Wazazi acheni kulaumu wake zetu, Sisi hatuna Pesa za kuwapa wala hatujalogwa

Wazazi acheni kulaumu wake zetu, Sisi hatuna Pesa za kuwapa wala hatujalogwa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Assalamu alyekum!

Sina maneno mengi leo si mnajua ni weekend. Nijikite kwenye mada.

Wazazi nataka kuwaambia kuwa mnawaonea wake zetu(ambao mi wakamwana wenu) Kwa kuwatuhumu wametuloga, wametufumbata, wametuweka kiganjani Kama online business kisa tunashindwa kuwahudumia na kuwatumia pesa huko vijijini.

Najua mnamjua kijana wenu Taikon ni msema kweli na wala hajawahi kuficha kitu, siku zote nimekuwa nikisema mambo bayana.

Watoto wenu huku mjini hatujalogwa wala nini. Acheni kuwasimanga na kuwawekea vinyongo msongo Wakamwana wenu. Kuwaandama tadhani mwezi mwandamo wa mfungo unavyokodolewa macho Kodi.

Wazazi wetu huku mjini mambo Bora yangekuwa bilabila tungeshukuru lakini mpaka sasa Jiji linatuendesha vilivyo likiwa mbele Kwa bao 4 Sisi tukiwa nyuma Kwa 0(4-0) mabao matatu tukiyarithi kutoka kwenu, Sisi tukiwa tumefungwa moja hapa na kukamilisha idadi tajwa hapo.

Ball possession tunaongozwa Wazazi wetu.

Kusema tumekuja mjini tukajisahau sio kweli,
Wengi wetu tunapambana kufa na kupona huku tukizingatia Yale maadili mliyotuachia tusiibe cha mtu.

Huku kila kitu ni pesa.

Shikamoo ni pesa
Kuelekezwa ni pesa
Maji ni pesa
Kodi ni pesa
Chakula ni pesa.
Kuachia mambo na vijambo ni Pesa kwani huwezi kujamba pasipo pesa ya Kula.
Huku vijambo hukusanywa na manispaa ya jiji Kwa magari maalumu ya taka.
Hakuna kuchimba shimo la taka.

Wazazi lawama zenu hazitasaidia Jambo lolote.
Shutuma zenu hazisaidii lolote.

Kwani hamjui huku mjini hatuna kazi ya maana zaidi ya kubangaiza?
Kwani hamjui huku mjini tunakimbizana Kama wendawazimu kuzitafuta pesa na bado tunakosa? Hamjui nauliza!!

Au mnafikiri watoto wenu wote tuliomjini tunafanya kazi kwenye viyoyozi? Ndivyo mnavyodhani mmechelewa kujua.
Huku mjini tunatembea huku na huko tukiuza Laini za simu, tukiwaambia tunafanya kazi kwenye MAKAMPUNI ya simu mlidhani ni ofisini 😀😀. Ni kutembeza sako Kwa bako, kiguu na njia huku jua likituadhibu kichwani.

Huku tunauza Ice Cream za Bakhresa kwenye mabarabara tukiziweka roho zetu rehani Kwa kukukoswa koswa na bodaboda wasumbufu na madereva WA magari wasiojali sheria za barabara.

Huku mjini tunauza barakoa kwenye malango ya hospital na maofisi makubwa tukiwashawishi watu Corona inaua😊😊 huku nafsini mwetu tukiona ni uongo😀😀.

Wazazi wetu huku mjini ukiona kijana kashika kalamu na karatasi usije ukadhani ni mwanachuo, huyo ni afisa wa kubeti, kazi yake ni kubeti na ndio anaendesha maisha yake hivyo.

Huku mjini wazazi wetu Sisi tulishaonja joto la jiwe na kuijua ladha yake. Tumefukuzwa kwenye masoko kwani tuliwadanganya Sisi ni wafanyabiashara ilhali ukweli ni kuwa tulikuwa Machinga. Tumefukuzwa sehemu zenye wateja tuliowafuata wenyewe tumeelekezwa Maeneo yasiyo na wateja. Hivyo msishangae tukishindwa raundi hii kuwatumia hata hizo Mia mbili.

Hivi mnavyosema Wakamwana wenu wametuloga ndio maana hatuwatumii pesa, mnadhani tuna hizo pesa basi. Sisi huku mjini ni wazugaji tuu.
Kurudi kijijini hatutaki na kuhama mjini hatuhami.

Mbona hao ambao hawajaoa nao hawatumii pesa Kama tatizo ni kuoa. Wake zetu sio shida wazazi wetu. Shida ni pesa huku mjini ni kipengele.

Nasikia kuna mswada umepelekwa Bungeni kuhusu Kuruhusu Watu kuuza Figo zao Kwa hiyari Yao wenyewe. Vijana wengi huku mjini wanasubiri Kwa hamu na nidhamu mswada huo upitishwe ili tuweze kuuza Gigi zetu ili tupate pesa tusuuze roho zenu.
Na wala msije sema tusiuze wakati kutwa kuchwa mnatusimanga Kwa Ngoma za sapanka.

Hao Wake zetu wanatupunguzia uzia na kutupa Raha za dunia licha ya ukabwela wetu. Tunakula uroda bila kupimiwa ndio maana kila siku Asubuhi tunaamka tukiwa na nguvu mpya ingawaje matokeo tupatayo niyazamani.

Kila siku kuwasifia Dada Safina na Mwari Daina kuwa wao ndio wanawajali walau Kwa kuwatumia pesa.

Mlitaka tuwe wanawake Kama wao ili tuuze miili yetu Kama wao wafanyavyo? Sikutaka kusema haya lakini Masimango yenu yamevuka maji ya shingo,

Hamjui huku mjini binti zenu wanauza sebule na Uani? Ninyi mnadanganywa na televisheni za superwoman wakati ukweli ni mchungu.

Mtoto hakusoma, mume wake ni Taikon wa Fasihi ambaye kazi yake ni Beting alafu anakutumia laki moja nawe mzazi Kwa vile ni kichwa nazi maji ya madafu unamuona wa maana!! Anyway Mimi siwachagulii maisha.


Ninachotaka kusema acheni tabia yenu mbaya ya Kuwashutumu wake zetu kuwa wanatuloga tusiwatumie pesa wakati Sisi hatuna hizo pesa ambazo zinatutosha na wake zetu.

Najua mtakereka😊😊
Najua mtakwazika, na nafahamu mmoja wenu Kwa vile ni mwepesi WA hasira atajifanya kunipa Laana😀😀.
Tuliza ball, maisha yenyewe tuliyo nayo mjini ni laana tosha. Hiyo nyingine utakayotupa ni kutuumiza tuu.

Nakala moja Kwa
1. Mama
2. Baba
3. Mjomba Nchumali
4. Shangazi Kaja
5. Mama Mkwe

Ndukiii!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Ubungo
 
Akili za wazazi wa kibongo kipindi wako wana nguvu za kufanya kazi haswa wanaume wanakuwa na wanalelea ndugu zao bila kujiwekezea hapo watoto wao hawawapi matunzo bora kisa ndugu

Wakipeleka misaada mikubwa huoo kwao

Wakifika uzeeni wanawakaba watoto wao tu wala sio wale ndugu waliospend nao hakika kila mtu atakula alikopeleka mboga


Kama swala la kulea na kuwahudumia watoto ni lazima kwao hamna malipo la sivyo wasizae
 
Back
Top Bottom