Wazazi jukumu lenu lisiwe ni kuwasomesha watoto tu, jitaidini kuwatafutia connection. Dunia imebadilika

Wazazi jukumu lenu lisiwe ni kuwasomesha watoto tu, jitaidini kuwatafutia connection. Dunia imebadilika

Konseli Mkuu Andrew

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2013
Posts
749
Reaction score
875
Salaam Wakuu.

Dunia ya sasa mambo yamebadilika tofauti na miaka ya nyuma , (nasikia) zamani ukisoma hadi level ya degree ilikuwa ni rahisi sana kupata nafasi ya kazi pasina na hata kujuana na mtu katika idara au taasisi fulani.Wazazi wa wakati huo jukumu lao lilikuwa ni moja kuwapeleka watoto shule na kuwatafutia ada tuu.

Jukumu ili la kuwasomesha watoto naona kama bado limerithishwa na wazazi wa kizazi hiki na kushindwa kuelewa kuwa elimu bila ya connection ni sawa kazi na bure huu ndio ukweli.

Nawashauri wazazi wakati mnaangaika kuwatafutia ada watoto basi msisahau kuangaika kuwatafutia connection watoto wenu pindi wanapomaliza masomo.Huko kwenye majumuiko yenu hao mnaokutana nao watumieni kama fursa kwa watoto wenu msiishie kusema "jana nilikuwa meza moja na RPC tulikunywa sana kwakweli"

ELIMU BILA CONNECTION NI SAWA NA GUNIA BILA NAFAKA
 
Najutia kwanini ni likua na mkera baba angu ahame chama cha kijani, kumbe ndo connection yenyewe huenda ange toka kwa kujifanya kwamba yataka haki na kupinga ufisadi wengi tusingekua na ajira.
 
Najutia kwanini ni likua na mkera baba angu ahame chama cha kijani, kumbe ndo connection yenyewe huenda ange toka kwa kujifanya kwamba yataka haki na kupinga ufisadi wengi tusingekua na ajira.
Hongera.uhanarakati bila pesa ni sawa kazi na bure. Hao wapinzani wakubwa nao wanawategemea wakijani kuendwsha big programs zao , niamini mimi
 
Tatizo ni kubwa zaidi ya connection unazoziimba, hata wazazi wote wakiwa na connection watu bado watakosa kazi kwasababu hizo kazi za kuwatosha wote hazipo.
 
Tatizo ni kubwa zaidi ya connection unazoziimba, hata wazazi wote wakiwa na connection watu bado watakosa kazi kwasababu hizo kazi za kuwatosha wote hazipo.
Ila inaweza saidia kwa hao wachache, neno connection lina maana pana pia, connection katika kupata mtaji huko katika halmshauri zenu au taasisi za kifedha, connection katika kupata ufadhili wa miradi mbali mbali n.k
 
Ndio maana nasemaga kulipa mamilioni ili mtoto asome English Medium ni kupoteza hela tu bure hiyo pesa bora uwajengee wanao na kuwatengenezea miundo mbinu mingine
 
Ndio maana nasemaga kulipa mamilioni ili mtoto asome English Medium ni kupoteza hela tu bure hiyo pesa bora uwajengee wanao na kuwatengenezea miundo mbinu mingine
Uwajengee nini sasa?
 
Back
Top Bottom