Wazazi acheni uhuni na visingizio, toeni urithi kwa watoto. Elimu sio urithi!

Urithi ungekuwa ujinga hii nchi ingekuwa Yenu??

Itashangaza mtu ni msomi asielwe concept ndogo niliyoieleza, pia itashangaza Kama mtu anaumri wa zaidi ya miaka 25 asielewe mantiki ha kile kilichozungumzwa hapa.
Now mkuu tofautisha Nchi na urithi wa mali these are two different things ni impossible kufanya kuwa mfano wa kuthibitisha ulichoandika ni sahihi in anyway.

Na Nchi sio urithi sababu sio mali ya mtu mmoja bali kila mtu aliyekuwepo nchini basi na yeye ataitwa mwananchi, au unataka kusema kuna mtu mmoja ambaye ameturithisha nchi?

Na ili kukuprove wrong vizuri na mfano wako wa nchi kama kithibitisho cha mtoto kupewa urithi.
Ni hivi yoyote aliyezaliwa nchini ni mwananchi na kuwa mwananchi haaimaanishi kwamba unaimiliki nchi bali ni mshiriki tu na ndio maana unalipia kodi ya ardhi, kodi za vichwa na kodi za aina nyingine, kuna viongozi na serikali, kuna sheria na kanuni.
Na pia ukifanya Utumbo wowote basi unahukumiwa, kifo, kifungo cha maisha nk

Mpaka hapo unaona hiyo nchi ni yako au bure?
Kwanini ufanyi unachokitaka kama ni yako ambayo umerithishwa sijui na nani?

Sababu nchi haiwezi kuendelea bila ya wananchi kufanya chochote ili kuongeza chochote kwenye nchi yao.
Ni lazima ufanye kazi ulipe kodi ili zijengwe shule, hospitali, maji na huduma nyingine za kijamii ambazo zitafanya nchi iendelee na kuweza kusurvive au Nchi itakufa kwa umasikini wa kutisha.

Na kama ilivyo nchi ndivyo ilivyo familia na mali ya urithi.
ni lazima isimamiwe means ipate uongozi na watoto wafanye chochote ili kuendeleza na kukuza hizo mali za urithi ili familia ikue.
Au kila mtu akipewa na kufanya anachokitaka lazima mali ipotee na umasikini kushamiri kwenye familia.

In simple terms as possible ni kuwa mali haitakiwi kurithishwa bali inatakiwa kuendelezwa na watoto.

Ni kama zile familia tajiri ambazo baba akifa na kugawa urithi kwa watoto basi ghafla familia inageuka masikini.
Again urithi ni ujinga unaofanya familia izidi kuwa masikini hii sio opinion bali ni fact na ukweli. utakataa only kama umeamua kukaza kichwa sababu ndivyo ulivyoamua kuamini.
 
Uko sahihi Elimu inaweza isiwe Urithi.

Kwangu mimi mambo ya urithi naona ni ujinga unaofanya familia zizidi kuwa masikini hivyo hakuna kitu nakichukia kama urithi kwenye mambo ya familia...
Familia zote zenye nguvu ya kiuchumi Duniani zinarithisha mali kwa vizazi vyao.
Hii mantiki yako uliyoielezea haina mashiko pia inapingana na uhalisia.
Mfano wa familia zenye mafanikio zaidi ni hizi
The Rothschild family(bankers)
Bush family(politicians)
Sinclair(nobles)
Toyoda family (Toyota)
Lee family(Samsung)
Waltons family
Mars family
Al Saud family
Ambani family
Koch family
Hizo familia zote zimefika hapo zilipo kwa kurithishana mali, kurithi ni suala na uumbaji na muendelezo wa maisha ya binadamu na urthi pekee ulio halali ni ule mtoto kurithi kwa mzazi wake (BABA).
 
Familia zote zenye nguvu ya kiuchumi Duniani zinarithisha mali kwa vizazi vyao.
Hii mantiki yako uliyoielezea haina mashiko pia inapingana na uhalisia...
Sawa mkuu, wamerithi.

Lakini hawajarithi kwa kugawana kila mtu na chake asepe afe kivyake, sababu hivi ndivyo watanzania wengi wanafikiria wakisikia neno urithi. Na ndicho kinachofanyika mpaka leo.

Bali wamerithi kwa kuendeleza kile kilichoachwa na wazazi, wanapambana kwa nguvu zao wenyewe kuendeleza kilichoachwa na waliopita. na bila shaka waliambiwa nini cha kufanya na waliopita ili kuziendeleza au kuna vitabu kabisa na darasa la jinsi ya kukuza mali na utajiri waliorithishwa.

Na sio kwamba wamegawana tu hovyo'hovyo na kila mtu kwenda kivyake au usingesikia wala kujua kama zilikuwepo. na ndio maana mpaka leo unazisikia zinaitwa "family" hata wewe umeziita hivyo, unaona? unarudia kilekile nilichokiandika?

Sasa hiki ndicho ninachokiongelea hapa.
 
Mungu wa Isaka na Yakobo na akujaalie uyatimize maono yako. Urithi kwa vizazi vyetu ndo jambo muhimu. Na hongera kwa kuwa mmojawapo wa wachache tuliolielewa somo hili.
Ni jambo muhimu na wajibu kutoka kwa Mungu, na baraka ndipo zinapoanzia, imagine mzazi anapenda mtoto wake apate zawadi au mambo makubwa kutoka kwa watu wengine wakati yeye mwenye mtoto na wajibu wa kumpa Mali anaona wivu kumpa mtoto wake Sasa hizo bahati anazoomba zimshukie mtoto kutoka kwa watu wengine zitakujaje?
 
