Wazazi hebu njooni tuongee:- Kwani mnashida gani na mali zenu kwa watoto wenu, Mbona watoto wenu tupo nao huku mtaani wanateseka na nyie ni matajiri?

Wazazi hebu njooni tuongee:- Kwani mnashida gani na mali zenu kwa watoto wenu, Mbona watoto wenu tupo nao huku mtaani wanateseka na nyie ni matajiri?

Hii stori/uzi umenigusa moja kwa moja. Nna jamaangu naye Baba yake ni Don kweli kweli. sitaki kuelezea utajiri wa babake, just imagine kama Mama anaweza kuingia kwenye Mzozo wa Kutapeliwa na Wachina Dolla laki sita, je baba atakuwa na ukwasi kiasi gani? halafu mtoto unahaso mtaani kwenye vijiofisi uchwara na Degree yake ya IT tena umesomea Nje huko. Hi ni noma sana. Tuombe sana Mungu atupe kipato halali ili kiweze kuwanufaisha familia zetu hata ikiwezekana Majirani zetu.


Kuna rafiki yangu yeye huwa nina mwambia akishindwa kumuombea Mzee wake huko alipo/tangulia atakuwa anamkosea kwa kweli. Mzee wakati wa Uhai wake alifaiti vibaya sana. Huku na huku, akafanikiwa kuwa na Petrol station 2, sehemu ambazo ni very premier, achilia nyumba kadhaa maeneo ambayo ni vey prime areas. Kwenye nyumba tu kodi wanazokusanya toka kwa foreigners, zaweza fika $16K kwa mwezi. Uzuri Jamaa kasoma kadegree kake kamoja katulia. Jamaa yuko very peace, hashoboki na utajiri wa wazazi wake. very cool. anauwezo wa kundesha hata Vella au Cruiser ya 450M ila katulia na Forester yake ya mwaka 2009. Jamani, tufanye kazi kwa ajili ya uzao wetu.

Raisi Museveni aliwahi kuhojiwa na Waandishi wa Habari kuhusu utitiri wa Investments anazomiliki ili hali hata akistaafu leo, serikali itaendelea kumhudumia yeye na familia yake, lakini alichowajibu waandishi wa habari, wewe mwenyewe utacheka. Aliwaambia waandishi wa Habari, alaaniwe yule asiyefanya kazi. hata hivyo, yeye anafanya kazi kwa ajili ya uzao wake. kisha akawahimiza nao waandishi wa habari nao waige kwake. wafanye kazi kwa ajili ya uzao wao.


hii philosophy niliipenda, nikaibeba. natembea nayo. napiga moyo konde na mimi ipo siku uzao wangu hauta tabika, na utaendelea kunikumbuka kwa nguvu zangu kwao.
Kweli Mungu awabariki wale wote wenye vision kwa ajili ya uzao wao.
 
Back
Top Bottom