Wazazi mmekuwaje?

Wazazi mmekuwaje?

Habari!

Nilipomaliza chuo nilipatwa na mkasa. Ile nimemaliza tu mitihani nikamtaarifu mama, tukaongea tu vizuri kwa muda mfupi chumbani kwake, sasa wakati natoka nje akaniuliza swali 'kwahiyo ushapata mtu wa kukuoa?' moyo ulishtuka halafu chap nikaendelea na safari hapo nikajifanya sijamsikia.

Ikawa wimbo anaoupenda 'ushapata wa kukuoa? Nikawa namwambia sipo tayari kwa sasa nikimjibu hivyo anaanza kutoa risala 'unajua inabidi uolewe mimi najisikia vibaya kukuona tu hapa nyumbani'

Siku moja nikamwambia mimi sijapata hata wa kunioa, akasema 'uzuri wote huo hakuna aliyesema anataka kukuoa' ilibidi tu nicheke mimi nilikuwa nishasoma akili yake kwamba uoga wa maisha unamsumbua.

Ishapita miaka 3 tokea kisa hiki kitokea, juzi nikasema acha niwaulize wenzangu kama wanakutana na maswahibu kama yangu sababu huu wimbo mama yangu bado anauimba.

Rafiki yangu FLORA
Yeye aliniambia alivyomaliza Mitihani alichelewa kurudi nyumbani kwa miezi kadhaa, sasa kuna siku akaumwa akalazwa mama yake alivyoenda hospital akamkuta Flora yupo na boyfriend wake ila huyo bf akawapisha waongee.

Mama yake akamuuliza 'huyo kijana ni nani' Flora akamjibu ni rafiki yake.
Mama yake akamwambia bills ni kiasi gani ili alipie! Flora akamwambia 'rafiki yangu ameshalipia' mama yake akaguna.

Sasa Flora alivyorudi kwao, mama yake akaanza kuimba nyimbo kila mara 'Yule rafiki yako yuko wapi akuoe kuliko kushinda ndani kila siku' Flora akaishia tu kucheka.

Rafiki yangu REBECCA
Yeye alikuwa anabanwa sana, ni wale watoto geti kali. Alivyomaliza chuo kuna siku akamuomba mama yake ruhusa ya kwenda kumsalimia rafiki yake. Mama yake hakumuuliza maswali mengi kama alivyokua anafanya hapo awali.

Jioni mapema Rebecca aliporudi mama yake akamwambia 'Mbona umerudi mapema' akamjibu nilienda kumuona tu mara moja. Mama yake akamwambia 'Ebu tembeatembea wachumba wakuone sio kujifungia tu ndani'

Ila ameniambia huo wimbo mama yake aliuacha baada ya yeye kupata kazi.

Rafiki yangu ASHA
Huyu ndiye amenichekesha sana, anasema tulivyomaliza chuo baba yake akawa anamwambia 'fanya uolewe sitaki kukuona nyumbani kwangu'

Kuna siku akaenda kazini kwa baba yake akamkuta yupo na wanaume wengine akawasalimia.
Kijana mmoja akamwambia mzee wake kwamba hakujua kama ana binti mkubwa vile! Mzee wake akajibu 'Huyu ni binti yangu kamaliza chuo mwaka huu na bado hajaolewa' wote wakaishia kucheka.

Haikupita miezi mingi baba yake akamletea mchumba, ubani ukachomwa sasa hivi yupo kwenye ndoa.

Nilichokiona wazazi wengi ambao hawajajipata kazi wanayotupa watoto wa kike ni kuolewa tena kama mtoto hajapata kazi ya kufanya.

Ila ukiwa na kazi nzuri unapata pesa, hii risala ya kuolewa hawatoi hata ukifikisha miaka 40.

Sasa sijui wa kulaumiwa ni CCM, wazazi wetu au sisi watoto.
Such a wonderful overview ...

Labda tu nikuambie, hilo ni suala la kawaida sana na linatokea kwa karibia watu wote women/ old men with job; I have also been there na naamini baadhi ya sababu ni kama zifuatazo:

1. Kwa wanawake, muda sahihi wa kuolewa ni as soon as possible vile mnavozidi kuwa watu wazima chances get reduced so hakuna muda sahihi zaidi kwa mzazi kuanza ku break the ice kama baada ya kumaliza chuo and kuwa over 22 years old

2. Kama ilivyo kujitegemea, NDOA ni tukio la kuogofya, lenye sintofahamu nyingi sana na kwa karibia watu wote sio tendo la hiyari - means hata wazazi wako kuwa pamoja ni vile all option run out and they decided to take risk. Ndoa is a game of chance na kama sio kukamatika kimahaba na kimazingira, hakuna ambaye angeoa.

3. Kusukumwa pekee ndio kitu kinaweza kukutoa kwenye confort zote na time is the only limiting factor hivyo wazazi na ndugu sometimes based on the experience na kuona mbali wanaanza kukushtua mapema

4. Ndoa na mtu sahihi kwa mwanamke ni hazina, ushindi na mafanikio makubwa, so ni furaha kwa familia, ndugu na jamaa kuona ukivuka hicho kihunzi. Through ndoa, wazazi watapa wakwe, wajukuu, mafaniko, majukumu yatapungua kwako na pengine msaada wakati wa shida.

Mwisho:

Za kuambiwa changanya na zako, kwa umri wako may wazazi dont see any movement and thus why wanakusaidia ku create need ili labda after 5 years wavune from there investment

You have wonderful Mother, ongea naye na take it positive, she have been there - done that.
 
Habari!

