosa lolote, akikuuliza kwanini umemtukana, usikae kimya as if you did nothing wrong!, jifunze kusema sorry!.

P
 
Wapewe kura ya maoni kuwauliza kama wanautaka Muungano au hawautaki.

Huo ndio mzizi wa fitina hizi nyingine ni mazungumzo baada ya habari tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…