Ninachokiona hapa kila anayechangia anatoa maoni ya alichosoma au alichoambiwa kuhusu Zanzibar.
Kabla ya kutukanana hebu mjiulize hivi Visiwa vipo tangu lini?. Je historia ya kuwa ilikuwa ni sehemu ya Bara iliyomeguka ni sahihi?.
Ni ajabu kuona mmoja anaamua kumtolea Mwenzake matusi huku akimpinga...sasa si uje na taarifa uliyonayo wewe Watu tuisome kama yeye alivyoileta hakuna ulazima wa kutukana.
Mtu unapohoji kama Visiwa vilikutwa bila Watu, sasa kwani hilo haliwezekani?. ni huenda walitoka mbali sana au walitoka maeneo ya jirani..siku zote lazima wapo waliofika hapo kwanza na walikuta Kisiwa kikiwa tupu au kina Viumbe/Wanyama n.k...vipi pia kama kulikuwa na mapambano ya umiliki na hakuna maandiko wala simulizi?.
Na vipi kuhusu Kisiwa cha Mafia?.
Hofu yangu ni kuwa tunabisha tu kwa tusilolifahamu kwa usahihi.