Nilipomaliza chuo nilipatwa na mkasa. Ile nimemaliza tu mitihani nikamtaarifu mama, tukaongea tu vizuri kwa muda mfupi chumbani kwake, sasa wakati natoka nje akaniuliza swali 'kwahiyo ushapata mtu wa kukuoa?' moyo ulishtuka halafu chap nikaendelea na safari hapo nikajifanya sijamsikia.

Ikawa wimbo anaoupenda 'ushapata wa kukuoa? Nikawa namwambia sipo tayari kwa sasa nikimjibu hivyo anaanza kutoa risala 'unajua inabidi uolewe mimi najisikia vibaya kukuona tu hapa nyumbani'

Siku moja nikamwambia mimi sijapata hata wa kunioa, akasema 'uzuri wote huo hakuna aliyesema anataka kukuoa' ilibidi tu nicheke mimi nilikuwa nishasoma akili yake kwamba uoga wa maisha unamsumbua.

Ishapita miaka 3 tokea kisa hiki kitokea, juzi nikasema acha niwaulize wenzangu kama wanakutana na maswahibu kama yangu sababu huu wimbo mama yangu bado anauimba.

Rafiki yangu FLORA
Yeye aliniambia alivyomaliza Mitihani alichelewa kurudi nyumbani kwa miezi kadhaa, sasa kuna siku akaumwa akalazwa mama yake alivyoenda hospital akamkuta Flora yupo na boyfriend wake ila huyo bf akawapisha waongee.

Mama yake akamuuliza 'huyo kijana ni nani' Flora akamjibu ni rafiki yake.
Mama yake akamwambia bills ni kiasi gani ili alipie! Flora akamwambia 'rafiki yangu ameshalipia' mama yake akaguna.

Sasa Flora alivyorudi kwao, mama yake akaanza kuimba nyimbo kila mara 'Yule rafiki yako yuko wapi akuoe kuliko kushinda ndani kila siku' Flora akaishia tu kucheka.

Rafiki yangu REBECCA
Yeye alikuwa anabanwa sana, ni wale watoto geti kali. Alivyomaliza chuo kuna siku akamuomba mama yake ruhusa ya kwenda kumsalimia rafiki yake. Mama yake hakumuuliza maswali mengi kama alivyokua anafanya hapo awali.

Jioni mapema Rebecca aliporudi mama yake akamwambia 'Mbona umerudi mapema' akamjibu nilienda kumuona tu mara moja. Mama yake akamwambia 'Ebu tembeatembea wachumba wakuone sio kujifungia tu ndani'

Ila ameniambia huo wimbo mama yake aliuacha baada ya yeye kupata kazi.

Rafiki yangu ASHA
Huyu ndiye amenichekesha sana, anasema tulivyomaliza chuo baba yake akawa anamwambia 'fanya uolewe sitaki kukuona nyumbani kwangu'

Kuna siku akaenda kazini kwa baba yake akamkuta yupo na wanaume wengine akawasalimia.
Kijana mmoja akamwambia mzee wake kwamba hakujua kama ana binti mkubwa vile! Mzee wake akajibu 'Huyu ni binti yangu kamaliza chuo mwaka huu na bado hajaolewa' wote wakaishia kucheka.

Haikupita miezi mingi baba yake akamletea mchumba, ubani ukachomwa sasa hivi yupo kwenye ndoa.

Nilichokiona wazazi wengi ambao hawajajipata kazi wanayotupa watoto wa kike ni kuolewa tena kama mtoto hajapata kazi ya kufanya.

Ila ukiwa na kazi nzuri unapata pesa, hii risala ya kuolewa hawatoi hata ukifikisha miaka 40.

Sasa sijui wa kulaumiwa ni CCM, wazazi wetu au sisi watoto.
Huwenda hujaelewa wazazi walikua wanakusudia nini.
Haimaanishi wao walikua wana uoga wa maisha juu yako.Bali wana uoga wa heshima ya binti yao.
Na kukaa kwao kimya haimaanishi kwamba hawana hilo wazo.

Sasa juu yenu muendelee kutafunwa kama bubble gum ama mtulie na mchi mmoja.
Maana leo gwede kesho Lucas Mwashambwa .
 
Ushauri ulikua mzuri mpaka pale ulipomtaja Guede na Lucas
 
Hivyo ni vibwagizo.
Ila hujachelewa sana 37 years dadeqi duuh😂😂😂😂.
Ndoa ina maana yake,maana tafiti zinaonesha watu wazima kuanzia miaka 35 kwenda juu wana upweke sana.
 
Sasa mimi nina 37 ila upweke sina najiona kama myoto wa miaka 9😂😜
Aaah wapi tusidanganyane😂😂😂.
Kuna muda ukijitizama cowgirl alone lamamaye 😂😂😂 halafu ukicheki sio official Mrs yeyote upweke must.
Kuna muda unakuja unconditionally.
 
Una hoja usikilizwe!😂
 
Na nyie mpo, Asha alikua anasisitizwa na baba yake aolewe hadi mchumba akamtafutia
Basi baba Asha anamatatizo mazee....
Mie binti zangu nawasisitiza kutunza afya, kumuhofia Mungu, bidii na nidhamu katika kila watakalo barikiwa kuwapatia rizki na pia kuheshimu watu wote wakubwa kwa wadogo.
 
Mama yako ana hekima sana.
Mabinti wengi baada ya kumaliza vyuo na kubaki nyumbani bila kuolewa hudinywa sana na kupelekea kei zao kutanuka haswa na pindi waolewapo mimba huwa zinatoka au mambo ya bed rest hadi muda wa kujifungua.

Naomba namba ya mama yako nimpongeze mkubwa mwenzangu,mm ni mstaafu wa umma,nina deserve kuongea na mama yako muda wowote.
 
Back
Top Bottom