Sawa mkuu, wamerithi.

Lakini hawajarithi kwa kugawana kila mtu na chake asepe afe kivyake, sababu hivi ndivyo watanzania wengi wanafikiria wakisikia neno urithi.
Na ndicho kinachofanyika mpaka leo...
Sasa madingi zetu hapa bongo hawapo hivyo mkuu, ukumbuke urithi sio mali pekee bali huambatana na maarifa ya urithi husika ambavyo kwa pamoja hubeba tabia ya familia husika.

Kama alivyosema mtoa mada kwamba maarifa(elimu) sio urithi bali ni siraha/mbinu za kuendeleza urithi. Katoa mfano mtoto wa mkulima atafundishwa kilimo kisha atarithishwa shamba ili atumie maarifa yake kuendeleza maisha.

Leo hii wazee wengi wa kichaga kwa mfano wanawaambia watoto wao hakuna mali ya kurithi wakati huo huo mzee huyo anamiliki kipande cha ardhi kule Kilimanjaro alichokirithi kwa baba yake mzazi na anakitumia kwenda kupumzika kila mwisho wa mwaka.

Wazazi waache uhuni, wahakikishe wanawarithisha mali watoto wao.
 
Nihitimishe kwa kusema tu mtoto wangu lazma nimpe mali aisee! Huu msoto naopitia sio kitoto. Kama ataziharibu atauza atajua mwenyewe ila lazma nimpe njia ya kuishi bila stress[emoji23]
Huu ndio mtazamo chanya aisee, ni lazima mtoto aanzie nilipoishia mimi. Tena kwangu mm kama nisingeachiwa kaurithi sijui hata ningekuwa na hali gani mana mzee wangu alikufa nikiwa bado mdogo sina nijualo kuhusu maisha.
 


Hawatakuelewa
 
Hawatakuelewa
Huyo jamaa jamaa anakomaa na wale wanaotapanya mali baada ya kurithishwa kuwatumia kama excuse. Mtoto hajaomba ruhusa kuna duniani,anatakiwa apewe nyenzo za kuishi duniani; elimu na mali.
 
Maniga wakiona tinafuatilia urithi wanaona tunatamaa na Mali za baba
 
Ukiona kijana amepata elimu na maarifa halafu bado anaongelea mambo ya urithi maana yake amefilisika kimawazo. Kwani huyo mzazi alipata wapi hizo mali? Kizazi hiki cha Wagalatia kinasikitisha sana, ukiwepo urithi sawa hakuna shida, lakini sio wakung'ang'ania urithi mpaka wengine wamewauwa wazazi wao ili tu wapate urithi. Unaelimu unaujuzi pambana utafute chakwako nawewe uwarithishe wanao na sio kuwazia kupata urithi kwa nguvu kutoka kwa wazazi wako. Nasema Elimu na ujuzi ni Urithi kama urithi wa mali. Kwavile elimu na ujuzi ndio vinaweza kukupatia mali
 

Mtumwa anawaza Kama wewe!

Watawala, wanasiasa, wafanyabiashara Wakubwa na matajiri Wakubwa wanawaza kuacha urithi mpaka Kwa vitukuu alafu Kapuku mmoja anadhani kielimu chake sijui cha degree kitamfikisha wapiπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Elimu bila Rasilimali ni Sawa na Masai mwenye ugoro mdomoni
 
Hujitambui ndio maana unashindwa kupambanua na kuelewa hoja, unaishia kutukana. Kutukana haikusaidii chochote, sana sana inaonyesha jinsi ulivyomtupu kichwani kwako na hujakomaa. Nilidhani una busara kumbe ni zero kabisa. Na hata elimu yako inaonekana ni ya kubabaisha ndio maana hujiamini. Kutofautiana mitizamo au hoja sio sababu ya wewe kutoa matusi, kwanza huna adabu na hujui unaongea na nani, wengine hapa tumekuzidi kila kitu, hata kiumri wewe ni sawa na mtoto kwangu. Jifunze kuheshimu wakubwa. Hoja inajibiwa na hoja sio matusi kijana wewe. Uwe na adabu kwa wakubwa
 
Hili ni moja ya Bandiko lako Ambalo Sitakaa nilielewee!! Watu tupo makabila na Imani tofauti....Hivi Unafahamu kuna makabila yana utaratibu wao wa kugawa mirathi na Serikali inatambua hilo?
.Hivi Unafahamu katika Dini Kiislamu kuna Utaratibu mzima Umepangwa kuhusu mirathi,Una uhakika gani km unaendana na Huo utaratibu unaotuwekea hapa?? Jaribu kufanya tafiti kwanza kwenye Jamii tofauti Ndio ulete bandiko km Hili hapa....
 

Sasa wapi nimekutukana?

Kutofautiana Kwa watu ndio unaita matusi?
Hujui kuna wenye mtizamo wa kitumwa kwani Hilo ndilo kwako umeona Tusi?
 
Nikisema kwamba umezaliwa katika familia maskini, unawaonea wivu watoto wa matajiri wa rika lako nitakuwa nimekosea mkuu??. Vipi nikisema wewe una mali ila umezidisha uchoyo, unapenda starehe kuliko kujali watoto. Sustainablity in family wealth should be maintained over the present and future generations. One generation should get its share of wealth or income without limiting the future generations to get wealth. Sijapinga ulichokiongea ila nakushauri uukuze msimamo wako ufahamu kwamba pamoja na hayo uliyoyasema (Kama watoto kuwa komavu kwa kujua kujipambania) mali uliyonayo siyo yako peke yako bali vizazi vyote vya sasa na vya baadae.
 

Ukiona Jambo nimeandika elewa nimeshalihakiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…