Tetesi: Wazanzibari wengi wanautweza Utanzania, shida ipo wapi?

Tetesi: Wazanzibari wengi wanautweza Utanzania, shida ipo wapi?

Ni nadra sana kumkuta Mtanzania wa visiwa vya Zanzibar akijitambulisha kwamba yeye ni Mtanzania.

Nimefanya utafiti wangu usio rasmi kuhusu hili suala. Ukimkuta Mzanzibari nje ya nchi, halafu ukamuuliza ikiwa yeye ni mtanzania, mara nyingi utapokea jibu kwamba 'Mimi ni Mzanzibari'.

Yaani ni kwamba wazanzibari wengi huwa wanajaribu kwa namna yeyote, kuukwepa utanzania na wengi hawapendi kuitwa watanzania. Kwa waliotembea uarabuni mtathibitisha hili. Yaani ukitaka ukosane na mzanzibari huko arabuni, basi we muite mtanzania.

Inaonekana ni kama wazanzibari wanahisi tayari wapo daraja fulani hivi la juu, hivo kitu utanzania ni kuwashusha hadhi.

Hili jambo ni moja ya mambo ambayo nahisi yanahitaji uwepo wa serikali tatu, maana huko tunapoenda, itafika mahali hata sisi wa bara tutatamani kuitwa watanganyika.

Mi binafsi naanza kuchukia jina Tanzania. Maana yake sioni faida ya huu muungano ambao, kuna upande unautweza wazi wazi.
Zanzibar ni nchi feki. Hawana jeshi ni maneno tu.
 
Ha ha haaa...
Naona unafunika kichwa kwenye mchanga ukijifariji kila kitu kipo sawa kama udhaniavyo.

Zanzibar haijawahi kuwa koloni la Oman Sultanate?
Hujui maana ya koloni kumbe. Jee Hawaii leo ni koloni la Marekani?
 
We are talking about Zanzibar and not other similar states not Hawaii.
Tunaongelea Zanzibar na wewe ukatoa mfano wa visiwa vya UK na France. Kwa nini na mimi nisitoe mfano wa visiwa vya Hawaii?
 
Back
Top Bottom